Geneva,Ask.mkuu Putzer:uhamiaji husababishwa pia na mabadiliko ya tabianchi!
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Vatican inazingatia ripoti ya Mwandishi Maalum juu ya uhamasishaji na ulinzi wa haki za binadamu katika muktadha wa mabadiliko ya tabianchi. Kama ilivyosisitizwa na Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican katika uingiliaji kati wa hotuba yake wakati wa Mkutano wa COP27 , 2022, kwamba: “uso wa kibinadamu wa dharura ya hali ya tabianchi unatupatia changamoto kubwa” na tuna jukumu la kimaadili kushughulikia athari zake za mara kwa mara na nzito za kibinadamu, hasa uhamaji wa kulazimishwa. Hayo yalisemwa katika hotuba ya Askofu Mkuu John Putzer, Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kimataifa huko jijini Geneva, Uswiss katika Kikao cha 53 cha Kawaida cha Baraza la Haki za Kibinadamu, mnamo tarehe 28 Juni 2023. Katika Hotuba hiyo, mwakilishi wa Vatican alibainisha kuwa “Uhamishaji unaweza kutokea baada ya vichochezi vya kuanza kwa haraka au michakato ya kushuka polepole, lakini shida ya hali ya tabianchi inaweza pia kuwa kichocheo kisicho cha moja kwa moja cha uhamaji, kuzidisha mvutano wa kijamii na kusababisha migogoro juu ya rasilimali chache. Papa Francisko amerudia kushutumu kuongezeka kwa kutisha kwa idadi ya wahamiaji wanaotaka kukimbia kutokana na umaskini unaoongezeka, na unaosababishwa na uharibifu wa mazingira, na ambao hawatambuliwi na mikataba ya kimataifa kama wakimbizi.”
Vatican inakaribisha mbinu za kitaifa kikanda na kimataifa
Mwakilishi wa Vatican kwa kuonezea alisema "Ijapokuwa Vatican inakaribisha mbinu zinazoendelea za kitaifa, kikanda na kimataifa za kisheria na sera za kushughulikia uhamishaji wa hali ya tabianchi, Vatican inasikitika kwamba hawa mara nyingi hawana maono na kusukumwa na wasiwasi wa kiuchumi, na kuongeza hatari ya unyonyaji, unyanyasaji na ubaguzi. Kwa maana hiyo, mwalikishi wa Vatican alisisitiza kwamba Vatican inapenda kuwahimiza wajumbe wa Baraza hilo kulinda haki msingi za binadamu za wahamiaji na watu wengine walioathiriwa na mabadiliko ya tabianchi, huku wakijenga mifumo ya kisheria inayolengwa ipasavyo. Akiendea na hotuba yake alisema kwamba “ingawa mabadiliko ya tabianchi yanazidi kuathiri kila mtu, maumivu makubwa zaidi ni kuhisiwa na wale ambao wamechangia kwa uchache zaidi. Kwa hakika, inaathiri isivyo uwiano katika nchi za kipato cha chini na zinazoendelea, ambazo hazina rasilimali za kukabiliana na matokeo yake pekee. Kwa hiyo, Vatican inaitaka Jumuiya ya Kimataifa kufanyia kazi mwitikio wa pamoja na ulioratibiwa kwa moyo wa mshikamano, kwa kuweka utu wa binadamu na huduma kwa nyumba yetu ya pamoja kuwa kiini cha juhudi zake zote”, alihitimisha.
Kikao kuhusu haki za kupata elimu huko Geneva 27 Juni 2023
Na wakati huo huo katika kikao cha 53 cha kawaida cha Baraza la Haki za Binadamu kuhusu haki ya kupata elimu, kilichofanyika mnamo tarehe 27 Juni 2023, Mwalikishi wa kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa huko Geneva Uswiss alitoa Hotuba yake kuhusiana na “Mazungumzo ya Maingiliano na Mwandishi Maalum kuhusu haki ya elimu”. Akianza hotuba hiyo alisema kwamba “ Vatican inazingatia Ripoti ya Mwandishi Maalum kuhusu haki ya elimu pamoja na maadhimisho ya miaka 25 ya mamlaka ya haki ya elimu. Katika ripoti yake, Mtaalamu Maalum alielezea jinsi migogoro mingi inayoathiri elimu pia inatoa fursa mpya za mageuzi, ushirikiano wa pande nyingi, na mkataba mpya wa kijamii. Elimu zaidi ya shule pekee ni muhimu kwa maendeleo fungamani ya binadamu kwa wote.
Pendekezo la Papa Francisko la Mkataba wa Elimu kimataifa wa 2019
Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwa hiyo alisisitiza kuwa “Vatican inakaribisha wito wa Mwandishi wa usaidizi zaidi kwa aina zinazofaa za elimu ya awali, ya kiufundi, na ya watu wazima ili kuwasaidia watu hao kukuza ujuzi wao, kupata taarifa na kupokea elimu ambayo ingewasaidia katika njia yao.” Kiukweli, alisema kwa kutambua hitaji la mbinu muhimu ya elimu, mnamo 2019 Papa Francisko alitoa wito wa kuwepo kwa Mkataba wa Kimataifa wa Elimu, huku akibainisha kwamba “hapo awali kumekuwa na haja kama hiyo ya kuunganisha juhudi zetu katika muungano mpana wa elimu, kuunda watu waliokomaa wenye uwezo wa kushinda migawanyiko na uadui, na kurejesha muundo wa mahusiano kwa ajili ya ubinadamu wa kidugu zaidi.”Kwa hiyo Vatican “inabainisha kwamba baadhi ya malengo ya kiutendaji yaliyoainishwa katika ripoti yanaweza kusaidia kuchangamsha juhudi hizo”, alisisitiza Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Umoja wa Mataifa.
Elimu ya mtoto ielekezwa kwenye ukuaji wa heshima kwa wazazi wa mtoto, utamaduni, lugha na maadili
Hata hivyo Vatican lazima ieleze wasiwasi wake kwa madai ya ripoti hiyo isemayo kuwa “ Mahitaji kutoka kwa wazazi na jamii kwamba watoto wazuiwe kutoka katika maudhui fulani ya elimu (...) yatakinzana na haki ya kupata elimu” (kifungu cha 50). Kwa bahati mbaya, madai hayo yanapingana na kifungu cha 29, c), ya Mkataba wa Haki za Mtoto, ambayo inathibitisha kwamba: “elimu ya mtoto itaelekezwa kwenye: Ukuaji wa heshima kwa wazazi wa mtoto, utamaduni wake mwenyewe, utambulisho, lugha na maadili, kwa ajili ya tunu za taifa za nchi anamoishi mtoto, nchi anayotoka, na kwa ustaarabu tofauti na wake mwenyewe maendeleo ya heshima kwa wazazi wa mtoto, utambulisho wake wa kiutamaduni”lugha ya Papa Franvisko, Ujumbe wa Uzinduzi wa Mkataba wa Kimataifa wa Elimu, tarehe 12 Septemba 2019 na maadili, na kwa maadili ya kitaifa ya nchi ambayo mtoto anaishi”. Kwa kuongezea, Mkataba huo unalinda haki na wajibu wa wazazi katika kuwaelekeza watoto wao katika utekelezaji wa haki zao za uhuru wa mawazo, dhamiri na dini Waelimishaji na taasisi za elimu wanapaswa kutafuta kutofuta au kudharau utamaduni na maadili ya jumuiya yao. Kinyume chake, ushirikishwaji wa kweli unaheshimu hisia za kiutamaduni na utofauti.
Ujumuisho wa kweli unapaswa kuwatazama walio dhaifu
Vile vile ni kuwekwa katika ajenda inayofanana, isiyobadilika na isiyovumilika kiukweli ni aina ya ukoloni wa kiitikadi, ambao, kwa maneno ya Papa Francisko, unapingana na ukweli wa maisha, huzuia kushikamana kwa ajili ya watu na maadili yao, na kujaribu kung'oa mila zao, historia na uhusiano wa kidini.Mtazamo huu, unaofikiri kwa kimbelembele kwamba kurasa za giza za historia zimeachwa nyuma, huwa wazi kwa ‘utamaduni wa kufuta’ ambao ungehukumu yaliyopita kwa misingi ya kategoria fulani za kisasa. Matokeo yake ni mtindo wa kiutamaduni ambao huweka kila kitu nje, hufanya kila kitu kuwa sawa, huthibitisha kutovumilia tofauti na kuzingatia wakati uliopo, juu ya mahitaji na haki za watu binafsi, huku mara kwa mara wakipuuza wajibu wao kuhusu wale walio dhaifu na walio hatarini zaidi.” Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican kwa hiyo alisema kuwa “Ujumuisho wa kweli, kama lengo halali la elimu, unapaswa kutuchochea badala yake tukubali, kwa subira na azimio, michakato ya kielimu inayotoa njia bunifu na za uwajibikaji za ukomavu wa binadamu kwa wote, huku tukiheshimu utu wa asili wa kila mwanamume na mwanamke, mvulana na msichana,” alihotomisha.