Papa Francisko amekutana na Rais wa Jamhuri ya Slovenia
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu 22 Mei 2023 amekutana mjini Vatican na Rais Nataša Pirc Musar wa Jumhuri ya Slovenia kwa karibu ya nusu saa ya mazungumzo na Papa. Mara baada ya mkutano huo pia amezungumza na Kadinali Parolin na Katibu wa Vatican akiongozana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher Katibu wa Vatican w masuala ya kimataifa, na mashirika ya Kimataifa. Kwa hiyo mazungumzo kati ya Papa Francisko na rais wa Jamhuri ya Slovenia, Nataša Pirc Musar, yalichukua nusu saa. Kuanzia 8.50 hadi 9.20, akiwa katika ziara yake nchini Italia na walifanya mazungumzo nyuma ya milango iliyofungwa katika Maktaba ya Jumba la Kitume.
Mazungumzo katika Sekretarieti ya Vatican
Wakati wa mazungumzo ya dhati na Katibu kwa mujibu ujumbe kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, shukrani ilioneshwa kwa uhusiano mzuri wa nchi mbili, na pia kwa mchango wa Kanisa Katoliki kwa jamii. Katika muendelezo wa mazungumzo hayo, wanabainisha kwamba walizingatia masuala mbalimbali ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na vita vya Ukraine na matokeo yake ya kimataifa, pamoja na hali ya kisiasa katika Balkan ya Magharibi na matarajio ya baadaye ya Mkoa huo. mchakato wa ushirikiano wa Ulaya.”
Zawadi
Wakati wa kubadilishana zawadi, Papa alimpatia rais kazi kisanii ya shaba iliyoitwa ‘Upendo wa Kijami, inayoonesha mtoto akimsaidia mwingine kuamka, na maandishi “Kupenda Kusaidia”. Kama zawadi pia Ujumbe wa Amani wa 2023, Hati ya Udugu wa Kibinadamu iliyotiwa saini huko Abu Dhabi na kitabu kuhusu Statio Orbis cha tarehe 27 Machi 2020, kilichohaririwa na LEV. Kwa upande wake, Rais Pirc Musar alimpatia Papa baadhi ya bidhaa za asali za Kislovenia na kielelezo cha mzinga wa wa nyuki maarufu wa Kislovenia, Anton Janša.