Tafuta

Hija ya Kitume ya Papa Francisko Bahrein:afla,mkutano na viongozi

Baba Mtakatifu Francisko mara baada ya kufika alikarbishwa kwa afla na kukutana na Viongozi wa Kisiasa,Kidiplomasia na Kiraia.Ifuatayo ni hali halisi ya tukio la kuwasili,afla na hatoba kwa njia ya video fupi na picha.

Na Angella Rwezaula -Vatican.

Hatimaye Baba Mtakatifu Francisko yuko katika Hija ya 39 ya Kitume kimataifa iliyoanza siku ya Alhamisi tarehe 3 Novemba na ambayo itahitimishwa Dominika tarehe 6 Novemba 2022 huko nchini Bahrein. Ni hija ya kushiriki katika maadhimisho ya Kongamano la Bahrein la Majadiliano: Mashariki na Magharibi Kwa Ajili ya Kuishi pamoja kwa Binadamu. Tarehe 4 Novemba linafungwa Kongamano hilo lakini Baba Mtakatifu anaendelea  kuwepo katika nchi hiyo.

Hija ya kitume ya Papa Francisko huko Bahrein 3-6 Novemba 2022
Hija ya kitume ya Papa Francisko huko Bahrein 3-6 Novemba 2022

Habari katika picha za ziara ya Baba Mtakatifu Francisko huko Bahrein  na Video fupi inaonesha  mara baada ya kufika alikaribishwa na afla kwenye uwanja wa Ndege wa Awali akiwa na wenyeji wake na kuelekea baadaye Ikulu kwa Mfalme huko Sakhir na kumtembelea kwa faragha Mfalme Hamad bin Isa bin Salman Al Khalifa pamoja na familia yake. Baadaye alikutana na mamlaka ya nchi na viongozi wa kidiplomasia.

Hija ya Kitume ya Papa Francisko hujo Bahrein

Na sehemu ya pili inajumuisha siku nzima ya Papa Francisko ya ziara yake ya kutume huko Bahrein.

Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko huko Bahrein 3-6 Novemba 2022
Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko huko Bahrein 3-6 Novemba 2022
04 November 2022, 10:34