Tafuta

2023.05.09 Mkutano wa kwa waandishi wa habati kuhusiana na Jubilei 2025: 'malengo yalifikiwa na mipango' iliyowasilishwa na Askofu Mkuu Rino Fisichella na Katibu Monsinyo Graham Bell 2023.05.09 Mkutano wa kwa waandishi wa habati kuhusiana na Jubilei 2025: 'malengo yalifikiwa na mipango' iliyowasilishwa na Askofu Mkuu Rino Fisichella na Katibu Monsinyo Graham Bell   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Jubilei 2025:Malengo yaliyofikiwa na mipango

Askofu Mkuu Fisichella akiwakilisha kwa waandishi wa habari kuhusu Jubilei 2025:Malengo yaliyofikiwa na mipango amekumbusha Mwaka ujao 2024, umewekwa na Papa Francisko,kwa ajili ya kwa Sala.Kanisa linajipanga kuelekea Jubilei kwa nia ya kukuza umuhimu wa sala ya kibinafsi na ya jumuiya.Wimbo wa maadhimisho hayo umewasilishwa.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Jumanne tarehe 9 Mei 2023 umefanyika mkutano, katika Chumba cha Waandishi wa Habari Vatican  kuhusi  kuwasilisha mipango ya awamu ya maandalizi ya Jubilei 2025 na hatua muhimu za Jubilei hiyo ambapo imeongozwa na mada: “Jubilei 2025:malengo yaliyofikiwa na mipango”. Waliowakilisha walikuwa ni Askofu Mkuu Rino Fisichella, Makamu mwakilishi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji, na Katibu  Monsinyo Graham Bell wote wawili katika Kitengo kwa ajili ya Masuala Msingi ya uinjilishaji Ulimwenguni. Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, pamoja na mambo mengine, ilikuwa ni kuonesha matukio makuu ya Jubilei hiyo, michakato iliyokamilishwa na malengo ambayo tayari yamefikiwa katika awamu ya maandalizi pamoja na ushiriki wa Tume nne za maandalizi, zikisaidiwa na kikao kinachowaleta pamoja wajumbe mabaraza ya Maakosu kimataifa, Kamati ya Kiufundi na Tume Ndogo 35.

Waandishi wa habari wakiwa wanasikiliza uwasilisho wa Mipango ya Jubilei 2025
Waandishi wa habari wakiwa wanasikiliza uwasilisho wa Mipango ya Jubilei 2025

Katika kikao hicho,  na waandisho wa habari tovuti mpya ya Jubilei 2025, (iubilaeum2025.va), pia imewasilishwa, itakayotumika kuanzia siku inayofuata, na programu ya mahujaji (iubilaeum2025), inayopatikana kwenye Android na IOS.  Vile vile, jukwa la kijamii la Jubilei pia litaanza kutumika katika kipindi cha vuli ijayo. Kupitia tovuti na programu, unaweza kufikia jukwaa ambalo litakuruhusu kujiandikisha na kupata “Kadi ya Hija”. Na wakati huo huo Kituo cha Hija pia kitazinduliwa  siku ya Alhamisi tarehe 1 Juni 2023  katika barabara ya  Conciliazione n. 7 Roma  kwa ajili ya  Maelezo ya Jubilei, ambapo waamini na watalii wataweza, kuomba omba taarifa za kushiriki, kuwa mtu wa kujitolea au kuandaa Hija mwenyewe ya 2025. Habari za kwanza kuhusu hilo pia zilitangazwa katika hafla za kiutamaduni zilizopangwa tayari kwa maandalizi ya Mwaka wa Jubilei.

Jubilei 2025: mipango ya kutekeleza hadi kufikia kilele
Jubilei 2025: mipango ya kutekeleza hadi kufikia kilele

Askofu Mkuu Fisichella akiwakilisha kwa waandishi  wa habari ameendelea kusema kuwa Mwaka ujao, 2024, tena kwa ombi la Papa Francisko, utawekwa wakfu kwa ajili ya  Sala. Kwa hiyo Kanisa linajipanga kuelekea Jubilei kwa nia ya kukuza umuhimu wa sala ya kibinafsi na ya jumuiya. Tunasoma uwezekano wa  kuwa Shule ya Maombi, yenye kozi zinazofunika ulimwengu mkuu wa Sala. Aidha, ili kuufurahia zaidi mwaka huu, Baraza hilo la kipapa litachapisha mfululizo wa zana ambazo tumetwa: kama mhutasari wa sala “ili kurudisha uhusiano wetu na Bwana kituoni, karibu kutaka kujifunza kila siku kujua jinsi ya kuomba.kwa njia iliyoshikamana, ikiungwa mkono na mapokeo makuu ya Kikristo”.

Uwasilishaji wa malengo yaliyofikiwa na mipango inayoendelea ya maandalizi ya Jubilei 2025
Uwasilishaji wa malengo yaliyofikiwa na mipango inayoendelea ya maandalizi ya Jubilei 2025

Kwa hili “Mahujaji wa matumaini”, kama tujuavyo, ndiyo kauli mbiu ya Jubilei ya Kawaida 2025. Maana yake ilielezwa moja kwa moja na Baba Mtakatifu katika barua ya tarehe 11 Februari ambayo ilirejewa tena na katika mkutano na wanahabari tarehe 28 Juni 2022, ikiwa ni pamoja na nembo rasmi ya Mwaka wa Jubilei iliyo wasilishwa.  Nembo hiyo inawakilisha ubinadamu unaotoka kwenye pembe nne za Dunia kwa kitendo cha kushikamana na Msalaba. Msalaba uko katika umbo la tanga, mojawapo ya ishara za Tumaini la Kikristo ambalo huleta uhakika wa ushindi wa wema dhidi ya uovu. Matanga ambayo yanajiweka juu ya bahari yakisukumwa na misukosuko ya maisha. Msalaba unaishia kwa umbo la nanga, ishara nyingine ya matumaini ambayo huleta uaminifu na usalama maishani

Uwasilishaji wa hatia za maandalizi ya Jubilei 2025
Uwasilishaji wa hatia za maandalizi ya Jubilei 2025

Askofu Mkuu kadhalia alisisisitizia juu ya Shindano la Kimataifa lilitohitimishwa tarehe 25 Machi 2023 ambalo lilikuwa linahusu Wimbo Rasimi wa Jibilei. Walioshiriki ni watu 270 kutoka nchi 38 tofauti ulimwenguni.  Cha ajabu umri wa watunzi walishiriki shindani ni karibu miaka 48 amesema. Na aliyeandika maneno ya muziki ni  Pierangelo Sequeri, Mtaalimungu na Mwalimu wa Muziki anajulikana kwa ngazi ya kimataifa. Baada ya mfufulizo wa kusikiliza Tume ya Kimataifa iliyokutana tarehe 18 Aprili 2023 iliweza kuwa na umakini wa kuchagua mshinidi wa shindano hilo. Kwa maana hiyo Mshindi wa Wimbo wa Jubilei  2025 ni mwalimu Francesco Meneghello, wa Mantova , Italia ambaye Askofu Mkuu Fisichella amemshukuru.

Jubilei 2025
Jubilei 2025

Katika fursa ya Mkutano huo kwa hiyo Kwaya ya Kikanisa cha Kipapa cha Sistina kimerekodi toleo la kwanza la Wimbo huo ambao umesikilizwa kipande kidogo. Katika mwaka mtakatifu, tarehe ya ufunguzu itategemea na tamko la Jubilei ambapo litatangazwa kwa mujibu wa kiutamaduni , katika sherehe ya Siku Kuu ya Kupaa kwa Bwana mnamo tarehe 9 Mei 2024. Jubilei ya kawaida itaanza kwa kufunguliwa na Mlango Mtakatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mnamo Desemba 2024. Kama Papa asemavyo:  “Ni lazima tuweke taa ya matumaini ambayo tumepewa ikiwaka, na kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba kila mtu anapata tena nguvu na uhakika wa kutazama siku zijazo kwa akili iliyo wazi, moyo wa kuaminiana na akili inayoona mbali”.  Kwa hiyo Askofu Mkuu Fischela amesema “Maneno haya yametusaidia katika miezi ya hivi karibuni, katika maandalizi ya mipango mingi”. Kwa hiyo wataendelea kusindikiza katika miezi ijayo mahali ambapo wanategemea mambo mengine. Kwa sasa ni matarajio ya wote kwamba ni kutangaza matumaini ambayo yanakuja kutoka katika Jubilei ijayo inayoweza kuwa kweli, ya dhati na inayoonekana kwa njia ya ishara nyingi za mshikamano ambao utasaidia kurejesha mtazamo wa utulivu na wa kuaminiana juu ya mahusiano ya kibinafsi, na kutoa mchango kwa ulimwengu wa kibinadamu zaidi na uhamasisho kutoka kizazi hadi kizazi wa mapokeo hai ya imani.

Mipango ya Jubilei 2025
09 May 2023, 17:01