Tafuta

Tume ya  Kipapa ya Uliniz wa watoto imehitimisha Mkutano wake Tume ya Kipapa ya Uliniz wa watoto imehitimisha Mkutano wake 

Ulinzi wa watoto,mikakati mipya dhidi ya unyanyasaji.

Mkutano wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto jijini Roma umehitimishwa.Mada zilikuwa ni kusasisha miongozo ya Mafundisho ya Imani ya 2011 iliyoingia katika makubaliano na ubia kwa ajili ya mafunzo na ulinzi,kuimarisha kujitolea kupambana na waalifu wanaopenda watoto mtandaoni.Kardinali O'Malley:“Papa ametuomba mengi na sisi sote tumejitolea kufanya hivyo.”

Na Angella Rwezaula, - Vatican.”

Mfumo mpya wa ulimwengu wote, kusasisha miongozo ya Mafundisho ya Imani miaka kumi na miwili iliyopita; Mfuko wenye michango kutoka katika Mabaraza ya Maaskofu kwa ajili ya malezi na usaidizi wa waathiriwa, ushirikiano na Mfuko wa  GHR kwa ajili ya programu za ulinzi wa watoto; mikakati ya kukabiliana na unyanyasaji wa watoto mtandaoni; utafiti wa kina juu ya mada ya mazingira magumu katika aina zake mbalimbali; mpango mkakati wa kuweka mahitaji ya wahanga na waathirika katikati na kuyashughulikia katika taratibu za kuripoti za Kanisa. Ndizo nguvu, mawazo na raslimali zilizotumiwa na wajumbe wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto wakati wa mashauriano ya kuchambua na kufafanua kazi ya sasa na ya siku zijazo, kwa kuzingatia mwaliko mpya wa Papa wa kuendelea kufanya kazi katika kuboresha viwango vya maadili na kulilinda Kanisa dhidi ya uhalifu wa kutisha wa unyanyasaji wa kijinsia.

 Papa: Tume sikate tamaa

Kiungo cha  tume kilichoanzishwa  mnamo mwaka 2014 na Praedicate Evangelium ikiingizwa ndani ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa kilihitimisha kikao chake, kilichoanza  tarehe 3 Mei  katika Juna la   Maffei Marescotti huko Roma. Licha y a kua kadiri ya miaka ilivyo kwenda na hata baadhi ya wajumbe kujiuzulu kurekodiwa lakini hivi karibunu, wanachama wapya kumi wametajirisha tangu Novemba 2022. Kwa hiyo Wanachama wote, wakiongozwa na Askofu Mkuu wa Boston Marekani, Kardinali Sean O'Malley, walipokelewa  tarehe 5 Mei  2023 na Papa, ambaye akilaani katika hotuba yake kutoweza kuchukua hatua za kutosha za kukomesha uovu huu na kusaidia waathrika wake na pia kuwanyanyapaa, dhambi za kuacha, ambazo si mbaya zaidi kuliko vurugu za wanyanyasaji,  aliiomba Tume isikatishwe tamaa katika utume wake ambayo inawakilisha maono ya kimataifa ya jinsi Kanisa linaweza kuwa mahali salama zaidi kwa wote. Miongozi ya

Kanisa imesasishwa

Tume inashikilia dira hii na inaamini kwa dhati kwamba ahadi hizo lazima ziambatane na mabadiliko yanayoweza kuthibitishwa ndani ya Kanisa ambayo yanadhihirisha kwamba vijana na watu walio katika mazingira magumu hawako hatarini na kwamba jitihada zinafanywa kusimama pamoja na wale walioathiriwa na unyanyasaji wa mahusiano ya kingono”, wasema waamini hao katika taarifa, ambapo wanasema walikaribisha maneno ya Papa, pamoja na uthibitisho wa Motu Proprio Vos estis lux mundi kamasheria ya kudumu. Kwa kuzingatia mabadiliko haya na mialiko iliyofanywa upya, baadhi ya ubunifu na kile ambacho Kardinali O'Malley Rais wa Tume hiyo  alikifafanua kama marekebisho ya mbinu ya kufanya kazi , vilianzishwa katika kikao cha mashauriano. Awali ya yote, Miongozo ya Kanisa ilisasishwa, iliyotolewa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2011 na Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa wakati huo, ambayo  kama ilivyoombwa na Katiba ya Sasa ya Praedicate Evangelium  inahitaji kuzingatia sera za ulinzi katika Kanisa lote. Kwa hiyo Mfumo mpya wa Miongozo ya Kiulimwengu (UGF) ulitayarishwa na kupatikana kuanzia tarehe 31 Mei na utawasilishwa kwa viongozi wa Kanisa, vikundi vya waathirika na washikadau kwa kipindi cha maoni ya umma kabla ya kuidhinishwa kwa mwisho katika 'mwaka.

Mfuko wenye michango kutoka kwa Mabaraza ya Maaskofu

Sambamba na maelekezo ya Papa ambaye alisifu kazi ya Tume ya kusuluhisha ukosefu wa usawa katika nchi maskini zaidi ambapo waathrika huteseka kimya kimya bila rasilimali za kuripoti na kupata msaada, Mfuko uliundwa unaojumuisha michango kutoka kwa Mabaraza ya  Maaskofu. Lengo la Mfuko huo ni kutoa programu za kujenga uwezo ili kuhakikisha upatikanaji zaidi wa mafunzo na usaidizi kwa waathirika, familia zao na jamii katika sehemu maskini zaidi duniani. Mpango wa majaribio ulitiwa saini na Kanisa nchini Rwanda, na ili kulinda mfuko huo, itifaki ya utoaji wa fedha iliidhinishwa ambayo inasimamia matumizi ya michango iliyotolewa kama sehemu ya mpango wa kujenga uwezo. Jina ni Memorare. Makubaliano mbalimbali yaliwekwa basi na Tutela Minorum yaani Ulinzi wa Watoto. Moja ni ushirikiano na Mfuko wa GHR wa Marekani, ulioshirikishwa kwa mara ya kwanza na Tume mnamo Desemba mwaka 2022, ili kuendesha programu ya kutoa washauri wa ulinzi wa kikanda. Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu (DIHD)tayari ilikuwa imetumia ushirikiano sawa na Mfuko GHR kusaidia mwitikio wa Kanisa kwa janga la UVIKO-19. Pamoja na Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto, Mfuko wa GHR unasimamia uajiri, na malipo ya moja kwa moja ya wafanyakazi wa kikanda. Washauri wote walikuwepo kwenye kikao na pia walishiriki katika katekesi ya Papa.

Mkataba mwingine

Mkataba mwingine wa ushirikiano ni ule uliotiwa saini tarehe 21 Aprili 2023 na Baraza la Kipapa la Uinjilishaji ili kukuza malengo ya ulinzi kwa kazi ya ofisi ya Vatican inayosimamia maisha ya Kanisa katika zaidi ya nusu ya dunia. Mkutano huo uliagiza utafiti wa kina juu ya mada ya udhaifu katika aina zake mbalimbali, ili kuvipa vyombo vya Kanisa hatua madhubuti za kupambana na sekta hii inayoibuka ya nyanyaso. Pia wakati wa mkutano huo, Roma, mfumo wa marejeeo wa Ripoti ya Mwaka juu ya ulinzi wa sera na taratibu katika Kanisa, ulioombwa na Papa mnamo Aprili 2022 na kuthibitishwa tena katika kusikilizwa kwa mwisho, ulirekebishwa.  Kwa hiyo Mpango unachukua mbinu ya kubuni inayozingatia binadamu ambayo inazingatia jinsi mahitaji ya waathirika na waathirika yanaweza kupewa kipaumbele na kushughulikiwa katika mifumo ya taarifa ya Kanisa, kwa lengo la kutoa mapendekezo kwa Baba Mtakatifu jinsi ya kushughulikia mapungufu”, yanasomeka maelezo kutoka kwa Tume  ya Ulinzi wa Watoto. 

Rasilimali zinazohitajika

Kati ya mambo mapya, basi, kazi ya chombo cha uthibitishaji kitakachotumika kutathmini utoshelevu wa miongozo ya ulinzi wa makanisa ya mahalia na pia mikakati ya kujibu ombi la  Papa Francisko la kupambana na uovu wa unyanyasaji wa watoto mtandaoni. Hatimaye, mpango mkakati wa miaka mitano unaobainisha malengo, shabaha na viashiria vya utendaji ili kupima maendeleo na kuwajibika kwa wadau. Baba Mtakatifu amewaomba mengi na:  “sisi sote tumejitolea kuifanya ifanyike, alisesema Kardinali O'Malley huku, akisisitiza kwamba maendeleo haya yanawakilisha mabadiliko muhimu kuelekea mwelekeo unaozingatia athari zaidi kwa Tume. Kwa hiyo ni welekeo na wa haraka kwa sisi sote”. Kwa kuongezea , Kadinali huyo alisema: “Kasi hii ya kasi katika miezi sita iliyopita imesababisha maumivu ya kukua, kwani tumejaribu kujibu mahitaji ya muda mfupi na ya muda mrefu." Katika kikao hicho, baadhi ya marekebisho kulingana na "mbinu yetu ya kufanya kazi kwa hivyo yanatengenezwa, ili kufafanua majukumu yetu tofauti na kuunda hisia ya kuwa mali ya pamoja ya mamlaka yetu na jukumu letu la pamoja la utekelezaji wake". “Tumetafuta rasilimali zinazohitajika kujibu vya kutosha na tuna imani katika mpango tuliofafanua na kwa watu wanaofanya kazi nasi”, alihitimisha Kardinali  O'Malley. 

Rais wa tume ya Ulinzi wa watoto
09 May 2023, 16:43