Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Firmino David, wa Jimbo kuu la Huambo na Gambera wa Seminari kuu ya Kristo Mfalme, Huambo kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Sumbe, nchini Angola. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Firmino David, wa Jimbo kuu la Huambo na Gambera wa Seminari kuu ya Kristo Mfalme, Huambo kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Sumbe, nchini Angola. 

Askofu Firmino David, Jimbo Katoliki la Sumbe, Nchini Angola

Askofu mteule Firmino David alizaliwa tarehe 13 Aprili 1962 Jimbo kuu la Lubango, Angola. Tarehe 21 Aprili 1991 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Huambo, Angola. Tangu wakati huo kama Padre amewahi kutekeleza utume ufuatao: Paroko-usu, kati ya mwaka 1991-1993 na Paroko 1994-1995 Parokia ya Santo Antonio e Sào Nuno, Jimbo kuu la Huambo. Baadaye aliteuliwa kuwa ni Padre mwongozi wa maisha ya kiroho Seminari ndogo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Firmino David, wa Jimbo kuu la Huambo na Gambera wa Seminari kuu ya Kristo Mfalme, Huambo kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Sumbe, nchini Angola. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Firmino David alizaliwa tarehe 13 Aprili 1962 huko mjini Sasalakata, Jimbo kuu la Lubango, Angola. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 21 Aprili 1991 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Huambo, Angola. Tangu wakati huo kama Padre amewahi kutekeleza utume ufuatao: Paroko-usu, kati ya mwaka 1991-1993 na Paroko 1994-1995 Parokia ya Santo Antonio e Sào Nuno, Jimbo kuu la Huambo. Baadaye aliteuliwa kuwa ni Padre mwongozi wa maisha ya kiroho Seminari Ndogo kati ya mwaka 1991 hadi mwaka 1994.

Askofu Firmino David, Jimbo Katoliki la Sumbe, Angola
Askofu Firmino David, Jimbo Katoliki la Sumbe, Angola

Kati ya mwaka 1995 hadi mwaka 2000 alikuwa nchini Italia kwa masomo zaidi ya Sheria za Kanisa na huko akajipatia Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana kilichoko mjini Roma. Aliporejea nchini Angola, akapangiwa kuwa Msimamizi wa Parokia ya Camunda kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2008. Baadaye akateuliwa kwa mshauri wa Jimbo kati ya mwaka 2000 Hadi mwaka 2019. Alikwisha wahi kuwa Jaji wa Mahakama kati ya Mwaka 2003 hadi mwaka 2017. Baadaye akateuliwa kuwa Makamu wa Gambera kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2013. Tangu mwaka 2013 hadi kuteuliwa kwake kuwa Askofu mpya wa Jimbo la Sumbe, tarehe 4 Mei 2023, alikuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Kristo Mfalme, nchini Angola.

Uteuzi Angola
12 May 2023, 13:47