Tafuta

kijana huyu alikuwa anakabiliwa na changamoto za afya ya akili. Kwa sasa amewekwa mahabusu, kwa ajili ya uchunguzi zaidi. kijana huyu alikuwa anakabiliwa na changamoto za afya ya akili. Kwa sasa amewekwa mahabusu, kwa ajili ya uchunguzi zaidi.  (ANSA)

Taharuki Kubwa Mjini Vatican Dereva Aingia Kwa Nguvu, Avuka Vizuizu Kwa Nguvu

Kijana alirudisha gari nyuma, na kuingia kwa nguvu zote, hali iliyowalazimisha walinzi wa Vatican kufyatua risasi kwenye gurudumu, lakini akaendelea na safari yake. Hali hii ilizua taharuki na hivyo vikosi vyote vya ulinzi mjini Vatican vikajiandaa kupambana naye kwa kufunga malango yote yanayoelekea Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Bustani za Vatican na hatimaye, kwenye Hosteli ya Mtakatifu Martha. Kwa sasa amewekwa mahabusu kwa uchunguzi zaidi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 40 ambaye anakabiliwa na changamoto ya afya ya akili, baada ya kusitisha kutumia dawa hivi karibuni, anashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama mjini Vatican, baada ya kutaka kuingia kwa nguvu mjini Vatican, baada ya kuzuiliwa kuingia kwa kukosa vitambulisho. Kijana alirudisha gari nyuma, na kuingia kwa nguvu zote, hali iliyowalazimisha walinzi wa Vatican kufyatua risasi kwenye gurudumu, lakini akaendelea na safari yake. Hali hii ilizua taharuki na hivyo vikosi vyote vya ulinzi mjini Vatican vikajiandaa kupambana naye kwa kufunga malango yote yanayoelekea Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Bustani za Vatican na hatimaye, kwenye Hosteli ya Mtakatifu Martha. Hayo yametendeka jioni ya tarehe 18 Mei 2023.

Kijana amekamatwa na kwa sasa yuko chini ya ulinzi
Kijana amekamatwa na kwa sasa yuko chini ya ulinzi

Kijana aliendesha gari hiyo kwa mwendo wa kasi na hatimaye, akasimama kwenye Uwanja wa “San Damaso” na kushuka ndani ya gari, akawekwa chini ya ulinzi. Kijana huyu akapelekwa kuchunguzwa afya yake kwenye Idara ya Afya na Usafi ya mji wa Vatican na kugundulika kwamba, kijana huyu alikuwa anakabiliwa na changamoto za afya ya akili. Kwa sasa amewekwa mahabusu, kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Taharuki Mjini Vatican
19 May 2023, 14:27