Tafuta

Kard.Farrell:Mwaka wa Familia ya Amoris Laetitia umetoa msukumo wa kichungaji

Katika kuhitimisha Misa Takatifu kwa ajili ya Mkutano wa X wa Familia duniani,iliyofanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha alimshukuru Baba Mtakatifu kwa kuanzisha Mwaka wa Familia ya Amoris Laetitia.Na Jubilee ya Familia itaadhimishwa jijini Roma kama sehemu ya Jubilei ya 2025,wakati Mkutano wa XI wa Familia Duniani utafanyika mnamo 2028.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Misa Takatifu iliyofanyika Jumamosi jioni tarehe 25 Juni 2022 kwa ajili ya Mkutano wa X wa Familia duniani, ulioanza tarehe 22 Juni, Kardinali Kevi Farrell Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, alitoa shukrani mbele ya Baba Mtakatifu Francisko, kwa niaba ya familia zote zilizokuwapo katika uwanja huo na wengine waliokuwa wanafuatilia sehemu mbalimbali za dunia. Awali ya yote alimshukuru kutoka moyoni mwake kwa kufanikisha Mkutano huo wa X wa Familia, na ambao umehitimisha Mwaka wa Familia wa Amoris Laetitia ambao Papa Francisko iliutangaza mnamo tarehe 19 Machi 2021. Kardinali Farrell alifurahi pia kutangaza kwamba mkutano ujao wa Familia na Baba Mtakatifu Francisko utakuwa ni “Jubilee ya Familia”, ambayo itaadhimishwa jijini Roma kama sehemu ya Jubilei ya 2025, wakati Mkutano wa XI wa Familia Duniani utafanyika mnamo 2028.

Misa ya Mkutano X wa Familia duniani 25 Juni 2022
Misa ya Mkutano X wa Familia duniani 25 Juni 2022

Kardinali Farrell akiendelea kueleza mwaka wa Amoris laetitia alisema, Mwaka huo ulitaka kutoa msukumo mpya kwa ajili ya huduma ya kichungaji ya familia katika majimbo yote ulimwenguni na hivyo  maaskofu, mapadre na walei wamefanya kazi kwa ari na kujitolea kusikiliza mahitaji halisi ya familia na kupitia kwa upya mbinu ya yaliyomo ya uchungaji. Kujitolea kwa upya kunahitajika kwa haraka, ambapo wachungaji na familia waliojengeka vyema wanajua jinsi gani ya kushirikiana ili kuwa na ufanisi zaidi katika kazi ya kusindikiza watoto, vijana, wenzi wa ndoa na familia nzima katika changamoto za kimaadili na kiroho za jamii za leo. Wajibu wa pamoja na ushirika thabiti na mzuri wa kikanisa unahitajika.

Misa ya Mkutano X wa Familia duniani 25 Juni 2022
Misa ya Mkutano X wa Familia duniani 25 Juni 2022

Kwa namna ya pekee, Kardinali alipenda kumshukuru Baba Mtakatifu, kwa msaada, shauku na ukaribu aliotaka kuzionesha familia zenye matendo madhubuti ya Upapa, kama vile Sinodi mbili za familia, ambapo Waraka wa Kitume Amoris Laetitia ulizaliwa humo, mafundisho tajiri ya kichungaji ambayo aliwapatia katika mzunguko wa katekesi juu ya familia, matamko mengi ya kutetea uhai na maneno yake ya busara ya kuwasaidia kugundua tena nafasi ya babu na bibi katika familia, pia kuanzisha Siku maalum ya babu na bibi na  wazee Duniani. Na kama hiyo haitoshi, Kardinali amependa kumshukuru zaidi kwa zawadi halisi ambazo ametoa kwa familia zote katika mwaka huu uliokuwa umewakwa kwa ajili yao kwao kwa Barua ya wenzi wa ndoa, hati ya hivi karibu kuhusu mchakato wa njia ya  Ukatekumeni kwa ajili ya maisha ya ndoa, Video 10 zinazogusa za Amoris Laetitia kuhusu familia na mzunguko wa Katekesi juu ya uzee inayoendelea, ambao anarudia tena katika mada ya wazee. Kwa hakika wamemshukuru sana Baba Mtakatifu kwa kazi hii yote ya kutegemeza familia, ambazo zinazidi kutambua upendo wake kama baba na kuhisi kwamba anaelewa vyema changamoto na matatizo yao.

Misa ya Mkutano X wa Familia duniani 25 Juni 2022
Misa ya Mkutano X wa Familia duniani 25 Juni 2022

Baraza la kipapa la Walei Familia na Maaisha, alisema Kardinali Farrell kuwa liko  inafanya kazi pamoja na Mabaraza ya Maaskofu na Majimbo ili kuwasaidia kuitikia wito wake wa kuinjilisha familia na kuinjilisha pamoja na familia. Bado kuna kazi nyingi ya kufanya, lakini baada ya mkutano huo na  Yeye ni mategemeo kuwa  wamekuwa na imani na shauku iliyofanywa upya mioyoni mwao wote. Familia, pamoja na wito wao maalum wa utakatifu, kwa hakika ni sura nzuri zaidi ya Kanisa na wanaweza kuchangia kwa namna ya pekee kuinjilisha ulimwengu kwa uwezo wao wa kutoa ushuhuda wa upendo, nguvu katika magumu na saburi katika kutumainia kwa Mungu.

Misa ya Mkutano X wa Familia duniani 25 Juni 2022
Misa ya Mkutano X wa Familia duniani 25 Juni 2022

Kardinali Farrell aidha alifurahi kutangaza kwamba mkutano ujao wa Familia na Baba Mtakatifu Francisko utakuwa ni “Jubilei ya Familia”, ambayo itaadhimishwa jijini Roma kama sehemu ya Jubilei ya 2025, wakati Mkutano wa XI wa Familia Duniani utafanyika mnamo 2028.  Lakni kuanzia sasa Kardinali Farrell alisema: “Tuombe kwamba haya pia yawe matukio makubwa ya neema yanayogusa mioyo ya maelfu ya familia.” Amemshukuru tena Baba Mtakatifu, kwa ukaribu na kujitoa kwake kwa familia. Kwa upendo wa kimwana wameahdi kumwombea kila siku na utume wake, alihitimisha.

Hotuba ya Kardinali Farrell akimshukuru Papa Mara baada ya Misa ya Mkutano X wa Familia duniani
26 June 2022, 12:28