Tafuta

2023.02.02 Mkutano wa vijana na makatekista katika Uwanja wa Mpira wa Mashahidi huko Congo DRC. 2023.02.02 Mkutano wa vijana na makatekista katika Uwanja wa Mpira wa Mashahidi huko Congo DRC.   (Vatican Media)

DRC:Thamani ya binadamu katika furaha ya kukutana

Papa Francisko anaacha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ili kwenda Sudan Kusini.Shukrani zisizoelezeka na furaha ya Kinshasa kwa ajili ya mkutano huu ambao ulisambaratisha mantiki ya uwindaji na umiliki.Ni kwa maoni ya Dk.Menichetti wa Radio Vatican,Vatican News katika ziara ya kitume ya Papa.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Afrika inayoonekana kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni tofauti sana na unapokuwa nje ya bara hilo. Ndivyo anasema Mwandishi wa Habari wa Radio Vatican, Vatican News, Dk. Massimiliano Menichetti ambaye anaambata na waandishi wengine katika ziara ya Kitume ya 40 ya Baba Mtakatifu huko Jamhuri  ya Kidemokraisa ya Congo DRC(31 Janauari -3 Februari) na Sudan Kusini (3 -5 Februari 2023). Kwa mujibu wake amebainisha jinsi ambavyo inatosha siku moja tu kuwa na mtazamo wa kila kona yenye matarajio ya kushangaza sana na kuwa uwezekano wa kutambua kile ambacho kinatoroka na kusahauliwa kutoka pembe nyingine nyingi. Dk. Menichetti akiendelea na maelezo kuhusu hali halisi ambayo anajionea mwenyewe kwa siku hizi amesema: “hapa moyo wa mwanadamu una uwezo wa kufurahiya kukutana. Amani, maelewano, udugu kweli hutoka kwenye uhusiano, ambao unaweza kuguswa na kuonekana mahali hapa".

Hata mabango yameandikwa kuwa "Papa Francisko tunataka amani"
Hata mabango yameandikwa kuwa "Papa Francisko tunataka amani"

Katikanchi ya almasi amebainisha kwamba "wanafanya siku kuu wakati rafiki akifika kuwatembelea, wanaheshimiwa na ziara ya jamaa, babu, ambaye anashiriki historia yao, na hekima ya maisha. Neno furaha halijaondolewa maana, sio ya kijuu juu, lakini inaonekana iliyo kamili, kwa sababu haiunganishwi na ujuu juu, bali mwanadamu. Ni furaha ya mkutano huo uliojaa watu, waliojazana kwenye sehemu kadhaa kwa mfano kandoni mwa barabara, hata barabara za juu, katika uwanja wa ndege wa Ndololo, uwanja wa mpira wa Mashahidi , kwa wakati wa ziara ya Papa Francisko." Kwa hiyo Shauku ilikuwa ni kuona, kusikia, lakini pia kusalimiana, kutoa heshima, kusherehekea na kushiriki. Na furaha hiyo, katika Afrika, inaimbwa, inachezwa, inashirikishwa. Hisia zilizooneshwa machoni mara nyingi zikilowanishwa na machozi, katika tabasamu pana la watoto, watu wazima na wazee, waliojikuta wakitembea pamoja na Mrithi wa Petro, kufuatia ufahamu wa tumaini lililosimikwa juu ya Kristo.

Papa akukutana na vijana na makateksitoa katika uwanja wa Mashahidi Kishasa
Papa akukutana na vijana na makateksitoa katika uwanja wa Mashahidi Kishasa

Katika kuielezea ziara hiyo nchini Congo Dk. Menichetti amebainisha kwamba “Katika nchi hii, ambapo Mzungu labda hatapata starehe za lazima ambazo amezoea, inawezekana kufuatilia mizizi ya kila kitu, kizuri na kibaya. Pengine hutokea kwa sababu mwanadamu hajashughulikiwa na utajiri wa ustawi, au kwa sababu hapa wakati bado haujaoneshwa kabisa na mambo mengi ya kufanya, lakini kwa pumzi ya jua, ya asili. Kinshasa ni jiji lenye machafuko na fujo, ambapo vibanda, kwenye barabara za udongo na lami, hupishana na marundo ya taka taka, majengo yanayoendelea kujengwa, nyumba zinazotunzwa vizuri na mifupa ya zege zilizotengemezwa vizuri kwa ulinzi.”

Zawadi ya Kasula waliyomzawadia vijana
Zawadi ya Kasula waliyomzawadia vijana

Kwa njia hiyo hali halisi ya jiji ni kwamba foleni ya magari utafikiri kana kwamba hakuna sheria, ikiwa magari hayajazuiwa, yanabadilishana huko na kule, yanaruka haraka, yakipita kushoto na kulia. Magari mengi yameharibika, vioo vya kutazama nyuma vimefungwa kwa waya na mikanda ili viasianguke, milango ya mabasi ya usafiri wa umma mara nyingi yako wazi ili kuwaruhusu kupenyeza watu wengi iwezekanavyo, wengine wanasafiri wakiwa wamesimama nje. Polisi na wanajeshi wanapiga doria mitaani, wana vibao virefu ambavyo hupeperusha dhidi ya wale wanaokiuka maagizo. Watu wanne wanaweza pia kupanda pikipiki moja. Watoto wengi wanaocheza nyuma ya karatasi za rangi ambazo hutenganisha nafasi tupu, wanawake wanabeba mifuko ya ukubwa wote juu ya vichwa vyao”.

Maombi ya watu wakiwa katika uwanja wakimkaribisha Papa
Maombi ya watu wakiwa katika uwanja wakimkaribisha Papa

Mtazamo wa wenyeji daima ni sawa sawa wanakatisha mbele yako. Katika nchi hiyo ambapo migongano ya utajiri na umaskini ulio chini ya ardhi, uzuri wa asili na vita huishi na kugongana, kinachotawala ni msukumo usiozuilika wa watu, yote yanatarajiwa mbele. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itakuwa mbingu. Tumaini hilo si kungoja, kelele, bali ni kile kinachosikika na kizazi kizima, na wale ambao, wakimbeba Kristo, wanajenga siku baada ya siku kati ya vifusi, rushwa, kukataliwa, vurugu, dhuluma, unyonyaji, na mgawanyiko kikabila.

Maaskofu wakimsikiliza Papa
Maaskofu wakimsikiliza Papa

Pengine, hata hivyo, hii ndiyo hasa inayowatia hofu wale wanaoipora, kuiponda na kuinyamazisha Afrika, wale wanaojaribu kuiweka kwenye tatizo ili kutatuliwa au mataifa kusaidia.  Dk. Menichetti amesema kuwa kila  mtu hapo anakumbuka ziara mbili za Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, lakini pia zile za hivi karibuni zaidi za Kardinali Parolin Katibu wa Vatican, ambaye alikwenda Julaikumwakilisha Papa Francisko, ambaye alikuwa ame ameahirisha safari hiyo kutokana na maumivu ya goti. Katibu wa Vatican alileta ahadi kwamba Baba Mtakatifu atakuja. Imekuwa mwaka, sasa Papa aliweza kupumulia  kwenye ndege  wakati akielekea Kinshasa.

Mkutano wa Papa Francisko na maaskofu wa DRC kabla ya kuondoka kwenda Sudan Kusini

Papa alitimiza neno lake na watu hawa hawamsahau, wanahisi kuheshimiwa, kupewa hadhi, na kupendwa. Papa Fransisko amethibitisha katika nchi hiyo, ambapo Kanisa linastawi, uhakika wa upeo, ufahamu wa vifungo thabiti katika Kristo.

Vijana wakimshangilia Papa Francisko katika uwanja wa Mashahidi Kinshasa
Vijana wakimshangilia Papa Francisko katika uwanja wa Mashahidi Kinshasa

Bara hilo aliendelea kueleza Dk. Menichetti kuwa linaendelea kukua sana, sio tu kwa suala la pato la taifa, lakini fursa hazitatokana na  koltani, mafuta, mawe ya thamani japokuwa kwa hakika vitakuwa zana, lakini ni kutoka katika  kumbukumbu ya mwanadamu, kutoka katika shauku ya kukutana, kutoka katika nguvu ya ujana. kutokana na shauku ya watu hao, ambayo itawawezesha ubinadamu wote kupata changamoto mpya, kubadilika, kukua, na kuendelea. "Huu ni mtazamo ulioletwa na Papa ambaye alionesha nuru ya Kristo kama nuru ya kufuata, kwa sababu ndani yake mantiki ya kikoloni au ya kinyama inayeyuka, ikiruhusu mwanadamu kuwa yeye mwenyewe kuhusiana na wengine", alihitimisha huku akiendelea na safari kuelekea Sudan Kusini.

Dk Menichetti na maoni yake kuhusu ziara ya Papa DRC
03 February 2023, 10:28