Tafuta

Papa Francisko amemteua Askofu Mpya wa jimbo la Katiola nchini Ivory Coast. Papa Francisko amemteua Askofu Mpya wa jimbo la Katiola nchini Ivory Coast. 

Papa amemteua Padre Honoré Beugré Dakpa kuwa Askofu wa Katiola

Papa amemteua Padre Honoré Beugré Dakpa kuwa Askofu mpya wa Jimbo katoliki la Katiola nchini Ivory Coast:Kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afrika Magharibi(UCAO/UUA).

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko,  Jumamosi tarehe 13 Mei 2023 amemteua Askofu mpya wa Jimbo katoliki la Katiola nchini Ivory Coast,  Mheshimiwa Padre Honoré Beugré Dakpa, wa Jimbo Kuu la Gagnoa, ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afrika Magharibi(UCAO/UUA).

Wasifu wake:

Padre Honoré Beugré Dakpa alizaliwa tarehe 30 Julai 1969 huko Grand-Lahou, Jimbo kuu la  Gagnoa. Baada ya majiundo katika seminari ndogo alimalizia mzunguko wa mafunzo ya Falsafa na alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 20 Desemba 1998 kwa ajili ya Jimbo Kuu Katoliki la Gagnoa. Majukumu mengine aliyofunika na mafunzo zaidi amewahi kuwa Paroko wa parokia ya Gbagbam (1998-1999); Paroko wa  parokia ya Mtakatifu Jean Baptiste huko Lakota na mratibu katika kituo cha katekesi cha Gagnoa (1999-2000); Paroko wa parokia ya Mtakatifu Jacques Cocody II Plateaux, Abidjan (2000-2001); Paroko  wa parokia ya chuo kikuu cha Mtakatifu  Albert le Grand de Cocody, msaidizi wa wanafunzi na mkurugenzi wa kiroho wa Seminari ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu  Paulo VI, Abidjan (2001-2004);

Aidha amekuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu Katoliki cha Afrika Magharibi (UCAO/UUA) na Mwadhiri wa  nidhamu katika Seminari ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu  Paulo VI (2004-2007); Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanoni  katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, Roma (2008-2010); Pprofesa wa sheria za kananoni za Sheria katika UCAO/UUA na mjumbe wa Tume ya Masuala ya Kisheria na Mahakama za Baraza la Maaskofu wa Ivory Coast (2010); jaji wa Baraza la Kitaifa la Kikanisa (2011-2016); mkurugenzi wa Taasisi ya Sheria ya Kanoni ya  UCAO/UUA (2013-2019); tangu 2016, Jaji wa kwanza wa Mahakama ya Jimbo ya Mtakatifu Pedro na, tangu 2020, wamekuwa Katibu Mkuu wa UCAO/UUA .

13 May 2023, 16:45