Vatican yapongeza mashirika ya kitawa yanayoendesha shule licha changamoto!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Shukrani kwa wale wote wanaotoa rasilimali bora za maisha kwa utume muhimu wa elimu ambao wameitiwa, kwa walimu na kwa wafanyakazi wote wa utawala na utumishi, ambao wanakuwa kama nyuzi za rangi tofauti zilizofumwa pamoja na familia zote ambazo, zikitumia uwezo wa elimu wa jumuiya ya Kikristo, huwalea wana na binti zao katika ushirikiano wa kielimu na shule za Kikatoliki, zilioneshwa katika barua iliyotiwa saini na Kardinali Braz de Aviz, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya kitawa na vyama vya Kituma pamoja na Kardinali de Mendonça, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu, kwa watu wote na taasisi zinazohusika na elimu ya Kikatoliki.
Mkataba wa kimataifa kati ya chuo kikuu na huduma ya kichungaji
Mkataba wa kimataifa kati ya chuo kikuu na huduma ya kichungaji ili kukuza utamaduni wa familia ndiyo ilikuwa kauli mbiu ambayo ukumbusho wa kile kilichotokea mnamo tarehe 22 Mei 2023 iliyopita, wakati baadhi ya wahusika wakuu wa mtandao wa ulimwengu wa shule za Kikatoliki walipoalikwa Vatican,ili waweze kujieleza wenyewe uwezekano na changamoto za utume wa elimu katika msimu wa historia. Mkutano ulioandaliwa na mabaraza hayo mawili katika kukubali pendekezo la Papa Francisko la kusikilizana kati ya miimili ya Kanisa Takatifu na kwa sababu sehemu kubwa sana ya shule zaidi ya 240,000 za Kikatoliki zinazolifanya Kanisa kuwa miongoni mwa wahusika wakuu wa elimu ya msingi na sekondari duniani inaongozwa na Taasisi za Watawa na Mashirika ya vyama vya Kitume.
Shukrani kwa maaskofu pia na taasisi za kitawa
Kwa sababu hiyo, shukrani pia ziliwaendea maaskofu, majimbo na taasisi za watawa ambao, pamoja na wadau wengine, wamejenga mtandao mkubwa, wakitaka mtu yeyote asitengwe kwenye ngoma ya maisha. Kwa mujibu wa barua hiyo, wakati wa mkutano huo, matatizo makubwa ya sekta pia yalijitokeza. Baadhi wana ulimwengu wote kwa pamoja kama vile athari za janga la Uviko, msukosuko wa uchumi wa ulimwengu, kushuka kwa kiwango cha kuzaliwa, umaskini na kukosekana kwa usawa kwa upatikanaji wa chakula, maji, afya, elimu, habari, utamaduni na mtandao. Wengine badala yake wanajali angalau katika baadhi ya nchi, ukosefu wa kutambuliwa na mfumo wa sheria wa usawa wa kiuchumi wa shule zisizo za serikali, pamoja na kupungua kwa miito na hasa katika ulimwengu wa Magharibi, imani kwa Mungu inabakia kutengwa sana kutoka katika maisha ya umma na, kwa ujumla zaidi, kutoka kwa maisha ya wanaume na wanawake wa wakati wetu.
Kuna haja ya kuhifadhi matumaini
Hii ina athari za kiutendaji kwa kufungwa kwa baadhi ya shule. Kwa hakika, “pale ambapo kijimbo au shule ya za kitawa zinafungwa, alama za historia ya Kanisa moja la mahalia, la uzuri usio na shaka ya familia hiyo ya kidini, inafutiliwa mbali katika mazingira ya elimu. Mahali panapobainisha na kuhifadhi sehemu ya matumaini na katika baadhi ya matukio, hufanya usemi wa utambulisho wa Kikristo na Kikatoliki katika mazungumzo lakini thabiti, njia thabiti lakini ya kirafiki kuwa ngumu zaidi”, inabainisha barua hiyo.
Fursa ya hatua ya mbele katika ubunifu na uwezo wa kushirikiana kwa siku zijazo
Barua hiyo inasisitiza kwamba kwa bahati mbaya, “zaidi ya hayo, nyakati nyingine shule za Kikatoliki hufanya kazi katika eneo lile lile si kama waimbaji pekee ambao, kwa shukrani kwa sauti yao ya sauti ya pekee, hutajirisha kwaya nzima, lakini kama sauti nje ya kwaya, zilizotengwa, bila muktadha; katika baadhi ya matukio hata katika mashindano yasiyo na maana”. Kwa sababu hiyo, “ili kuchukua fursa ya kuchukua hatua mpya mbele ni muhimu, na haraka, kwa watendaji wote wanaohusika kuungana pamoja. Katika suala hilo baria unahimizia kuanzisha mipango ya mwendo, hata ya asili ya majaribio, yenye nguvu ya mawazo na ubunifu, yenye uwezo wa kushirikiana na siku zijazo, sahihi katika uchunguzi na hewa katika maono. Hofu ya hatari haizimi ujasiri; kwa hakika mgogoro si wakati wa kuweka kichwa mchangani, bali ni kuangalia nyota”.