Tafuta

Asfoko kuu  Richard Gallagher Katibu wa Vatican wa mahusiana na mataifa na Mashirika ya Kimataifa. Asfoko kuu Richard Gallagher Katibu wa Vatican wa mahusiana na mataifa na Mashirika ya Kimataifa. 

Askofu Mkuu Gallagher:ubinafsi na matumizi mabaya yanapotosha demokrasia

Mafundisho kutoka kwa Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa juu ya mada ya demokrasia kulingana na hekima ya Papa katika hali ya sasa ya kimataifa,katika muktadha wa mkutano kuhusu:"Demokrasia kwa manufaa ya wote.Tunataka kujenga ulimwengu gani?iliyoandaliwa na Kitivo cha Sayansi Jamii cha Gregoriana,Roma.

Na Angella Rwezaula, - Vatican.

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, alianza mafundisho yake kwa kuuliza swali kuwa :“Demokrasia ni nini na nini cha kufanya ili kuihifadhi? Ni katika Somo la Mafunsiaho kuhusu Demokrasia kulingana na hekima ya Papa katika hali ya sasa ya kimataifa, kama sehemu ya mkutano uliongozwa na mada: “Demokrasia kwa manufaa ya wote. Unataka kujenga?, ulioandaliwa na Kitivo cha Sayansi ya Jamii cha Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriana, Roma. Askofu Mkuu Gallagher kwa hiyo alisema kwamba  “Kwa bahati mbaya, leo inaonekana kuwa kinachoendesha uhuru wa watu, dhamana ya uhuru na usawa wa raia wote ni siasa hasi, kupitishwa kwa mapendekezo ya wengine, chochote kile, ili kuongeza malengo ya mtu binafsi na makubaliano, lakini kidogo inabainishwa juu ya juhudi za kutafuta umoja. Ubinafsi na matumizi yanaonekana kuwa majibu pekee kwa hitaji la furaha ambalo linaunganisha miundo ya demokrasia ya uwongo. 

Sera za kisiasa 

Matokeo yake ni wazi, kwa mujibu wa Askofu Mkuu  Gallagher kwamba: "Katika sera za kisasa, hata zaidi ya hapo awali, si nguvu ya hoja bora inayoamua sera za siku zijazo, lakini nguvu ya malalamiko, hisia za silika, na  taswira potofu. Alimulika kile anachofafanua kama mabadiliko ya uzuri katika siasa: wanasiasa na vikundi vinashinda uchaguzi kwa sababu ni wazuri", sio kwa sababu wana mawazo, programu na nadharia zilizoelezewa. Katika muktadha huo, siasa inashindwa kwenda zaidi ya mahitaji ya kiuchumi. Askofu Mkuu Gallagher alijikita kuzungumza juu ya sadaka  ya nguvu zote za kisiasa na za mtu binafsi kwenye madhabahu ya ushindani wa kijamii na kiuchumi.

Nyaraja za kijamii

Kwa upande huo alichukua  taswira ya nyuma hadi Papa Leo XII na kupitia kwa Papa Pio XII ambaye alishutumu jinsi ambavyo mgogoro wa utawala wa kiimla ulivyo sababishwa na kutenganisha fundisho na utendaji wa kuishi pamoja katika jamii kutoka kwa marejeo ya Mungu na kwa kukanyaga chini ya miguu tabia takatifu ya mtu, binadamu, kituo cha uwajibikaji cha utaratibu wa kijamii. Kwa Papa huo Askofu Mkuu Gallagher aliendelea kusema kwamba alitangaza, fundisho la kijamii la Kanisa ambalo  sasa limechukua demokrasia kikamilifu. Na Nyaraka za kijamii zilizofuata, na  zitafuata njia hiyo hiyo. Bado  Askofu Mkuu alikumbuka mchango katika mwelekeo huo wa Yohane XXIII, wa Yohane Paulo II hadi kufikia kwa Papa Francisko ambaye, alipokuwa Kardinali mwaka 2011, kwamba aliandika juu ya "kuzorota kwa siasa, juu ya kuondolewa kwa demokrasia na  juu ya mgogoro wa wasomi".

Fumbo la utawala bora

Katika nafasi za upapa wa siku za mbele  wa Argentina, "mtu aliweza kuona mara moja suala mahiri la maadili, ukumbusho wa jukumu la kila mtu, hasa wale wanaoongoza serikali, ili tujitolee kushinda hali ambayo haikubaliki tena na ambayo haikubaliki tena hali  endelevu". Kwa ufupi, Papa Francisko "anapendekeza kwamba demokrasia ijengwe kwa njia kubwa, shirikishi na kijamii. Kwa kumalizia, Askofu mkuu Gallagher alisisitiza kuwa  ikiwa utawala bora ungeshindwa, irannide ingechukua nafasi, na kukosekana kwa sheria yoyote ya maisha ya kijamii: vurugu tu, uharibifu wa majengo na mashamba, moto na vifo vingetawala". Akirejea juu ya Fumbo la Utawala Bora, alikanusha kwa "kuonesha fadhila za kupata msukumo kila mara kutoka katika: amani, ujasiri, busara, uungwana, kiasi huku ukiambatana na fadhila za kitaalimungu. Haya yote yalifupishwa vyema katika hotuba ya Papa Francisko kwa Wanadiplomasia (Januari 2023): "kujenga amani katika ukweli ina maana zaidi ya yote kuheshimu utu

28 March 2023, 16:44