Tafuta

Askofu mkuu George George Panamthundil, Balozi mpya wa Vatican nchini Kazakhstan Askofu mkuu George George Panamthundil, Balozi mpya wa Vatican nchini Kazakhstan 

Askofu mkuu George George Panamthundil kuwa Balozi wa Vatican nchini Kazakhstan

Askofu mkuu mteule George George Panamthundil alizaliwa tarehe 20 Mei 1972 huko, Trivandrum City nchini India. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 18 Februari 1998 akapewa daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Trivandrum Madhehebu ya Siro‑Malankaresi. Baadaye alijiendeleza kwa masomo na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu kwenye Sheria za Makanisa ya Mashariki. Tarehe 1 Julai 2005 akaanza utume wake wa diplomasia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo George George Panamthundil kuwa Balozi wa Vatican nchini Kazakhstan na kumpandisha hadhi na hivyo kuwa ni Askofu mkuu. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule George George Panamthundil alizaliwa tarehe 20 Mei 1972 huko, Trivandrum City nchini India. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 18 Februari 1998 akapewa daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Trivandrum Madhehebu ya Siro‑Malankaresi.  

Papa Francisko akiwa Kazakhstan
Papa Francisko akiwa Kazakhstan

Baadaye alijiendeleza kwa masomo na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu kwenye Sheria za Makanisa ya Mashariki. Tarehe 1 Julai 2005 akaanza utume wa diplomasia ya Kanisa na hivyo kupelekwa nchini Costa Rica, Guinea, Iraq, Austria, Israeli na Mwakilishi wa Kitume mjini Yerusalem, Palestina na huko nchini Cyprus.

Kazakhstan
18 June 2023, 14:17