Tafuta

Askofu mkuu João Carlos Hatoa Nunes wa Jimbo kuu la Maputo kuanzia tarehe 5 Mei 2023 Askofu mkuu João Carlos Hatoa Nunes wa Jimbo kuu la Maputo kuanzia tarehe 5 Mei 2023  (Vatican Media)

Askofu mkuu João Carlos Hatoa Nunes wa Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji

Askofu mkuu João Carlos Hatoa Nunes alizaliwa tarehe 8 Machi 1968 Jimbo kuu la Beira, Msumbiji. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 17 Julai 1995 akapewa Daraja takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji. Tarehe 25 Mei 2011, Baba Mtakatifu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Maputo na kuwekwa wakfu ili kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu tarehe 10 Julai 2011.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa kwake na Askofu mkuu Francisco Chimoio, O.F.M. Cap. wa Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu João Carlos Hatoa Nunes kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Maputo. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu João Carlos Hatoa Nunes, alikuwa Askofu mkuu Mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu João Carlos Hatoa Nunes alizaliwa tarehe 8 Machi 1968 Jimbo kuu la Beira, Msumbiji. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 17 Julai 1995 akapewa Daraja takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji.

Askofu mkuu Francisco Chimoio ameng'atuka kutoka madarakani
Askofu mkuu Francisco Chimoio ameng'atuka kutoka madarakani

Tarehe 25 Mei 2011, Baba Mtakatifu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Maputo na kuwekwa wakfu ili kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu tarehe 10 Julai 2011. Tarehe 12 Januari hadi tarehe 29 Juni 2012 akateuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto XVI kuwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo kuu la Beira. Ilikuwa ni tarehe 2 Januari 2017 alipoteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Chimoio, nchini Msumbiji. Tarehe 15 Novemba 2022, Baba Mtakatifu Francisko akamteua Askofu mkuu João Carlos Hatoa Nunes kuwa Askofu mkuu Mwandamizi mwenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Maputo, Msumbiji. Na tarehe 5 Mei 2023 Askofu mkuu João Carlos Hatoa Nunes ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Maputo.

Uteuzi Maputo
05 May 2023, 15:56