Sudan Kusini inasherehekea kuwasili kwa Papa Francisko
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Hatimaye kile kilichosubiriwa kwa muda mrefu kimetimia, Papa Francisko sasa yuko ziara yake ya Kitume na Kiekumene nchini Sudan Kusini ambayo imeanza Ijumaa tarehe 3 Februari. Amelakiwa kwa nyimbo na kauli mbiu akishangiliwa huko jijiniJuba kwa furaha tele, japokuwa furaha hizo zikiwa na hisia za ndoto ambazo kwa wengi waliamini kuwa hisingewezekana, hasa baada ya kusitishwa kwa ziara hiyo mwezi Julai mwaka 2022, na kumtuma Kardinali Pietro Parolin, kutokana na kuahirishakwa sababu ya ya matibabu ya goti.
Waliomkaribisha Papa anapowasili jijini Juba, akitokea Congo DRC, kwa ndege ya ATI ni Rais Salva Kiir, ambaye alikutana na Papa Francisko mnamo mwaka 2019 katika nyumba ya Mtakatifu Marta, pamoja na makamu wa rais, ambapo katika tukio hilo lilionesha picha zake, Papa anainama kuibusu miguu ya watawala wa nchi iliyoliwa na ghasia tangu kuzaliwa kwake mnamo mwaka 2011 na ambazo bado ziko hai katika kumbukumbu ya Wasudan Kusini.
Kupitia taarifa za moja kwa moja kutoka kwa wawakilishi wetu huko Juba Francesca Sabatinelli na JohnBatist Tumsime waliofika mapema kwa ajili ya ziara hiyo wamebainisha kwamba ngoma na nyimbo zimesikika zikimkaribisha Papa Francisko kwenye uwanja wa ndege ambazo kwa hakika ni kielelezo cha furaha kubwa wanayopata wananchi kwa uwepo wake, jambo ambalo kwa wengi hapo litamaanisha kuthibitishwa katika imani ambayo imeendelea kuwa thabiti. Na hii hata hivyo licha ya vurugu za kidugu ambazo hazijakoma za kuharibu maisha ya watu na kusababisha watu waliokimbia makazi yao, kama vile wale ambao Papa Francis atakutana nao Jumamosi tarehe 4 Februari katika Ukumbi wa Uhuru, inafafanuliwa na wengi kuwa ni uteuzi mzito zaidi ambao Papa atakuwa nao nchini humo hadi siku ya kuondoka kwake, tarehe 5 Februari 2023.
Papa Francisko amepita katika barabara pekee yenye lami katika mji ambayo imetengenezwa kwa sababu ya ujio wake na ambayo pia inaelekeza kwenye Ubalozi wa Vatican ambayo pia ilikamilishwa haraka haraka kwa masaa ya mwisho wa siku za ujio wake na kupambwa. Kufika kwa Papa Sudan Kusini kunaleta tumaini kwa watu wanaotafuta kabisa amani na umoja, wa nchi nzima ambayo, licha ya ardhi yake tajiri sana, imekandamizwa na vita, umaskini, na sasa pia na hali ya tabianchi ambayo inajidhihirisha yenyewe kuwa kama kichaa cha mafuriko yanayoendelea na mabaya kwa sababu ya uchumi ambao tayari ulikuwa kwa bahati mbaya na ambayo haufanyi chochote zaidi ya kuongezeka hali mbaya ya kutisha ya wakimbizi na watu waliokimbia makazi yao ndani.
Mji wa Juba kwa hakika ulijiandaa kukutana na Baba Mtakatifu, na ulijitayarisha kwa kutafakari juu ya thamani ya upatanisho, ambayo kwa hapo imesalia kuwa changamoto kubwa lakini inayobebwa mbele na wale wote wanaomwona Papa kuwa ndiye atakayeweza kuzungumza na viongozi ili kuwachochea katika makubaliano ya amani ya mwaka 2018 kati ya makundi yaliyotia sahini yasiendelee kuwa katika karatasi bure na kuwataka ili washirikiane kwa manufaa ya watu wao.
Hija ya kiekumene inayoanza tarehe hii 3 Februari ya Papa Fransisko, Askofu mkuu wa Canterbury Welby na msimamizi wa Kanisa la Scotland Mchaungaji Greenshields, kwa hiyo inataka kuwa ni ushuhuda wa amani na haki, kwa mshikamano na watu, si lazima tena kulilia wafu na uharibifu bali matumaini mapya. Ratiba ya siku ni Mara baada ya kuwasili na kukutana na rais na makamu wa rais katika ikulu ya rais, Papa atakutana na mamlaka, mashirika ya kiraia na mabalozi katika bustani ya ikulu hiyo, ambapo atahutubia hotuba yake ya kwanza ya hatua hiyo ya Sudan ya kusini, mara baada ya kutakuwa na uhamisho kwenda Ubalozi wa Vatican mahali atakapokuwa kwa siku hizi za ziara yake.