Tafuta

Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro 

Kard.Piacenza kwa ‘Monasteri Wi-Fi’.Mungu anaumba na kusamehe tu

Mhudumu Mkuu wa Toba ya Kitume aliongoza misa Takatifu katika hitimisho la Mkutano Mkuu wa IV wa Monasteri Wi-fi,katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,Septemba 24.Ni Mpango ulioanzishwa na mwandishi na mtunzi Costanza Miriano,kuhusu mada ya Kuungama.Gazeti la Osservatore Romano limechapisha mahuburi yake.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Ulifanyika Mkutano Mkuu wa IV wa Monasteri Wi- Fi  Jumamosi tarehe 24 Septemba 2022 uliongozwa na mada ya ‘Kutubu’ mara baada ya ‘utangulizi’ na kuhusu ‘Neno la Mungu na sala’. Katika Mkutano huo walisaidiwa kutafakari juu ya dhambi, nini maana ya kuungama na matokeo yake juu ya roho za watu, jinsi gani ya kuungamana na sio kama kufanya mazoezi ya kiroho tu au kama kufanya mtiani wa dhamiri, jinsi gani ya kutumia mchakato wa safari ya uongofu, ni nini maana ya ungammo kuu, jinsi gani neema ya Mungu inavyofanya kazi hasa kwa mwenye kutubu anapokabidhi dhambi. Gazeti la Osservatore Romano limechapisha mahubiri ya Kardinali Mauro Piacenza Mhudumu Mkuu wa Toba ya Kitume.

Katika  mahubiri yake kwenye  hitimisho la Mkutano Mkuu wa  IV wa Monasteri Wi-fi, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, alisema   “Ni Mungu tu anaye umba na kusamehe. Katika sakramenti ya upatanisho Mungu anatukabidhi sisi kwa huruma kwa ajili ya kutupatia maisha mapya, kwa kutukabidhi namna hiyo, si msamaha tu lakini pia yeye mwenyewe. Kila sakramenti ya Toba, Yesu Kristo anajitoa mwenyewe na anatuomba kuwa wapya kwa kupokelewa katika mioyo yetu na katika maisha yetu. Na uongofu ni hali ambayo inaanzia na makaribisho. Kardinali Piacenza alisema Fumbo kubwa lisilo na mwisho  wa upendo wa Mungu ni kwamba anaumba bure, anaokoa bure na kutakatifuza bure.

Kwa sababu hiyo sisi tunaamini na Mtakatifu Yohane, ambaye anasema Mungu mwenyewe ni upendo. Sio hilo tu la kupenda, lakini ni Upendo na ni dhamiri ya dhati tu ya Mungu ambayo inaweza kuonesha kwa mtu nini maana ya upendo. Nje ya uhusiano hai na Mungu utatu, inawezakana kuwapo kwa kuiga kutoka katika upendo, ambako hakuna au kidogo ambacho kinaweza kushinda shauku ya moyo wa binadamu kwa kupenda na kupendwa na ambao unatuachia ukosefu wa ukame wa mwanga na wa matumaini. Mtakatifu Paulo tayari alikuwa amesisitiza jinsi mgogoro wa imani katika ulimwengu wa sasa ungeweza kuwa na ukosefu wa matumaini, ambapo kwetu kama  wakristo na wala sio muhimu wa kwa masuala matatu, bali ni Kristo mwenyewe, kama Maandiko matakatifu yasemavyo. Ni Bwana anayejikabidhi kwetu sisi katika Sakramenti ya upatanisho kama Bwana wa huruma, mwenye uwezo wa kuunda tena mtu kwa kumpatia maisha mapya,na kwa kumwingiza kwa upya katika neema ya ubatizo. Kardinali Piacenza alisema, wasisisahau kuwa Maandiko yote Matakatifu yana maneno mawili tu ambayo ni kama mambo ya mwisho ya Mungu. Haya ni Kuumba na kusemehe.

Ni Mungu tu anayeumba kutoka katika utupu, ni Mungu tu anayeumba tena, anasamehe, kwa kuta maisha mapya kwa kiumbe chake. Kwa kusisitiza zaidi, Kardinali Piacenza alisema kwamba kujikabidhi mwenyewe kwa Mungu , kwa upande wa mwaamini, ni kwa lazima kwa kabidhi jingine, lile la kutubu dhambi zetu kwa muungamishi. Shutuma ya unyenyekevu na fungamani ya dhambi zote zilizotendwa na maungamo ya mwisho ya zile za kufa kwa hakika na pengine za mwili  ni hali ya moyo ili uweze  kupatanishwa, kuponywa kutokana na jeraha la uovu na hivyo kufanywa kwa upya na amani ya Mungu au kuwa na uwezo  wakukubali kutolewa kwa huruma  ana kwa ana, ya utoaji ambao Yesu anajifanya mwenyewe kama  mwenye dhambi aliyepatanishwa, hivyo kumhusisha tena na maisha yake mwenyewe .

Kardinali, Piacenza aliendelea kwa kuuliza “Ni nini kinachotusukuma kujisalimisha kikamilifu katika kuungama? Jinsi gani ya kushinda upinzani wote katika maungamo fungamani  na ya unyenyekevu wa kweli, bila kusita au kujihesabia haki, kwa kukubali dhambi ya mtu?  Na akatoa jibu, akionesha nguvu za kuvutia za kudumu mbili Kwanza ni  tukio la ajabu na utambuzi wa Mungu ambaye anajitoa kwa wanadamu ili kuwaokoa, na pili uzoefu wa furaha, unaoambatana na kile ambacho ni hakika cha  maadili na imani ya  kusamehewa. Hiyo sio asili ya kisaikolojia, lakini ya kitaalimungu kwamba " Hatuwezi kijidanganya kuwa kuungamani kfanya kutoweka hisia za hatia; badala yake, ni lazima kutatua hisia ya dhambi, ambayo kiukweli ni ya kitaalimungu, sio ya kisaikolojia".

Kardinali Piacenza kwa maana hiyo alisisitiza kuwa kuna uwajibu wa ukarabati. Kwa hakika, dhambi inaondolewa kwa huruma ya Mungu, na Kanisa kupitia kwa mhudumu wake, hasa kuhani, lakini wajibu wa kurekebisha uovu uliotendwa unabaki kuwa ni wajibu mzito wa kimaadili wa mwenye kutubu. Katika safari hiyo Kanisa hutusaidia kupitia zawadi ya thamani na isiyo ya kawaida ya msamaha. Kardinali alihitimisha mahubiri yake kwa hisia, akifikiria ukweli kwamba sikuzote tunawekwa kwa Mama mpole zaidi, ambaye hutusindikiza bila kuchoka, kututegemeza na kutufunika kwa vazi lake jeupe.

26 September 2022, 15:03