Marekani:Kard.Czerny amebariki sanamu kuhusu ukaribu wa wahamiaji&wakimbizi
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Sanamu ya shaba, iliyopewa jina la Be Welcoming yaani Kuwa mkarimu ni kazi ya Timothy Schmalz, mtengenezaji wa Kumbusho sanamu nyingine kubwa ya wahamiaji katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ,mjini Vatican. Mwaliko wa wema kwa wale ambao mara nyingi hulipa ghrama ya kutojali kwa wengine, yalikumbushwa na sanamu ya Mkanada Timothy Schmalz, mchongaji pamoja na mambo mengine ya sanamu kubwa ya "Malaika usiowjua", ya wahamiaji na wakimbizi, iliyobarikiwa miaka mitatu iliyopita na Papa katika uwanja wa Mtakatifu Petro, ambapo iko karibu na nguzo katika uwanja. Mtindo ule ule wa kweli na nyenzo sawa, shaba vinarudi kuwa kazi iliyobarikiwa na Kadinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamukatika nafasi mbele ya Kanisa la Mtakatifu Maria wa Ziwa huko ChicagoMarekani
Malaika aliyejifichwa
"Kuwa Mkarimu", ndilo jina la sanamu, au kuwa wakarimu, kwa mtazamo wa kwanza inaonesha mgeni ameketi kwenye benchi na kifungu kwenye mabega yake. Lakini ukigeukia sanamu, hapa kuna mshangao: mgeni anageuka kuwa kweli malaika aliyejificha na kwa kufungua mabawa yake. Ni matumaini ya mchongo huo unaweza kuwafanya waendelee kuwa makini kila wakati kwa kujua malaika ni nani, kuwatahadharisha kuwa malaika kwa wengine katika kugundua kuwa Mungu "anatutumia malaika kupitia masikini, waliopotea na waliosahaulika", alisema Kardinali Czerny, huku msanii huyo alisema kwamba kazi hiyo imeongozwa na kifungu cha Biblia kinachokumbusha hitaji la kuonesha fadhili na ukarimu kwa wale wanaokutana.
Timothy Schmalz ametumia miaka 25 kuchonga kazi kubwa za shaba ambazo zimewekwa ulimwenguni kote. Mada ya wengi wao inahusu masuala ya sasa ya haki ya kijamii, kama vile ukosefu wa makazi, wahamiaji, biashara ya binadamu. Nguvu ya sanaa, Schmalz alisema katika mahojiano na Vatican News mapema mwaka huu, ni "kujenga ufahamu kwa njia ya hila na nzuri kwa jamii nzima".