Mkate kwa ajili ya Papa,zawadi ya Wahungaria kwa kumkaribisha
Na Angella Rwezaula, - Vatican.
Tarehe 25 Aprili, ilikuwa ni Sikukuu ya Mtakatifu Marko Mwinjili ambapo , Kanisa la Hungaria kiutamaduni hubariki ngano. Na hasa katika siku hiyo utengenezaji wa mkate ambao utafanywa katika makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Hungaria kabla ya kuwasili kwa Papa uliwasilishwa kwa vyombo vya habari. Kata Sümeghy alileta unga uliotiwa chachu kutoka nyumbani na akatengeneza kwa mkono wa mtaalam. Katika familia yake, wamekuwa wakitengeneza mkate nyumbani kwa miaka mitatu.
Matunda ya kazi inayompa mtu heshima
Mkate huo unaashiria kukaribishwa kwa Baba Mtakatifu, nchini Hungaria kama ishara rahisi lakini yenye maana, ishara ya kukaribishwa kwa watu. "Tungependa uionje," alisema Kata Sümeghy, afisa habari wa Baraza la Maaskofu wa Hungaria, ambaye kwa miaka kumi iliyopita alifanya masomo yake katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Msalaba Mtakatifu, ambapo, kupitia Kardinali almoner Konrad Krajewski, alipata msaada wa Papa. Sasa ni yeye ambaye anamshukuru Papa kwa ishara ya mkate.
Kazi ya pamoja
Monsignor Tamás Tóth, mratibu mkuu wa ziara ya upapa ameeleza kuwa Sümeghy - alimuomba aweze kuandaa mkate kwa ajili ya Papa Francisko, ambao utakabidhiwa kwake tarehe 28 Aprili 2023 mara baada ya kuwasili kwake jijini Budapest, na vijana wawili waliovaa nguo za kiutamaduni. Mkate huo utaandaliwa kwa kwa njia ya jadi ya chachu na ina unga, maji na chumvi tu. Mkate huo ni maalum kwa sababu ni matokeo ya kazi ya pamoja ya kweli, shukrani kwa wafanyakazi wa Baraza la Maaskofu ambao walitoa viungo na vyombo vya kuutumikia.
Mapokeo
Katika Bara la Ulaya ya Kati ni desturi kumkaribisha Mrithi wa Petro kwa zawadi hiyo: pia ilitokea mnamo mwaka wa 2021 huko Bratislava wakati wa ziara ya Papa Francisko huko Slovakia. Msimamizi wa mkate na kazi ni Mtakatifu Cayetano (Mtakatifu Cajetan wa Thiene), ambaye ameheshimiwa kwa muda mrefu huko Argentina pia. Jorge Mario Bergoglio (Papa Francisko) anahusishwa na mtakatifu, kama Kadinali aliadhimisha Misa huko Buenos Aires siku ya sikukuu yake katika Madhabahu yake . Na Papa Francisko mara kadhaa amekuwa akisema kwamba “kupelekea mkate nyumbani, matunda ya kazi, humpatia mtu hadhi.”