Tafuta

Papa Francisko alikwenda Hospitalini Gemelli kwa ajili ya vipimo Jumanne 6 Juni 2023. Papa Francisko alikwenda Hospitalini Gemelli kwa ajili ya vipimo Jumanne 6 Juni 2023. 

Ziara fupi ya Papa huko Gemelli kwa uchunguzi wa kimatibabu

Papa Francisko alikwenda Hospitali ya Gemelli asubuhi Jumanne 6 Juni 2023 kurudi Vatican kabla ya saa sita mchana.Ni katika muktadha wa kufanya vipimo vya kimatibabu.

Vatican News

Baba Mtakatifu alirudi Hospatalini Gemelli  Roma,  lakini kwa wakati huu, ukilinganishwa na zaidi ya miezi miwili iliyopita, ilikuwa ni kwa ajili ya uchunguzi wa haraka wa kimatibabu. Haya yaliwasilishwa na Msemaji wa Vyombo vya habari katika Ofisi ya Waandishi wa Habari Vatican, Dk. Matteo Bruni, wakati  akijibu maswali ya waandishi wa habari na  kuripoti kwamba asubuhi tarehe 6 Juni 2023 Baba Mtakatifu  Francisko alikwenda Hosptalini Gemelli kwa ajili ya vipimo vya kliniki na akarudi Vatican kabla ya saa sita mchana.

Machi iliyopita Papa alilazwa hospitalini huko Gemelli

Ikumbukwe mnamo tarehe 29 Machi, iliyopita Baba Mtakatifu Francisko alikuwa amelazwa hospitali hiyo hiyo ya Gemelli Roma  kwa sababu ya ugonjwa wa bronchitis ya kuambukiza na aliruhusiwa baada ya siku tatu, mnamo tarehe Mosi Aprili 2023.

Papa amekwenda Gemelli kufanya vipimo na kurudi Vatican.
06 June 2023, 17:26