Wasiwasi wa Vatican kuhusu ghasia nchini Sudan
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Katika Ujumbe kutoka kwa Mwalikishi wa Kudumu wa Vatican katika Ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva ameonesha wasiwasi wake mkubwa kutokana na hali mbaya ya migogoro na vurugu inayoendelea nchini Sudan. Katika hotuba yake iliyotolewa tarehe 11 Mei 2023, katika Kikao Maalum cha 36 cha Baraza la Madiwani kuhusu athari za haki za binadamu za vita vinavyoendelea katika nchi ya Kiafrika, na ongezeko la mateso ya watu, Vatican inapenda kuhakikisha ukaribu wake wa kiroho, sala zake na mshikamano wake na watu wa Sudan, hasa waliohamishwa na wakimbizi.”
Kwa hiyo Wasiwasi mkubwa hasa ni atahari za kibinadamu za mzozo na hivyo Vatican inatoa mwaliko unaoelekezwa kwa wahusika wote, kusimamisha mashambulizi ya silaha na kuhakikisha upatikanaji wa zana msingi na muhimu kwa raia, popote zinapohitajika, ambayo inajumuisha uwezekano wa kusambaza usaidizi wa kibinadamu wa usalama. Kuhusiana na hilo hata hivyo Vatican ina matumaini ya kwamba makubaliano yanaweza kurefushwa na kuheshimiwa kikamilifu na kwamba mazungumzo kati ya wawakilishi wa pande zote zinazozozana na kuweza kuleta makubaliano yenye tija kwa usitishaji vita na masuluhisho ya amani na ya kudumu, kwa maslahi ya idadi ya watu wa Sudan, pamoja na kuepuka hatari ya kuenea kwa ghasia katika nchi jirani, na kudhoofisha amani na usalama wa kikanda.
Kwa kuhitimisha ujumbe wake mwakilishi wa Kudumu wa Vatican anabainisha uhakika wake kwamba “mazungumzo, katika roho ya udugu, yanaweza kuleta muafaka wa amani ya haki na ya kudumu. Kwa hiyo, ombi la Papa Francisko linasisitizwa tena la kuombe kweka sialaha chini na kuanza tena njia ya amani na maelewano pamoja.