Tafuta

Malkia  Bagration wa Moukhrani Khétévane , Balozi wa Georgia anayewakilisha nchi yake Vatican. Malkia Bagration wa Moukhrani Khétévane , Balozi wa Georgia anayewakilisha nchi yake Vatican. 

Vatican na Georgia,miaka 30 ya mahusiano katika mwelekeo wa utamaduni

Ili kusherehekea na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi mbili,matukio mengi ya kiutamaduni yamepangwa pia kwa kuzingatia msukumo wa majisterio ya kipapa.Aliyezungumzia hayo ni Khétévane Bagration de Moukhrani,balozi wa Georgia anayewakilisha nchi yake jijini Vatican.

Vatican News.

Dominika ijayo tarehe 26 Juni  Vatican itakuwa na wakati mzuri wa muziki kutoka nchini Georgia ambapo kwa hakika, Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Kikristo linatoa mwaliko kwenye tamasha hilo maalum katika mazingira ya kipekee, pamoja na kwaya ya Kanisa kuu la Upatriaki la Tbilisi likitumbuiza katika Kikanisa cha Sistine Vatican. Balozi wa Georgia anayewakilisha nchi yake Vatican amezungumza na Vatican News na kuelezea jinsi tamasha hilo lilivyozaliwa: “Kwaya hiyo inatumwa na Patriaki Ilia II ambalo  ni jibu lake kwa barua ya Papa ya miaka mitatu iliyopita, ambapo Papa alikuwa amemwalika Roma katika tukio la kipekee sana. Kutokana na janga la uviko, ziara hiyo iliahirishwa mara kadhaa na sasa hali za sasa za kiafya za Baba wa Taifa hazimruhusu kufika Roma binafsi”.

Hata hivyo Balozi huyo amebainisha kwamba Ilia II amesikitika sana na kwa sababu hiyo alitaka kupeleka kwaya yake, yenye watu 35, jijini Roma. Kwa maana hiyo tamasha la Dominika 26 Juni,  sio tu sehemu ya moja kwa moja ya sherehe za kumbukumbu lakini pia hata wakati mzuri wa   onesho la kwaya Jumatatu 27 Juni  ijayo kwenye Ubalozi nchini Italia ambao  ni  Mpango unaokusudia  si kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizi mbili, bali pia kusisitiza umuhimu wa majadiliano kati ya Makanisa na umuhimu wa sanaa. Hadi sasa mpango wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 30 imekuwa tofauti sana: mnamo Mei 25 jijini  Roma kulikuwa na maonesho maalum ya mchoraji wa Georgia ambaye alitengeneza  uchoraji wake kwa kutumia divai, ambayo wageni, katika darasa la Bwana, wangeweza kujaribu  kufanya vivyo hivyo. Katika mahojiano na  balozi wa Georgia anayeakilisha nchi yake Vatican alikumbuka kwamba mwaka mmoja uliopita, rais wa Georgia, Salome Zurabishvili, alikutana na Papa Francisko na kutembelea Vatican kwa ujumla.

Katika ziara hiyo, Vatican,  Georgia na Baraza la Kipapa la Utamaduni  ambao leo hii linaitwa  Baraza la Elimu na Utamaduni chini ya uongozi wa Kardinali Gianfranco Ravasi, walitia saini katika Hati ya maelewano yenye lengo la kuimarisha ushirikiano wa kitaasisi, uliohusisha hasa Taasisi ya Kipapa ya Muziki Mtakatifu na Taasisi ya Juu ya Muziki Mtakatifu wa Tbilisi.  “Kwa mawazo haya, tunaweza pia kuona mapema kubadilishana kwa wanafunzi, ambayo ni kuweza kuwapeleka wanafunzi wetu, ambao tayari wamefikia kiwango cha juu, kwa kozi katika majira ya kiangazi ambapo, kwa mfano, wanaweza kusoma kupiga kinanda cha kanisani,  chombo ambacho kiukweli sisi hutumia kidogo. Lakini watu wa Georgia ni watu wa muziki sana”, alisisitiza. Na kiukweli, karibu kila nyumba nchini Georgia kuna kinanda, kuna mengi ya kuimba na muziki. Ndiyo maana mazungumzo ya kidiplomasia na Vatican yanalenga utamaduni na zaidi ya yote muziki. Kipengele kingine cha kuvutia kinawakilishwa na waraka Laudato si  wa  Papa Francisko, ambapo balozi alisema , Laudato si ilipokelewa vizuri sana nchini  Georgia na Wananchi wameupokea vizuri,  shukrani kwa tafsiri ya

Lugha yao kwa njia ya Balozi wa Tbilisi, na kwamba  Waraka wa  Papa uliangukia katika ardhi yenye rutuba. Baada ya yote, Waorthodox wamejitoa kwa miaka tayari katika Mikutano ya Laudato si' ambayo ilifanyika pia huko Georgia na  moja ya mikutano hiyo iliandaliwa na Ubalozi wa kitume wa Vatican  kwa kurejea kwa Pa Maximus Muungamishi na Baba wa Kanisa, kama onesho la kile ambacho Waraka wa Papa, sanjari na mapokeo ya muda mrefu ya Kikristo. Balozi wa Georgia alieleza matumaini kwamba ushirikiano kati ya Makanisa, Vatican  na Georgia utazaa matunda zaidi,  kwa kuzingatia hali ya sasa ya vita barani Ulaya, ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote.

25 June 2022, 14:51