Mwakilishi wa Papa huko Timor Mashariki:Tamaduni na mafudisho ya heri
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu Msaidizi wa Masuala ya Mkuu wa Sekretarieti ya Vatican , katika Misa Takatifu katika Kanisa Kuu la Mama safi huko Dili, mji mkuu wa nchi ya Tomor Mashariki , pamoja na Kardinali Virgilio do Carmo da Silva, askofu mkuu wa jiji hilo wakati wa mahubiri alianza kusema kuwa “Wapendwa Watimorest wa Mashariki, ili muweze kuendelea kuwa nuru ya ulimwengu, ili muweze kumpeleka Kristo kwa wale wote wanaotafuta kumwona, ni muhimu kuutafakari uso wa Kristo, na kwamba muwe wanaume na wanawake wa sala ya kina, mazungumzo ya kina na ya kudumu na Mungu”. Kabla ya maadhimisho hayo, Askofu Mkuu Peña Parra alikuwa ametembelea mnara uliowekwa wakfu kwa Mtakatifu Yohane Paulo II huko Tasi-Tolu ambapo, tarehe 12 Oktoba 1989, katika ziara yake ya kihistoria, Papa huyo aliadhimisha Misa wakati nchi hiyo ilipokuwa bado iko sehemu ya Indonesia. Wakati wa mchana, Askofu Mkuu alikutana na Waziri Mkuu wa Timor Taur Matan Ruak. Na Ziara ya Mwakilishi wa Papa itakamilika tarehe 23 Septemba 2022, baada ya kukutana na Rais wa Bunge la Kitaifa, Aniceto Guterres Lopes.
Askofu Mkuu Peña Parra akifungua mahubiri alisisisitiza kwamba Askofu Mkuu Virgilio, tangu tarehe 27 Agosti, ni mtoto wa kwanza wa taifa kijana, ambalo mwezi Mei liliadhimisha miaka 20 ya uhuru wake na kwamba ni ishara ya umuhimu na utume wa Kanisa la Timor Mashariki kuendelea kutangaza ujumbe wa wokovu katika nchi hizi za Kusini-mashariki mwa Asia na kutetea imani ya Kikristo na ikibidi hata kumwaga damu. Askofu Mkuu pia ali linukuu mahubiri ya Misa iliyoadhimishwa na Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili huko Tasi-Tolu, mnamo tarehe 12 Oktoba 1989, alipokumbuka kwamba Wakatoliki wa Timor ya Mashariki wana mila na desturi ambayo maisha ya familia, tamaduni na desturi za kijamii zimekita mizizi katika Injili, na mapokeo haya yanajumuisha sehemu muhimu ya utambulisho wao. Tamaduni iliyojaa mafundisho na roho ya Heri, kumtumaini Mungu kwa unyenyekevu, msamaha na huruma na, inapobidi, kuteseka kwa subira katika dhiki.
Katika familia zao alieleza Askofu Mkuu Peña Parra, waishi desturi ya kanisa la nyumbani, ambamo wazazi hupitisha maadili ya Kikristo na furaha ya Injili kwa watoto wao, (Evangelii Gaudium), hivyo wakirudi kwenye asili, wakiiga mfano wa Wakristo wa kwanza, kama Papa Francisko alivyombusha wakati wa safari yake kwenda Malta mnamo Aprili 2022. Papa Wojtyla, yaani Yohane Paulo II katika ziara yake ya 1989, akitoa maoni yake juu ya maandishi ya Injili ya Mtakatifu Mathayo, alimkumbuka Askofu mkuu mbadala, alisisitiza utume ambao, Titimor Mashariki , lazima uwe 'chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu'. Kiukweli, katika muktadha wa kikanda ambao Wakristo ni wachache, nchi yao, pamoja na Ufilipino ina idadi ya watu walio na Wakatoliki wengi. Askofu mkuu Peña Parra kwa maana hiyo alitoa wito wa kuwa ushuhuda wa imani wa Timor Est Mashariki, mbele ya upeo mkubwa wa uinjilishaji unaofunguka mbele ya macho yako na kwa ushahidi wao wa upatanisho na msamaha, matunda yasiyoweza kukanushwa ya kuishi kwao kwa uthabiti mafundisho ya Yesu Kristo. Shukrani kwa imani hii ambayo wanaishi kwa uthabiti amekiri Askofu mkuu wa Venezuela, baada ya kupitia kipindi cha kihistoria cha dhiki kubwa, leo hii nchi yao yenye amani na demokrasia, iliyojitolea kujenga jamii yenye mshikamano na udugu na kukuza uhusiano wa amani na wa kujenga na majirani zake na jumuiya ya kimataifa kwa ujumla.
Katika mtazamo wa Injili iliyopendekezwa na liturujia na mwinjili Luka, Askofu Mkuu Peña Parra alisisitiza kuwa watu wengi, kama Herode, wanajaribu kutaka kumwona Yesu, kwa sababu wanajaribu kutafuta maana ya ndani kabisa ya maisha yao, ambayo kama Herode tunajua vizuri inaweza kupatikana tu katika kutafakari kwa siri ya Kristo, kama Mtakatifu Augstino anavyo tufundisha katika Kukiri kwake. Katika Waraka wa Kitume Gaudete et Exsultate, (Furahi na Shangilia) Papa Francisko anaeleza kwamba ni kutafakari uso Yesu aliyekufa na mfufuka kunakorudisha ubinadamu wetu, hata ule uliogawanyika na taabu za maisha au kutiwa alama ya dhambi. Ndiyo maana aliwauliza Wakatoliki wa Timor ya Mashariki: Je, mna nyakati ambazo mnasimama mbele yake kwa ukimya, kubaki naye bila haraka na kujiruhusu kutazamwa naye? Je, mnaruhusu moto wake uwake moyo mwenu? Ikiwa watamruhusu Yesu kulisha ndani yanu joto la upendo na huruma watakuwa na moto na kwa hiyo jinsi wanavyoweza kuwasha mioyo ya wengine kwa ushuhuda wao na maneno yao.
Kwa kuhitimisha mwakilishi huyo wa Vatican mahubiri yake alikumbusha kwamba ni kwa kuutafakari uso wa Kristo tu, kuanzia kukutana na Yesu katika sala na maisha ya sakramenti tu ndipo wataweza kuonesha njia wale wanaomtafuta, pia ikiwa mara nyingi hawajui mada ya uchunguzi wao. Na ikiwa woga wa kutojitayarisha mbele ya utume huo wa kuwa 'nuru' kwa wengine unawashambulia wasisahau kile ambacho Yesu alirudia kusema kwa wanafunzi wake kwamba ‘Msiogope’; wasisahau historia na ushuhuda wa imani ya makatekista wao, wasambazaji wa imani, kwa sababu wao na Bikira Maria safi na mlinzi wa taifa hilo daima atawasindikize na kuwasaidia kutimiza utume wao walioitwa kuufanya.