Kard.Parolin:Habari kuhusu utume amani wa Vatican unasonge mbele
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Kardinali Pietro Parolin kwa mara nyingine tena amejibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu utume wa wa Vatican wa kuendelea kuhamaisha amani nchini Ukraine, ambao Papa Francisko alitangaza wakati wa mahojiano kwenye ndege wakati wa safari ya kurudi kutoka jiji la Budapest nchini Hungaria. Katika swali hilo, Katibu wa Vatican ameabainisha kuwa “Ndio, kuna habari lakini kwa kawaida katika kiwango cha siri. Kwa vyovyote vile, ninaamini kuwa imeelezwa na ninaamini kuwa itaendelea.”
Ujumbe ambao serikali za Moscow na Kyiv, kupitia maafisa, zilidai katika siku za hivi karibuni kwamba hazikujua, na kwamba hawakuwa wamepokea mawasiliano maalum juu ya suala hilo. Tayari wiki moja iliyopita, katika uwasilishaji wa kitabu katika Chuo Kikuu cha Lumsa, Katibu wa Vatican alitoa maoni yake juu ya suala hilo, akisema kwamba “ameshangazwa na mwitikio wa Urussi na Ukraine kwani kwa ufahamu wangu, wao walikuwa wanafahamu pande zote mbili”. Inawezekana kwani “Unajua jinsi ilivyo, katikati ya msururu wa urasimu inaweza kuwa mawasiliano hayafiki mahali yanapotakiwa kufika,” aliongeza kusema. Kwa njia hiyo tarehe 10 Mei 2023 , akiwa kando ya uzinduzi wa maonyesho ya picha zilizowekwa za Padre Lorenzo Milani, wa Barbiana za karne baada ya kuzaliwa kwake, Kardinali Parolin akihojiwa tena na waandishi alieleza kuwa hata hivyo halikuwa suala la kukanusha na kwamba kulikuwa na habari juu ya utume huo kwa siku zilifuatazo, lakini kwa kiwango cha siri.
Mara nyingi katika kanisa inatokea kutoeleweka
Kwa upande mwingine, alipoulizwa kuhusu sura ya Padre Milani, aliyekosolewa na kupingwa maishani na hata baada ya kifo chake na wawakilishi mbalimbali wa Kanisa, Kardinali Parolin alisema: “Imetokea hiyo mara nyingi katika Kanisa kwamba watu hawakueleweka mwanzoni, na wala hawakuthaminiwa, lakini basi kwa nuru ya kile walichokifanya walipata tena nafasi ya kuwa mfano katika uhusiano na Kanisa lenyewe.” Padre Milani, kwa hivyo siyo hisotria ya kipekee.” Alisisitiza Katibu wa Vatican. Bila shaka, siku zote ni matukio yenye uchungu kutokana na ugumu wa kuelewa mambo mapya ambayo Roho huleta katika Kanisa. Lakini hii ni sehemu ya mwelekeo wa kibinadamu wa Kanisa, kwa hivyo hatupaswi kuogopa kukashifiwa pia.” “Uzuri hata hivyo ni kwamba tunajua jinsi ya kupona na kutambua ishara za Roho na kazi yake katika watu hawa ambao walitambua ishara za nyakati.”
Kuhusu jaribio la kumuua Papa Yohane Paulo II
Kwa maneno ya Katibu wa Vatican, hakukuwa na kumbukumbu ya shambulio la Papa Yohane Paulo II katika uwanja wa Mtakatifu Petro na hisia ambayo ilifanya ukweli huo na zaidi ya yote kujua ni nani alikuwa nyuma yake, na nini maana ya ukweli huo”, alitoa maoni yake Kardinali Parolin. Kwa hiyo “Ilikuwa ni wakati wa majaribio makubwa kwa Kanisa kwamba jaribio lilifanywa juu ya maisha ya Papa na kwa hivyo ilikuwa ni wakati wa mkanganyiko mkubwa.”