Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Lénard Ndjadi Ndjate, M.C.C.I., kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Kisangani, nchini DRC. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Lénard Ndjadi Ndjate, M.C.C.I., kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Kisangani, nchini DRC.  (Vatican Media)

Askofu Msaidizi Lénard Ndjadi Ndjate, Jimbo Katoliki Kisangani

Askofu mteule Lénard Ndjadi Ndjate, alizaliwa tarehe 2 Januari 1976 huko mjini Yanonge, Jimbo kuu la Kisangani, DRC. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa tarehe 10 Oktoba 2005 akaweka nadhiri za daima na hatimaye, tarehe 13 Agosti 2006 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Amewahi kuwa Mshauri wa Shirika Kikanda, Mlezi wa Wanovisi na hatimaye, Padre mkuu wa Kanda, Shirika la Wamisionari wa Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, nchini DRC.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Lénard Ndjadi Ndjate, M.C.C.I., wa Shirika la Wamisionari wa Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Kisangani, nchini DRC. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu mteule Lénard Ndjadi Ndjate, alikuwa ni Padre mkuu wa Kanda, Shirika la Wamisionari wa Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu nchini DRC. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Lénard Ndjadi Ndjate, alizaliwa tarehe 2 Januari 1976 huko mjini Yanonge, Jimbo kuu la Kisangani, DRC. Baada ya masomo na majiundo yake ya kitawa tarehe 10 Oktoba 2005 akaweka nadhiri za daima na hatimaye, tarehe 13 Agosti 2006 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Askofu Msaidizi Lénard Ndjadi Ndjate, M.C.C.I.,
Askofu Msaidizi Lénard Ndjadi Ndjate, M.C.C.I.,

Tangu baada ya kupadrishwa amewahi kuwa Paroko Bangui na Mshauri wa Shirika Kikanda. Baadaye kati ya mwaka 2013 hadi mwaka 2015 alitumwa na Shirika lake kujiendeleza zaidi katika masomo ya tasahufi na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu, au Shahada ya Umahiri kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, kilichoko mjini Roma. Baada ya kurejea kutoka masomoni kati ya mwaka 2015 hadi mwaka 2019 akateuliwa kuwa Mlezi wa Wanovisi wa Shirika la Wamisionari wa Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu Kimataifa, wanaozungumza lugha ya Kifaransa, huko Cotonou, nchini Benin. Kati ya mwaka 2020 hadi kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu tarehe 13 Mei 2023 Askofu mteule Lénard Ndjadi Ndjate, M.C.C.I., wa Shirika la Wamisionari wa Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, alikuwa ni Padre mkuu wa Kanda, Shirika la Wamisionari wa Wacomboni wa Moyo Mtakatifu wa Yesu nchini DRC.

Uteuzi Kisangani

 

13 May 2023, 16:39