Tafuta

2023.05.11 Papa na washiriki wa Mkutano wa Caritas Internationalis. 2023.05.11 Papa na washiriki wa Mkutano wa Caritas Internationalis.  (Vatican Media)

Kard.Czerny:kuongozwa na dira ya Neno la Mungu

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu wakati wa hotuba yake kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Caritas Internationalis(CI)unaoendelea mjini Roma amewaomba watembee katika njia ya upatanisho na kuacha migawanyiko nyuma.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Ijumaa asubuhi tarehe 12 Mei 2023 na Kardinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu wakati wa hotuba yake kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Caritas Internationalis (CI) unaoendelea mjini Roma. Takriban wajumbe 400 wanashiriki katika Mkutano mkuu huo wakiwakilisha mashirika 162 ya Caritas yaliyopo duniani kote amesema kuwa “Kubadilika kwa siku zijazo haimaanishi kukataa matokeo ya wakati uliopita. Na mfanye kazi pamoja, mkiongozwa na dira ya neno la Mungu na kutumia vyema uwezo wenu mwingi. Naomba njia zote mnazotembea zazo  ziendeleze upatanisho na kuacha nyuma migawanyiko na mivutano iliyopita. Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu wakati wa hotuba yake kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Caritas Internationalis (CI) unaoendelea mjini Roma.

Washiriki wa IC
Washiriki wa IC

Siku hizi za mkutano wao watakuwa na kazi ya kuwachagua Rais, Katibu Mkuu, Mweka Hazina, Halmashauri Kuu na Baraza la Wawakilishi la Shirikisho, ambao watakaa madarakani hadi 2027. Uchaguzi unafanyika baada ya mwezi Novemba mwaka 2022 Baraza la Huruma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu  inayoongozwa kwa Kardinali  Czerny kuweka  mwongozo wa Caritas Internationalis (CI) kwa utawala wa muda kufuatia tathmini ya kazi yake na tume huru.  Kwa hiyo katika hotuba yake  Kardinali aligusia tena na kueleza kilichopelekea Baba Mtakatifu kuchukua hatua hizo kali za mabadiliko.  Kwa upande wake Kardinali ana uhakika kwamba wao “wote  walishangazwa na kukerwa nayo” na kwa hiyo mara moja ametaja kwamba “tukio hilo halikuwa ni  uchunguzi wa Caritas Internationalis kwa ujumla. Haikuwa swali la kutilia shaka mafanikio ya kustaajabisha na ya lazima ya CI au mwanachama wake yeyote wa Caritas”.

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa CI
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa CI

Kwa urahisi kabisa, alisema “ baadhi ya watu wanaofanya kazi katika Sekretarieti Kuu walilalamika kuhusu matatizo katika sehemu za kazi. Ni wangapi au nini kilisemwa na nani ... haya ni maelezo ambayo lazima nayahifadhi kwa siri”. Kardinali Czerny alifafanua kuwa iwapo malalamiko ya awali yangeonekana kuwakilisha tu kutoridhika kwa wafanyakazi wachache, hatua zinazofuata zingekuwa tofauti sana. Uchunguzi badala yake uliangazia mifano ya mahusiano na michakato ya kazi ambayo inaweka hatarini shughuli, jina na sifa, sio tu ya Caritas Internationalis lakini ya Caritas yote. Kwa hiyo, baada ya kuzingatia matokeo ya tathmini, Papa alifanya mabadiliko ya uongozi.

Vile vile  iliagiza kusahihishwa kwa sheria ili sheria na taratibu mpya ziwe rahisi kwa mashirika husika ya shirikisho kutambua na kutatua matatizo yajayo. Na zaidi Kardinali  Czerny alihakikishia kuwa “ uponyaji umeanza.  Kanuni zimerekebishwa, Sekretarieti imeweza kuandaa Mkutano Mkuu  na CI iko tayari kufanya kazi na kutumika vizuri zaidi katika siku zijazo”. Akihitimisha, Kadinali huyo alisema: “Kuteuliwa kwa Msimamizi wa Muda kulikuwa tendo la upendo na kujali, si la kukashifu, kwa sababu Caritas iko karibu na moyo wa Papa, wa Kanisa, wa Baraza la Kipapa la huduma ya Maendeleo fungamani ya Binadamu na ulikuwa wito wa lazima wa kukarabati na kurekebisha chombo muhimu kwa ajili ya Kanisa zima.”

12 May 2023, 16:44