Tafuta

Ni mwezi Mei ni mwezi wa Maria: Sanamu katika Bustani za Vatican. Ni mwezi Mei ni mwezi wa Maria: Sanamu katika Bustani za Vatican. 

Mwezi Mei na Maria,sanaa na imani katika Bustani za Vatican!

Katika fursa ya mwezi wa Maria,Makumbusho Vatican,inapendekeza mfululizo wa matembezi hasa katika Bustani za Vatican.Mchakato wa utamaduni na kiroho katika ugunduzi wa mazingira ya ajabu na kazi za kisanii ambayo Mapapa walifanya ibada kwa Bikira.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Hatua kumi ya kipekee kwa kila tendo la Rosari ndiyo zinajikita katika mchakato wa kiroho, kiutamaduni na asili kwa ajili ya Bikira Maria katika mwezi wa Mei, kwa kila Jumatano na Jumamosi katika jumba la makumbusho ndani ya Bustani za Vatican.

Unaweza kujionea mwenyewe ukijani huu
Unaweza kujionea mwenyewe ukijani huu
Unaweza kuhisi hali ya utulivu katika bustani za Vatican
Unaweza kuhisi hali ya utulivu katika bustani za Vatican

Maria, ua zuri zaidi kwa kazi ya uumbaji
Kwa njia ya sanaa na imani husindikiza mgeni-mhujaji na mtalii kwa kutafakari juu ya kazi ya uumbaji, sifa ya Mungu, Muumba wa Uzuri wote. "Ni desturi ya Kanisa  kuweka wakfu mwezi wa Mei kwa Bikira Maria kwa sababu kama vile katika mwezi huu asili huamsha na kujionesha katika uzuri wake wote, na ndivyo tunaheshimu ua zuri zaidi la uumbaji kwa mana Maria hasiye na doa. Ikiwa tunafikiria pia sala nzuri ya Rozari Takatifu, tunakumbuka kwamba ilizaliwa ili kumpatia Mama Maria taji la waridi ambalo baadaye liinageuka kuwa Salamu Maria."

Uzuri wa Maua ya mawaridi katika Bustani za Vatican
Uzuri wa Maua ya mawaridi katika Bustani za Vatican

Hatua ya ibada kwa Maria
Miongoni mwa miti ya mizeituni ya kidunia, mierezi, misonobari, misonobari, ikifuatana na harufu ya maua na nyimbo za ndege wanaoishi kwenye bustani ya Vatican, katika msimu huu picha nzuri za Maria huonekana kama vile sanamu ya Maria wa Ulinzi iliyotolewa na Genoese kwa Papa Benedikto. XV katika kumbukumbu ya tokeo  kwa mkulima Benedetto Pareto au sanamu ya Bikira wa Fatima, kumbukumbu ya kuonekana kwa watoto watatu wa wachungaji wa Ureno mnamo 1917 na matukio ambayo yalifuatana nao (kama vile muujiza wa jua), lakini pia ya shambulio lililotendewa kwa Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo tarehe 13 Mei 1981. Mama wa Moyo Mtakatifu sana kabisa  na mwenye wenye macho ya kupendekeza iliyotolewa mwaka 2006 na Askofu wa Ventimiglia kwa Papa Benedikto XVI kwa akili ya kumbukumbu ya sanamu ya miujiza ambayo huko Taggia mnamo 1855 aligeuza macho yake na kuwa kama sura ya mtu aliye hai.

Uzuri hata michoro katika bustani za Vatican
Uzuri hata michoro katika bustani za Vatican

Lourdes ndogo mjini Vatican
Baadaye mchakato wa hija unakupeleka katika mnara kwa ajili ya Mama Yetu wa Guadalupe ambao unajikita na historia ya  wakati ambapo Juan Diego aliyefungua vazi lake, akimuonesha Askofu Juan de Zumárraga maua yalichanua nje ya msimu ambapo Madhabau Takatifu ilijengwa baadaye. Jukwaa lililo mbele ya utayarishaji wa Grotto ya Mama yetu wa Lourdes linavutia sana, ambalo leo hii kama ilivyokuwa wakati wa Papa Leo XIII, linakuruhusu kusali mjini Vatican kwa Mama Safi aliyetokea huko Ufaransa mnamo mwaka 1858 kwa Bernadette Soubirous.

Maeneo ya kijani katika bustani za Vatican
Maeneo ya kijani katika bustani za Vatican

Katika Bustani kwa hiyo  Grotto ya Lourdes katika Bustani za Vatican na altare iliyohifadhiwa katika mahali alipotokea hadi 1958, wakati alipozawadiwa Papa Giovanni XXIII Roncalli, aliyekuwa tayari ni Balozi wa Vatican huko Paris. Ratiba basi inaongoza hadi Amerika ya Kusini katika  picha kumi za Maria zinazoheshimiwa na kutekelezwa kwa michoro na wasanii mbalimbali au na Bikira wa Lujan, mlinzi na msimamizi wa Argentina na hasa anayependwa na Papa Francisko. Kwa mujibu wa Sr. Emanuela Edwards ameeleza kuwa “Kazi hii iliundwa na Alejandro Marmo ambaye, kwa mapenzi ya Papa, alitumia taka ili kutukumbusha kwamba mbele ya Mungu hakuna kitu kinachotupwa lakini sisi sote tunapona kwa huruma zake".

Kutazama Bustani kwa juu
Kutazama Bustani kwa juu

Baada ya katekesi ya Papa
Kalenda ya mwezi Mei na Maria inampatia mwanahija na mtalii fursa ya kushiriki katika uzoefu huo, pamoja na kwa Jumamosi, Jumatano, ambayo ni siku ya katekesi ya Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ambapo mara tu baada ya katekesi kuisha inawezekana hadhira kuchukua fursa ya hija hiyo ya ajabu ya kiroho. Matembezi hayo unaweza kujiandikisha:(Tovuti ya Jumba la Makumbusho) ambayo iko wazi kwa kila mtu, ikiwa ni pamoja na familia zilizo na watoto au watu wenye ulemavu wa hisia, magari na kiakili. Au inawezekana  kutuma maombi kwa barua pepe: education.musei@scv.va.

Uzuri wa Bustani Vatican
Uzuri wa Bustani Vatican

Katika mchakato huo kwa mujibu wa mkuu wa Ofisi ya Shughuli za Kielimu za Makumbusho ya Vatican amebainisha kuwa wanagusa kwanza njia nyingi ambazo Mama Maria amezungumza na watoto wake kwa muda. Daima inasonga mbele kuweza kukazia juu ya upendo wa kimama wa Maria kwetu sote na pia kuona jinsi sanaa ilivyofanya uwepo wa Maria katika maisha ya Kanisa. Kwa hiyo Sr alipenda kuwaalika mahujaji, mwishoni mwa hija warudi nyumbani, lakini hata zaidi katika mioyo yao, na maneno ambayo Mama wa Ulinzi alimwambia mkulima Benedetto Pareto kuwa: “Niamini, Njia hazitashindwa. Kwa msaada wangu, kila kitu kitakuwa rahisi."

Ni mwezi wa Maria: hija katika bustani za Vatican
04 May 2023, 12:16