Uchumi wa Francisko:Papa yuko Assisi
Na Angella Rwezaula- Vatican.
Mji wa Mtakatifu Francis wa Assisi, Jumamosi tarehe 24 Septemba umempokea Baba Mtakatifu Francisko ili kushirki na vijana wanauchumi, wajasiriamali na wanamapinduzi waliofika zaidi ya nchi 120 kutoka ulimwenguni kote ili kushiriki Tolepola III la tukio la Uchumi wa Francisko ana kwa ana mara baada ya matoleo mawili kufanyika kwa njia ya mtandao kutokana na janga la uviko.
Economy of Francesco”, ni harakati ya kimataifa iliyoanzishwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa kuweka ari ya mchakato wa mazungumzo jumuishi na wa mabadiliko ulimwenguni kueleka katika uchumi mpya. Kizazi kipya cha vijana kina shauku ya kufanya mabadiliko mapya.
Katika siku ya kwanza ya “Uchumi wa Francisko! huko Assisi tarehe 22 Septemba 2022 ilifunguliwa kwa mfululizo wa mijadala na meza za mduara kutoka pande zote ili kuwasilisha mavuno, yaani kile ambacho kimefanywa kutokana na mipango iliyofanywa duniani kote ili kushughulikia masuala ya kiuchumi na changamoto za kisasa. Wanauchumi vijana na wajasiriamali walishiriki mbegu na matunda yaliyotawanyika katika kanda mbalimbali za sayari.