Tafuta

2022.04.21 Nembo ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC) . 2022.04.21 Nembo ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC) . 

Mabaraza ya DID na WCC yalikutana huko Bossey Aprili 26-27

Mazungumzo na ushirikiano mbali mbalina maadhimisho ya ushirikiako kwa miaka 50 ifikapo 2027,vilikuwa ni mojawapo ya mada zilizojadiliwa kwenye mkutano wa siku mbli 26-27 Aprili 2023 kati ya Baraza la Kipapa la Majadiliano ya kidini(DID)na Baraza la Makanisa ulimwenguni(WCC),uliofanyika huko Bossey nchini Ufaransa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Baraza la kipapa la Majadiliano ya kidini(DID),  ilifanya mkutano wa Mwaka kati ya Baraza hilo na Baraza la Makanisa ulimwenguni (WCC) kwa siku mbili 26-27 Aprili 2023. katika  makao makuu ya Taasisi ya Kiekumene huko Bossey. Ulikuwa ni mkutano wa kwanza baada ya Mkutano wa Kumi na Moja wa  Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WCC) huko Karlsruhe (Ujerumani) mnamo 2022, na baada ya jina kubadilika kutoka Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini hadi Baraza la Kipapa la kwa Majadiliano ya Kidini.

Ilikuwa nembo ya Mkutano wa XI Mwaka wa WCC 2022
Ilikuwa nembo ya Mkutano wa XI Mwaka wa WCC 2022

Mazungumzo na ushirikiajo wa dini mbalimbali: Kwa mujibu wa taarifa, ni kwamba wakati wa mkutano huo wafanyakazi walisisitiza umuhimu wa kushiriki katika majadiliano ya kidini kiekumene, zaidi katika nyakati hizi zenye changamoto. Wahudumu kwa hiyo wa Baraza hilo la Kipapa la majadiliano ya kidini (DID) na wale wa (WCC) wanaoshughulikia Majadiliano na Ushirikiano wa Dini nbalimbali walikutana ili kushirikishana habari kuhusu shughuli katika mantiki ya  maajadiliano  ya kidini yaliyofanyika 2022, na matarajio ya ahadi ya pamoja ya siku zijazo.

Maadhimisho ya ushirikiano kwa miaka 50 ifikapo 2027

Mkutano huo ulisisitiza jukumu muhimu la majadiliano ya kidini ili kubadilisha hali ya migogoro na kukuza amani, hasa kuwawezesha vijana na wanawake katika nafasi za ushirikiano wa kidini, kushughulikia ukiukwaji wa haki za binadamu kwa pamoja, na kusisitiza umuhimu wa mshikamano wa kidini na hali ya kiroho ya mazungumzo. Mkutano huo wa pamoja ulijadili hatua za kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano wao mnamo mwaka wa 2027 na kuazimia kuendeleza urithi wa kufanya kazi pamoja kwa ari na kujitolea zaidi.

02 May 2023, 15:48