Tafuta

Waamini wa Ukraine wakidhiriki Sala ya Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Waamini wa Ukraine wakidhiriki Sala ya Papa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro 

Yale maswali ya Papa kuhusu amani

Katika sala ya Malkia wa Mbingu,Papa ameibua swali la dhamira ya kweli ya kusimamisha kuongezeka kwa nguvu za kijeshi na uchochezi wa maneno ili kufikia mchakato wa mazungumzo.

ANDREA TORNIELLI

“Ninajiuliza  kama kweli tunatafuta amani ...”. Papa FrancisKo amechagua kuwasilisha kwa njia ya maswali mashaka ambayo yanawakumba wengi na ambayo yanakua na ongezeko kutokana na kuongezeka kwa majeshi katika vita nchini Ukraine. Kuongezeka kwa majeshi katika wasiwasi kutokana na mzozo unaozidi kuharibu  na ambao una gharama kubwa sana kwa raia wasio na ulinzi na ambao unaenda sambamba na ongezeko la vitisho vya maneno, upotovu kamili wa adui, na uwezekano wa mashambulio ya nyuklia.

Kuendelezwa kwa vita vya uchokozi vilivyofanywa na jeshi la Urussi dhidi ya Ukraine, mbio za kuweka silaha tena, ukosefu wa mipango madhubuti kwa ngazi ya  kimataifa, inamaanisha kwamba fikra za wale wanaofikiria kuwa mzozo wa silaha ni jambo lisiloepukika, kurudi katika siku za nyuma za “mifumo” ya zamani ya vita ambayo walitarajia kuishinda. “Wakati tunashuhudia kudorora kwa ubinadamu,  alisema Papa  ninajiuliza, pamoja na watu wengi wenye huzuni, ikiwa tunatafuta amani kweli; ikiwa kuna nia ya kuzuia kuongezeka kwa nguvu za  kijeshi na kwa maneno; ikiwa tunafanya kila linalowezekalo kusitisha silaha”

Ni dhahiri kabisa katika uthibitisho huo kuna ugumu wa kujibu swali la Papa  Francisko. “Sote tunataka amani”, ni jibu la viongozi wa dunia. Lakini utashi  kwa maneno, ikiwa yameoneshwa, hayageuki kuwa azimio la ubunifu na nia ya kweli ya kujadiliana. Kuna mazungumzo ya amani na kile  ambacho Papa alikiita “mpango wa vita kinaendelea kutumika”. Katika siku za hivi karibuni, Kardinali Pietro Parolin, akitarajia mkutano mpya wa Helsinki, alisema: “Kutazama kile ambacho kimetokea katika miongo ya hivi karibuni inapaswa kutushawishi juu ya hitaji la kuamini zaidi mashirika ya kimataifa na ujenzi wao, kwa kujaribu kuyafanya kuwa “Nyumba yetu ya pamoja” ambapo kila mtu anahisi kuwakilishwa. Na kwa wakati huo huo inapaswa kutushawishi juu ya haja ya kujenga mfumo mpya wa mahusiano ya kimataifa, tena msingi wa kuzuia na nguvu za kijeshi: ni kipaumbele. Na ni kwa sababu, ikiwa hatutafakari juu ya hili, ikiwa hatufanyi kazi kwa hili, tumepangiwa hatima yetu kukimbia kuelekea shimo la vita kamili”.

Kwa sababu hiy Mfuasi wa Petro amerudia ombi lake huku akiomba kwamba “tusijisalimishe katika mantiki ya vurugu, katika mzunguko potovu wa silaha” na hatimaye kuchukua njia ya mazungumzo na ya amani.

01 May 2022, 15:25