Tafuta

Kardinali  Matteo Zuppi, alitumwa tena huko Moscow, Urussi 28-29 Juni 2023 kwa kile kiitwacho "kutafuta njia za amani ya haki". Kardinali Matteo Zuppi, alitumwa tena huko Moscow, Urussi 28-29 Juni 2023 kwa kile kiitwacho "kutafuta njia za amani ya haki".  (ANSA)

Moscow,Kard Zuppi:kutafuta nji za amani ya haki

Kardinali Zuppi akiwa Moscow Urussi kama alivyoombwa na Papa kwa siku mbili 28 na 29 Juni,alizungumza na Yuri Ushakov,Mshauri wa rais kwa ajili ya masuala ya Nchi za Nje,alikutana na Maaskofu katoliki katika Ubalozi wa Vatican,Marija L'vova-Belova, Kamishna wa haki za watoto,pia na Patriaki Kirill hatimaye Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mama wa Mungu.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Rais wa Baraza la maaskofu Italia (CEI) na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki, la Bologna, Kardinali Matteo Maria Zuppi, kama alivyotumwa na Baba Mtakatifu katika siku mbili za 28 na 29 Juni 2023 ili kutafuta “njia za amani ya haki” akiwa huko Moscow nchini Urussi, picha ya kwanza na ya kipekee iliyojionesha ilikuwa ni kupiga   magoti yake mbele ya picha ya Bikira Maria. Ni sanamu ya Mama wa Mungu wa Vladimir, anayejulikana kama Bikira wa Huruma. Ni picha ya zamani sana ya Bikira Maria nchini Urussi, iliyohifadhiwa kwenye Jumba la sanaa la Tretyakov, karibu na Kremlin. Kwa Kardinali ilikuwa ni maombi ya kwanza kabisa katika utume wake  katika  hatua yake ya  pili baada ule wa jiji la Kyiv nchini Ukraine iliyofanyika mnamo tarehe  5-6 Juni 2023 ambapo katika hafla hiyo, Kardinali alikutana na rais wa nchi hiyo Volodymir Zelensky.

Kardinali Zuppi alikutana na Kamishna wa haki za watoto Urussi
Kardinali Zuppi alikutana na Kamishna wa haki za watoto Urussi

Akiwa mjini Moscow tarehe 28 Juni 2023, Kardinali Zuppi alipokelewa na Yuri Ushakov, mshauri wa masuala ya sera za kigeni wa Rais Vladimir Putin,  mwenye umri wa miaka 76,  na ambaye aliwahi kuwa balozi wa Urussi  nchini Marekani kuanzia mwaka 1998 hadi 2008. Mahojiano yaliyohusu mzozo wa Ukraine na njia zinazowezekana za kisiasa na sera za suluhisho la kidiplomasia. Hii ndiyo iliripotiwa na mashirika ya Kirussi, ikiwa ni pamoja na Interfax ambayo iliripoti maoni ya msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov katika hatua ya waandishi wa habari tarehe 28 mara  baada ya mkutano wa Kardinali Zuppi na Ushakov kwamba:  “Kwa ujumla, tayari tumeeleza mara kadhaa kwamba tunathamini sana jitihada na mipango wa Vatican kutafuta suluhisho la amani kwa mgogoro huo na tunakaribisha ushauri  huu wa Papa kusaidia kumaliza mzozo wa kijeshi nchini Ukrain.” Alasiri hiyo  Kardinali Zuppi pia alikutana na maaskofu wa Katoliki wa Urussi kwenye makao makuu ya Ubalozi Vatican  akiongozwa na Askofu Mkuu Giovanni D'Aniello. Kardinali Zuppi aidha akiwa Moscow alifanya mkutano kati ya mwakilishi wa serikali waliojitolea kutetea haki za watoto. Kipaumbele kikubwa zaidi kilikuwa ni juu ya suala la zaidi ya watoto 19,000 wa Kiukraine waliopelekwa nchini Urussi, suala ambalo  hata Rais Zelensky aliomba usaidizi wa Vatican  katika Mkutano wake na Baba Mtakatifu Francisko mwezi Mei uliopita.

Kardinali Zuppi wakati anasali mbele ya Picha ya Mama Maria wa Huruma
Kardinali Zuppi wakati anasali mbele ya Picha ya Mama Maria wa Huruma

Mara baada ya Kukutana na Patriaki wa Moscow, ikiwa ni siku yake ya pili na ya mwisho, wa utume pamoja na kukutana na Marija L'vova-Belova, Kamishna wa Kremlin wa haki za watoto, Kardinali Zuppi alikuwenda katika Kanisa Kuu la Mama wa Mungu na kuongoza misa Takatifu katika Maadhimisho ya Siku Kuu ya Mtakatifu Petro na Paulo. Katika mahubiri yake, Kardinali Zuppi alisema siku hiyo ilikuwa ni kuwa kuwakumbuka mitume wawili watakatifu, walioungana kama utangulizi ulivyosema katika udugu wenye furaha: Petro, ambaye alikuwa wa kwanza kukiri imani yake katika Kristo, Paulo, aliyeangazia undani wa fumbo; mvuvi wa Galilaya, aliyeunda jumuiya ya kwanza pamoja na wenye haki wa Israeli, mwalimu na daktari, aliyetangaza wokovu kwa watu wote. Hivyo, kwa karama mbalimbali, walijenga Kanisa moja, na kuhusishwa katika ibada ya watu wa Kikristo wakishiriki taji moja ya utukufu.

Picha ya Pamoja baada ya mazungumzo
Picha ya Pamoja baada ya mazungumzo

Ni furaha iliyoje udugu wao na wetu, katika dunia yenye migawanyiko mingi, kwa upweke mchungu zaidi kwa sababu unatufanya tupotee katika bahari kuu ya utandawazi! Petro na Paulo ni tofauti. Imani ya unyenyekevu na thabiti ya Petro kama mwamba na moyo mpana na wa umisionari wa Paulo”, alisisitiza Kardinali Zuppi. Kardinali Zuppi aidha katika mahubiri yale alisema: “Kanisa halifanyi kuwa sawa, bali umoja, tofauti bali kwa pamoja. Mungu ametufanya kuwa wa kipekee, usioweza kurudiwa, na uwezo wa asili katika kila nafsi, ambayo hupata kile inachotafuta inapofikia ushirika na Mungu na jirani. Sisi ni wa kipekee kwa sababu tumeumbwa kupendana na sisi sote tunahitaji kufunguliwa na uovu na ili kufungwa katika upendo. Mitume hao wawili wameunganishwa vya kutosha kukumbukwa pamoja. Mkristo kamwe hajatengwa, hajifikirii peke yake, hayuko peke yake.

Kardinali Zuppi akihubiri 29 Juni 2023
Kardinali Zuppi akihubiri 29 Juni 2023

Umoja ni tunda la Injili unayotufundisha kuifikiria pamoja. Umoja hautolewi kwa nguvu bali kwa kuhudumiana; si kutokana na mahusiano ya damu bali kutoka kwa yule aliyetokezwa na Mungu anayetufanya kuwa watoto wake, sehemu ya familia yake. Umoja Kardinali Zuppi alikazia kusema kuwa unahitaji ushirika na hii daima inahusisha kila mtu na kila kitu cha kila mtu. Hatupaswi kamwe kuacha kuitafuta, kwa sababu mgawanyiko hukua kwa kutojali, huingia kwenye upendo mdogo. Mgawanyiko huo wakati mwingine hulisha sababu za moja dhidi ya zile za mwingine, kiasi kwamba zinakuwa fundo lililofungamana hivi kwamba inaonekana haiwezekani kulifungua. Mgawanyiko siku zote ni kashfa kwa Yesu, ambaye anaomba kwamba watu wake wawe kitu kimoja, yaani, wafikiriane wao kwa wao. Yesu anafundisha kila mtu kuwa jirani kwa mwenzake kwa sababu tunajifunza kwamba sisi sote ni Ndugu! Ushirika ni kifungo cha upendo kinachotuunganisha.

Misa katika Kanisa Kuu la Mama wa Mungu huko Moscow
Misa katika Kanisa Kuu la Mama wa Mungu huko Moscow

Ni wa mzunguko ambao unatusaidia kuwa bora zaidi kwa sababu unatufanya tufikirie wengine. Petro aliongoza katika ushirika na ambaye mamlaka yake ni daima na yale tu ya kuwa mtumishi wa watumishi. Kwa njia hiyo alisema “ hatukosi kamwe kuonesha ukaribu na msaada kwa mrithi wa Petro, Askofu wa Roma, kwa sababu ushirika daima unahitaji huduma hii tete na ngumu. Hakuna anayeachwa peke yake. Yeyote anayemfuata Yesu daima anaongozwa kwenye udugu mpya. Daima tuna kaka. Wa kwanza ni Yesu hasa, anayetutafuta, anatuita, hatuachi peke yetu, anakaa nasi kila siku, hata anahesabu nywele za vichwa vyetu, analisha mwili wetu. Lakini yeyote anayekutana na Yesu anakutana na Mama yake Kanisa akiwa na furaha na watoto wengi sana, ambapo udugu haubaki kuwa halisi, wa mfano, bali unachukua aina halisi za uzoefu wetu wa kibinadamu”.

Misa katika Kanisa Kuu huko Moscow
Misa katika Kanisa Kuu huko Moscow

“Yesu kutoka msalabani  alitukabidhi kwa mama yake na yeye kwetu! Ni mama yake ambaye anakuwa wetu kwa sababu tumezaliwa kama Yesu, watoto wa Mungu. Kanisa si takatifu peke yake. Linajumuisha wenye dhambi ambao wote daima wanahitaji huruma ya Mungu. Kuipenda kunamaanisha kuitumikia na kutoitumia; ifanye kuwa mahali pa upendo pasipo maafikiano, ya kindugu kweli, bila ya kujifanya, unafiki na maslahi ya bure, isiyo na hukumu za ulimwengu. Kulipenda Kanisa kunahitaji utakatifu wetu binafsi, yaani, upendo ambao Mungu anatupatia na kwamba hatupaswi kujiwekea wenyewe vinginevyo tunaupoteza na kuwafanya wengine kuukosa. Kanisa lina umoja lakini haliishi lenyewe. Linaitwa lakini limetumwa. Haliwi klabu, kikundi cha kujisaidia, lakini ni zaidi ya hayo maana ni familia na husaidia wengine. “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri Injili kwa watu wote,” aliwaomba.  Na Petro na Paulo walifika Roma.  Petro anatukumbusha juu ya umoja. Paulo kutangaza Injili kwa wote. Petro ni wito na kufuasa,” alisisitiza Kardinali Zuppi.

Wakati wa matoleo ya Misa Takatifu 29 Juni 2023
Wakati wa matoleo ya Misa Takatifu 29 Juni 2023

Paulo alitoka na kumfuata Yesu kupitia njia za ulimwengu. Tunawasilisha Injili kwanza kabisa na maisha yetu kwa sababu tutatambuliwa kwa jinsi tunavyopendana na jinsi tunavyopenda jirani zetu. Hivyo Injili ya Yesu inajibu maswali mengi kuhusu wakati ujao ambayo yanasumbua kizazi chetu na shauku ya kutafuta wakati ujao. Sisi sote tumeitwa kuwa mitume, watenda kazi katika mavuno, watu wenye moyo mpana, wa ulimwengu wote, wenye uwezo wa kusema na kila mtu na wa kusaidia Kanisa la Mungu, mama wa watu wote.” Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI) kwa hiyo akiendelea na mahuburi hayo alisema “Kama mama, Kanisa kamwe haliwezi kukubali mgawanyiko kati ya watoto. Yeye ni mama na daima hutafuta amani kwa subira na uthabiti ili kurudisha yale mabaya ambayo yamegawanyika. Kama Mama, Kanisa linaomba bila kukoma zawadi ya amani, ikitafuta bila kuchoka kwa sababu maumivu ya kila mtu ni maumivu yake. Sio ujinga: hukumbuka na haichanganyi majukumu, hutengeneza fursa za shida kwa upendo, hupanda mema kupigana na uovu na kurejesha haki, huweka matumaini katika giza la giza, husuka kitambaa cha amani na udugu, kwa vurugu kutokana na chuki na kutoaminiana.

Waamini ndani ya Kanisa Kuu la Mama wa Mungu huko Moscow, Urussi
Waamini ndani ya Kanisa Kuu la Mama wa Mungu huko Moscow, Urussi

Yeye ni mama. Hii ndiyo sababu pekee ya utume tunaoishi siku hizi, unaotafutwa na mrithi wa Petro ambaye hakati tamaa na anajaribu kufanya kila kitu ili matarajio ya amani itokayo duniani yapate kutimizwa hivi karibuni.  Kardinali Zupp alifafanua kuwa tarehe 28 Juni alimkabidhi utume huu kwa Mama wa Vladimir, ili huruma yake kwa wanadamu waliojeruhiwa na wanaoteseka isaidie kutafuta njia ya amani kwa akili na ujasiri, kwa ubunifu na uaminifu. “Upole huanza kwa watoto, kwa watoto wadogo, kwa walio hatarini, na wahaathiriwa wasio na hatia wa unyanyasaji usio wa haki, wakubwa zaidi kuliko wao, usiokubalika hata zaidi kwa sababu unahusisha wale ambao hawawezi kujitetea. Maumivu yao, ambayo mara nyingi yamefichwa kwenye vidonda virefu vya moyo, yanahitaji kujitolea kwa kila mtu kupata faraja na ulinzi. Sio ndoto isiyo na maana, lakini nia ya kibinadamu na ya Kikristo na wajibu, muhimu kwa siku zijazo kuwepo”. Kardinali Zuppi alitoa maombi yake kwamba “Amani na haki hulishana na kuhitajiana. Utufundishe, Bwana, kukiri imani kwako kama Petro, kupenda umoja na kutangaza Injili kwa wote, kukutambua kuwa wokovu wetu ambao hakuna mtu atakayeweza kututenga na kuwa mawe hai ya    Kanisa ambalo huwaweka huru wanadamu. kutoka kwa upendo kwa nafsi yake mwenyewe na kuwafunga katika kifungo cha milele cha upendo. Kwa sababu Wewe ni Mwana wa Mungu kweli, amani yetu na tumaini letu,”alihitimisha Kardinali Zuppi.

Utume wa Kardinali Zuppi huko Moscow Urussi
30 June 2023, 16:01