Tafuta

2023.05.10 Kardinali  Parolini akiwa huko Macerata alibariki sanamu za Padre  Matteo Ricci Xu Guangqi nje ya Kanisa Kuu. 2023.05.10 Kardinali Parolini akiwa huko Macerata alibariki sanamu za Padre Matteo Ricci Xu Guangqi nje ya Kanisa Kuu. 

Parolin:Matteo Ricci&Xu Guangqi ni cheche mbili za mwanga wa amani

Tarehe 9 Mei,Katibu wa Vatican alizindua na kubariki sanamu za Padre Ricci na rafiki yake, mfuasi wa Chinnje ya Kanisa kuu la Macerata,mahali alikozaliwa mmisionari maarufu wa Kijesuit.Hiyo ni zawadi kutoka kwa Jumuiya za Jimbo la Kikatoliki nchini China.Katika mahubiri,alikumbusha kuwa amani ya Mungu ni kujua kusamehe kila mtu,hata adui zako.

Na Angella Rwezaula, - Vatican

Padre Matteo Ricci, mwinjilishaji na  Mjesuit wa China na Dk. Paolo Xu Guanqi, mwongofu nchini China mashuhuri na rafiki mkubwa wa Padre  Ricci, hao walikuwa kama  cheche ya nuru, kitovu cha upendo, chachu ya maisha ya watu wengi kwa sababu waliishi katika umoja na Mungu. Kwa hiyo “ Sasa ni zamu yetu kukumbuka kwamba amani ya kweli ni ile inayokayo kwa Mungu, na ni kuwa kitu kimoja naye na kujua kusamehe kila mtu, hata adui zetu.  Hivi ndivyo,  Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican  alisema na akanukuu maneno ya waraka wa Pacem In Terris wa Mtakatifu Yohane XXIII, uliochapishwa miaka 60 iliyopita katika wakati mbaya wa ukosefu wa amani duniani, na mgumu kama ule ambao tumekuwa tukipitia kwa zaidi ya mwaka mmoja akifikira vita vya Ukraine na Urussi.

Kardinali Parolini akiwa Macerata
Kardinali Parolini akiwa Macerata

Ni katika fursa ya mahubiri yake kwa  kutoa heshima na kwa takwimu za Mjesuit anayeheshimika kutoka Macerata ncjhini Italia  na rafiki yake mkuu wa Kichina, katika mahubiri ya Misa kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Yohane  huko Macerata Italia wakati wa uzinduzi na  kutoa baraka ya sanamu mbili za marafiki hao wawili. Sanamu zilizowekwa kwe mbele ya hekalu jipya lililokarabatiwa na kutolewa na chama cha Wakatoliki wa China ambao ni marafiki wa Padre Ricci na Xu Guanqi.

Kardinali Parolini akitoa hotuba yake
Kardinali Parolini akitoa hotuba yake

Kardinali Parolin  katika mahubiri pia alisisitiza kwamba watu hao wawili, ingawa ni wa tamaduni za mbali na tofauti sana, lakini walikutana katika urafiki na kuzalisha urafiki wa kijamii, bila kujifanya kuwa sawa lakini wakikaribia kuheshimiana na walikabiliana kwa pamoja changamoto ambayo bado ni ya wakati wa sasa. Changamoto, kwa heshima kubwa ya  ukuu wa kiutamaduni nchini China, kushiriki na Wachina zawadi isiyokadirika ya Injili, iliyotolewa kama njia ya hekima na Bwana kwa watu wote wanaotaka wokovu. Kwa hiyo Amani ya Mungu haina mwisho, lakini amani ya ulimwengu inakwisha mapema au baadaye alisisitiza Katibu wa Vatican katika mahubiri.

Wakati wa kuzindua na kubariki sanamu ya Padre RICCI MMISIONARI WA CHINA
Wakati wa kuzindua na kubariki sanamu ya Padre RICCI MMISIONARI WA CHINA

Akizungumzia  kuhusu Injili inayosimulia kuaga kwa Yesu kwa wanafunzi, na zawadi yake kwao ya amani ya Mungu, katibu wa Vatican alikumbuka kwamba hilo ni “ondoleo la dhambi tulilopewa sisi wenye dhambi kwa njia ya Mwana wake na ni kuwa umoja naye na kujua kusamehe kila mtu, hata adui. Sio amani ambayo ulimwengu unaweza kutoa, kwa sababu amani ya ulimwengu mara nyingi ni matokeo ya nguvu,  kama Papa Francisko alivyosema, kuwa amani ya dunia itaisha mapema au baadaye na tunapaswa kutafuta mwingine, na mara nyingi inategemea mateso ya wengine na unyonyaji wao. Amani ambayo Yesu anatoa ni kitu chochote ila ila inakuongoza katika mwendo na kukutoa katika upweke wako, na kukuongoza kwenda kwa  wengine”. Kama vile Padre Ricci na utume wake  huko China.

KARDINALI PAROLIN HUKO MACERATA
10 May 2023, 17:00