Tafuta

Dk.Paolo Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano:“Ni mara ngapi kwa siku tunatumia neno VITA bila kupata maumivu,bila kusikia ndani yetu kilio cha kimya cha wale waliopitia vita? Dk.Paolo Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano:“Ni mara ngapi kwa siku tunatumia neno VITA bila kupata maumivu,bila kusikia ndani yetu kilio cha kimya cha wale waliopitia vita?  (© Todos os Direitos Reservados)

Dk.Ruffini:Ni muhimu kurudisha nguvu ya Mungu aliyesulubiwa na kufufuka!

"Tunaposema vita,hatufikiri vya kutosha kuhusu jinsi unyanyasaji wa kijinsia umekuwa silaha ya uharibifu wa ubinadamu,wenye uwezo wa kubadilisha kila kitu,kuiba nafsi,siku zijazo na uzuri wa dunia.”Haya yamesemwana Dk.Ruffini,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasilianokatika Warsha:“Mgogoro Unaohusiana na Nyanyaso za Kijinsia,kukuza ufahamu."

Na Angella Rwezaula, Vatican.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, (UN) katika kikao chake cha tarehe 27 Desemba 2007, lilitangaza Siku ya Kimataifa ya Kumbukumbu ya Biashara ya Utumwa na Kukomeshwa kwake, ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 25 Machi. Mantiki hiyo inayoonekana kuwa ya mbali na katika vitabu vya kihistoria, kumbe ni ambayo kwa bahati mbaya bado inaongoza katika safu za matukio ya habari leo hii. Kiukweli, ingawa utumwa umekomeshwa rasmi, biashara ya wanadamu haijatokomezwa katu  na kila mwaka, mahali fulani ulimwenguni, watu wanauzwa ili kunyonywa kwa njia fulani na aina zao (viwanda, omba omba, ukahaba, biashara ya madawa ya kulevya, vita na vurugu). Katika mantiki hii Ubalozi wa Uingereza unaowakilisha Vatican kwa pamoja na  Umoja wa Wanawake Katoliki ulimwenguni, wameandaa tarehe 24 Machi 2023, Warsha kuhusu mada ya “Mgogoro Unaohusiana na Unyanyasaji wa Kijinsia, Kukuza uelewa,” Ijumaa tarehe 24 Machi 2023. Kati ya watoa hotuba alikuwa ni  Dk. Paolo Ruffini Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano ambapo katika hotuba hiyo ameanza na salamu zake kwa Mhes. Chris Trott, Balozi wa Uingereza jijini Vatican na wawakilishi wa nchi nyingine kwa Vatican na wageni wote waalikwa wa kike na kiume. Dk. Ruffini ameeleza alivyo na machache ya kuzungumzalakini mengi ya kusikiliza, na kuonesha awali ya yote hisia ya hatia katika kuchukua nafasi hiyo, kwa sababu hana ufahamu wa moja kwa moja wa vurugu zinzozungumziwa, kwa kuwa hakuwahi kufanya uzoefu binafsi.

Wanawake wengi ambao walishikiri misa takatifu na mikutano huko DRC wakati wa ziara ya Papa
Wanawake wengi ambao walishikiri misa takatifu na mikutano huko DRC wakati wa ziara ya Papa

Katika kuendelea Dk. Ruffini amesema kwamba: “Ni mara ngapi kwa siku tunatumia neno “vita” bila kupata maumivu yoyote, bila kusikia ndani yetu kilio cha kimya cha wale ambao wamepitia vita, au bado wanaishi, ya wale ambao wameteseka katika nafsi zao. nyama, katika miili yao wenyewe, katika nafsi zao wenyewe, kama wanawake ambao wamebakwa katika miili yao na katika mapenzi yao? Tunaposema “vita”, tunafikiria nani atashinda na nani atashindwa. Tunafikiria juu ya silaha. Tunawasahau watu, nafsi zao na mioyo yao. Tunaposema “vita”, hatufikiri vya kutosha kuhusu jinsi unyanyasaji wa kijinsia umekuwa silaha ya uharibifu wa ubinadamu, wenye uwezo wa kubadilisha kila kitu, kuiba nafsi, siku zijazo, na uzuri wa dunia. Tunaposema “mipaka,” hatufikirii vya kutosha kuhusu mipaka mingapi iliyopo katika maeneo ya vita. Kando na zile za kijiografia, hatufikirii ni mara ngapi “mipaka” ya miili ya watu, mioyo, na roho zao zinakiukwa kila siku. Hata kama maoni ya umma ya kimataifa yangelijua hili kikamilifu mwishoni mwa karne iliyopita, ubakaji mkubwa na unyanyasaji wa kijinsia katika migogoro ya silaha daima umekuwa na bado ni silaha za vita ambazo zinalenga kuwalenga, kuwadhalilisha na kuwaangamiza wanawake, kuwanyima hadhi yao ili kuharibu nchi ambayo wao ni sehemu yake. Lakini hata hiovyo ni silaha ambayo inafedhehesha, inaharibu na kuangamiza wale wanaoikimbilia, na kuwa wahalifu.

Mikono hii ya wanawake inaeleza mambo mengi ambayo ni vigumu kuuleza
Mikono hii ya wanawake inaeleza mambo mengi ambayo ni vigumu kuuleza

Tangu kupitishwa kwa Azimio kifungu cha 1820 mnamo tarehe 19 Juni 2008 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ubakaji umezingatiwa kuwa uhalifu wa kivita dhidi ya ubinadamu na uhalifu unaojumuisha mauaji ya halaiki. Lakini bado aina hii ya ugaidi inastawi: Umoja wa Mataifa ulithibitisha kesi 3,293 za unyanyasaji wa kingono unaohusiana na migogoro  mnamo mwaka 2021, 800 zaidi ya 2020 katika nchi 18. Asilimia 96 ya waathirika ni wanawake na wasichana. Umoja wa Mataifa pia unakadiria kuwa kwa kila kesi iliyoripotiwa, kesi 10 hadi 20 haziripotiwi. Kwa hivyo, idadi halisi ya waathiriwa wa unyanyasaji wa kijinsia unaohusiana na migogoro ni kati ya 36,000 na 69,000. Unyanyasaji huu ambao hauna utamaduni, hauna dini, na hauna mipaka, lazima ulaaniwe. Ni lazima upigwe vita na  lazima ushindwe! Kulingana na Shirika la Amnesty International, Ufaransa, wanawake na wasichana milioni 44 walihamishwa kwa lazima ndani ya nchi zao mnamo mwaka  2021, na hivyo kuwaweka kwenye ghasia. Kwa mujibu wa Shirika (NGO)lisililo la Kiserikali la Madaktari Wasio na Mipaka linabainisha kuwa, wengi wa wanawake waliopokelewa barani Ulaya wamepitia ukatili wa kijinsia. Kwa hiyo “Kwa na uharibifu huu wa ubinadamu, wakati mwingine tunajiuliza: Je Mungu yuko wapi katika haya yote? Badala yake tunapaswa kujiuliza: Mwanadamu yuko wapi? tuko wapi? Yuko wapi kila mmoja wetu ambaye Mungu anamuuliza, kama alivyomuuliza Adam: Uko wapi? - kama Martin Buber alivyoandika katika ‘The Way of Man’. Njia za binadamu. Tuko wapi?

Wanawake ni wengi na wasichana ambao wameteseka nyanyaso za kijinsia
Wanawake ni wengi na wasichana ambao wameteseka nyanyaso za kijinsia

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasilianao amesema kwamba “Katika kila enzi Mungu anauliza kila mwanadamu kwamba “Uko wapi ulimwenguni? Uko wapi? Kama Adamu, sisi pia tunajificha. Tunafanya hivyo ili kuepuka uwajibikaji, kukwepa majukumu yetu. Na kwa hivyo, tunateleza zaidi na zaidi katika uwongo wa mijadala yetu kuhusu ulimwengu, kuhusu haki na ubatili, kuhusu mema na mabaya, kuhusu vita na amani. Tunajificha kutoka kwa Mungu, na kutoka kwetu wenyewe. Tunafikiri kwamba vurugu wanazofanya wengine si jambo letu. Na kwa hivyo, tunaishia kutoiona tena, hatuwezi kupambanua. Je ni mpaka lini? “Vitendo vya dhuluma na unyonyaji vinavyoelekezwa kwa wanawake, Papa Francisko anarudia kusema kuwa, “sio makosa tu. Ni uhalifu unaoharibu maelewano, ushairi na uzuri ambao Mungu alitaka kuupatia ulimwengu”; ni “woga na udhalilishaji wa wanadamu wote.” Kwa hiyo “Kila dhuluma anayofanyiwa mwanamke ni kufuru kwa Mungu aliyezaliwa na mwanamke. Wokovu wa wanadamu ulitoka katika mwili wa mwanamke na tunaweza kuelewa kiwango chetu cha ubinadamu kwa jinsi tunavyoutendea mwili wa mwanamke”. Mahali popote ambapo pamekuwepo au bado kuna vita, kwa bahati mbaya tunapima ghadhabu hii dhidi ya ubinadamu.

Mkono wa Papa na maneno yake yaliwaliwaza wenye kuteseka
Mkono wa Papa na maneno yake yaliwaliwaza wenye kuteseka

Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mawasilianao ameendelea na hotuba yake kwamba “Ushuhuda wa maumivu wa Mukumbi Kamala huko Kinshasa wakati wa ziara ya ya Kitume ya Papa  Francisko hivi karibuni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo unakuja akilini. Mnamo 2020, akiwa na umri wa miaka 17, alianza kile alichokiita Kalvari yake ya mateso. Alikuwa akweenda na wasichana wengine kuchota maji mtoni. Njiani alikutana na baadhi ya waasi ambao waliwakamata. Kila mmoja wao alichagua msichana wanayemtaka. “Yeye alichaguliwa na kamanda, amesisitiza Dk. Ruffini na kunukuu maneno yake: “Alinibaka kama mnyama. Yalikuwa mateso mabaya sana. Nilibaki kama mke wake. Alinibaka mara kadhaa kwa siku, wakati wowote alipotaka, kwa saa kadhaa. Hii iliendelea kwa miezi 19, mwaka 1 na miezi 7. “Ilikuwa kazi bure kupiga kelele, kwa sababu hakuna mtu aliyeweza kunisikia au kuja kuniokoa”. Nilikuwa na bahati ya kutoroka na rafiki yangu baada ya miezi 19 ya mateso. Kutokana na uzoefu huu nilirudi bikiwa mjamzito. Nilijifungua wasichana mapacha, ambao hawakuja kutamjua baba yao kamwe. Marafiki wengine ambao nilikuwa nimetekwa nyara siku hiyo hawakurudi tena. Sijui kama wamekufa au bado wako hai. Msalaba wa Kristo na uwasamehe walionibaka na kuwaongoza kuacha kuteseka kwa watu bila sababu.”

Papa wakati wakia ziarani alikuwa na viongozi wengine wa kidini
Papa wakati wakia ziarani alikuwa na viongozi wengine wa kidini

Dk. Ruffini kadhalika ametoa ushuhuda wa “maneno ya Emelda M'karhungulu wa Bugobe  ambayo bado yanaendelea kusikika moyoni mwake kuwa: “Waasi walikuwa wamevamia kijiji chetu cha Bugobe; ilikuwa Ijumaa usiku mnamo  2005. Walichukua mateka kutoka kwa kila mtu waliyeweza, wakimfukuza kila mtu ambaye wangeweza kupata, na kuwalazimisha kubeba vitu vilivyoporwa. Wakiwa njiani, waliwaua wanaume wengi kwa risasi au visu. Waliwapeleka wanawake kwenye Hifadhi ya Kahuzi-Biega. Wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 16. Nilishikiliwa kama mtumwa wa ngono na kudhulumiwa kwa miezi mitatu”. Kwa kuongezea alisema: “Tunataka kuacha maisha haya ya giza nyuma yetu na tuweze kujenga maisha mazuri ya baadaye. Tunadai haki na amani. Tunawasamehe wauaji wetu kwa yote waliyofanya na tunamwomba Mungu kwa neema ya kuishi pamoja kwa amani, utu na udugu.” Katika muktadha huo. Dk. Ruffini amebainisha jinsi ambavyo aliguswa na “kuwasikiliza na wakati huo huo akili yake ikawa ni kujitafakari  kwamba  hajuhi kama angekuwa na hadhi sawa nguvu sawa, upendo uleule wa maisha baada ya kushuhudia uovu mwingi kwa macho yangu, baada ya kuteseka sana katika nafsi yangu na mwilini mwangu. Ninachojua ni kwamba kilio chao hakiwezi kusikika”.

Papa alipta kuwasililiza wahanga wa nyanyaso za kijinsia
Papa alipta kuwasililiza wahanga wa nyanyaso za kijinsia

Kwa hiyo Dk. Ruffini alisema kwamba Papa Francisko kwa wakati huo  aliwajibu wahanga waliotoa ushuhuda wao binafsi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa “Tunaendelea kushtushwa kusikia unyanyasaji usio wa kibinadamu ambao mmeuona kwa macho yenu na uzoefu wenu binafsi. Tunaweza kulia tu kwa ukimya, kwa sababu tumebaki bila maneno. Machozi yenu ni machozi yangu; maumivu yenu ni maumivu yangu”, Papa Francisko aliendelea. “Kwa kila familia inayoomboleza au kuhamishwa kwa kuchomwa moto kwa vijiji na uhalifu mwingine wa kivita, kwa walionusurika katika unyanyasaji wa kingono na kwa kila mtoto aliyejeruhiwa na mtu mzima, ninasema: Mimi niko pamoja nanyi; Ninataka kuwaletea  matunzo ya Mungu. Anawatazama kwa upole na huruma.  Ingawa wenye jeuri wanawatendea ninyi kama pauni, Baba yetu wa mbinguni anaona hadhi yenu, na kwa kila mmoja wenu anasema: ‘Wewe ni wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami ninakupenda’ (Isaya 43:4)”. “Kaka na dada, Kanisa lipo na litakuwa upande wenu daima. Mungu anawapenda; hajawasahau. Lakini wanaume na wanawake wanapaswa kukukumbuka pia!”. Alisisitiza Papa hayo. Akiendelea kunukuu maneno ya Papa: Ni katika jina la Mungu kwamba, pamoja na waathirika na wale wote wanaofanya kazi kwa ajili ya amani, haki na udugu, ninalaani unyanyasaji wa kutumia silaha, mauaji makubwa, ubakaji... dhabihu ya kikatili ya waathirika wasio na hatia. Sikilizeni kilio cha damu yao (rej. Mwa 4:10), fungueni masikio yenu msikie sauti ya Mungu, awaiteni mgeuke, na sauti ya dhamiri zenu; ziwekeni silaha zenu, komesha vita.  Inatosha! Acheni kutajirika kwa gharama ya masikini, acheni kutajirika kwa rasilimali na fedha zilizochafuliwa na damu! … hapana kwa vurugu, kila mara na kila mahali, bila ‘ikiwa’ au ‘lakini’”.

Ziara ya Kitume ya Papa nchini DRC na Sudan Kusini
Ziara ya Kitume ya Papa nchini DRC na Sudan Kusini

“Dk. Ruffini amesema kuwa “Maneno ya Baba Mtakatifu yanaturudisha kwenye swali la Mungu lililoelekezwa kwa Adamu. Uko wapi? Umekwenda wapi? Unajificha wapi? Swali hili pia linaulizwa hata kwetu. Sote tunahusika. Je, tunaitikiaje kwenye vurugu zinazotokea mbele ya macho yetu? Tunaishi katika wakati ambapo hatuwezi kusema, ‘Sikuwepo, sikujua’.Tunapaswa kujibu Hapana kuwepo vurugu”kama alivyofanya huko Kinshasa: Na hakuna kukata tamaa ambayo inatufanya kuwa washirika wa sehemu ya uovu; ambayo haifikirii uwezekano wa mabadiliko”. Hapana kwa wazo la kufikiria uovu kama kitu kisichoepukika, wakati mwingine hata kama lazima. Ikiwa swali la Mungu,  la “Uko wapi?” linatuita tubadilike,  kama Martin Buber anavyoandika kuwa ‘mahali ulipo? kunong'onezwa na shetani, hutuongoza kuamini, badala yake, kwamba tuko kwenye njia ya upofu, akijaribu kutupigilia misumari kwenye uovu, ili kutufanya tuamini kwamba haiwezekani kuondoa vurugu kutoka mioyoni, na kwamba hakuna njia ya kurudisha hatua zetu na kurudi kwenye mwelekeo. Hili ni jaribio la kutufunga katika upotovu wa kiburi chetu”. Kwa kuhitimisha, Dk. Ruffini alibainisha kwamba ndiyo sababu ni muhimu wa uwepo wao hapo. “Ni lazima tuchukue jukumu letu wenyewe ili kuanza tena njia ya wema. Ni muhimu kurejesha nguvu za wale wanaoona, wale wanaojua jinsi ya kuona uovu, wanaojua kutofautisha, wanaojua kushutumu, kuchukua na kuibadilisha kwa nguvu ya wema. Hii ni nguvu ile ile isiyo ya kawaida ya Mungu aliyesulubiwa na kufufuka. Amewashukuru kwa uwepo wao siku hiyo ili kutafuta njia.

24 March 2023, 16:39