Tafuta

Kikosi kipya cha walinzi wa Kipapa kutoka Uswiss walitoa kiapo cha utume

Vijana 36 wa Kiswiss waliamua kujitoa angalau kwa miaka miwili ya maisha yao kumlinda Papa.Uchaguzi ambao si wa kupitwa pembeni,bali ni wa kutazamwa kama kujikatalia ili kufuata wito binafsi.Ni shughuli muhimu sana kwa mujibu wa Kanali Christoph Graf na ambaye amekumbusha hata vita vibaya vinavyoendelea huko Ulaya mashariki.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kusimamia na kulinda Papa anayetawala na kwa wote waliofuata kisheria hata kwa kuhatarisha maisha yao. Ndiyo vijana waliotia kiapo katika Ukumbi wa Paulo VI  jijini Vatican kwa walinzi wapya 36 wa Kikosi cha Ulinzi cha Kipapa cha Uswiss, wakiwa katika mavazi yao rasimi.  Hii ni sare yao rasimi yenye ngao ambayo huvaliwa wakati wa baraka ya upapa ya Urbi et Orbi wakati wa Noeli  na Pasaka. Kwa maana hiyo walitoa kiapo kwa lugha mbalimbali: Kijerumani, Kifaransa na Kiitaliano chaguo lao la kumtetea Papa kwa angalau miaka miwili, mrithi wa yule ambaye, tarehe 6 Mei 1527, walimlinda Papa Clement VII kutokana vita  vya gunia jijini  Roma.

Kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka Uswiss waliapa kwa ajili ya utume wa Kipapa
Kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka Uswiss waliapa kwa ajili ya utume wa Kipapa

Padre Kolumban Reichlin, msimamizi wa Kikanisa cha Kikoso cha Walinzi wa Kipapa alisema kwamba hili ni chaguo ambalo lakini haliwezi kuwekwa kandoni. Alisema  hayo kabla ya walinzi hao kutamka kanuni ya kiapo hicho mbele ya Monsinyo Edgar Pena Parra, Katibu Maidizi wa Vatican, Kadinali Kurt Koch wa Uswiss, mamlaka ya Uswiss, pamoja na Rais wa Shirikisho la Uswiss Ignazio Cassis na ambaye asubuhi  alikutana  na Baba Mtakatifu vile vile na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Uswiss Askofu  Felix Gmelix Gmür, wa Jimbo katoliki la Basel na Abate Urban Federer wa monasteri ya Einsiedeln.

Kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka Uswiss waliapa kwa ajili ya utume wa Kipapa
Kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka Uswiss waliapa kwa ajili ya utume wa Kipapa

Padre Reichlin alikumbuka kuwa hawa vijana ambao, katika enzi iliyojaa dhoruba na msukumo kwa hiari waliamua kukatiza njia ya haraka ya kazi na mapato mazuri, kwa makusudi na kuacha nyuma uwezekano usio na kikomo na faraja iliyotolewa na nchini ya Uswiss ili  kujiweka miaka miwili katika utimilifu wa maisha yao katika huduma ya Kanisa. Shughuli ya vijana 36 wa Uswiss ambao walianza rasmi huduma ya kuwa Walinzi tangu Juni iliyopita  ndiyo wnajikita katika  changamoto nyingi kama vile: Nidhamu, ujuzi wa lugha mpya, utamaduni mpya na maisha, kuishi pamoja katika nafasi iliyofungwa, kukataa sehemu kubwa ya nyanja za kibinafsi, kujitawala na kujitegemea. Hata hivyo akikiri Padre huyo amesema hiyo ni nguvu ya wito wao, wanapofanya yale kwa akili na moyo wanayotambua kuwa hatima yao ya asili, kuwa ni sawa na muhimu kwao, pia wanaazimia kuacha mambo mengine mengi ya kupendeza na yenye kuleta faida za haraka.

Kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka Uswiss waliapa kwa ajili ya utume wa Kipapa
Kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka Uswiss waliapa kwa ajili ya utume wa Kipapa

Takriban watu mia sita walikuwepo katika tukio la  kuapishwa, wakiwemo wazazi, kaka na dada wa walowasindikiza pamoja na familia za wale ambao tayari wameoa. Ukaribu na msaada wao, hata katika sala, ni muhimu sana, alikumbusha kabla ya kiapo, Kanali Christoph Graf, anayeongoza Jeshi la Kipapa la Uswissi katika majukumu yake ya ufuatiliaji katika lango la Vatican na Ikulu ya Kitume na utaratibu na uwakilishi wakati wa  sherehe za kipapa na mapokezi ya serikali. Akiendelea kusema Kanali amesisitiza kwamba Walinzi hufanya huduma inayohitaji sana, hasa kwa kwa kujitolea ambayo inaweza kukabiliwa sio tu kupitia mawazo ya Uswiss ya uadilifu, kuegemea, uaminifu, uvumilivu, kuthaminiana na mazungumzo, lakini zaidi ya yote kwa kuishi maadili ya Kikristo na kuundwa kutoka nayo. Ni kwa njia hiyo tu ambapo Walinzi wa Uswizi sio tu kuwa mshiriki wa kuishi pamoja, lakini chombo cha huduma ya amani.

Kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka Uswiss waliapa kwa ajili ya utume wa Kipapa
Kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka Uswiss waliapa kwa ajili ya utume wa Kipapa

Amani kiukweli, amekumbusha Kanali Graf imekuwa na inaendelea kutikiswa mara kwa mara kwa njia ya ukatili zaidi. Hakuna vita tena! watu walipiga kelele baada ya vita viwili vya uharibifu vya dunia vya karne iliyopita, amesisitiza kamanda wa Walinzi wa Uswiss, wakati sasa kilio hicho kimesahauliwa, kimepoteza nguvu, sana wakati mzozo uliporudi Ulaya wakati wa vita vya kutisha vya Balkan  na sasa, tena, na ukatili usiobadilika.  Vita, hata hivyo, sio tu uhalifu dhidi ya ubinadamu na uumbaji, lakini pia dhidi ya Mungu, wakati mwanadamu ameumbwa kwa ajili ya wema walioitwa kusali, Kanali Graf amesisitiza, akikumbuka pia maneno ya Papa Francisko katika  Waraka wake wa Laudato si 'Baba Mtakatifu anajishughulisha na kuhifadhi na uponyaji wa uumbaji, ustawi wa jumla na heshima ya mtu, haki na amani. Lengo hili linaweza kufikiwa tu ikiwa kila mtu atarejea kuelekeza maisha yake kwenye tunu msingi. Katikati ya maadili haya msingi hakuwezi kukosekana upendo tu.

Kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka Uswiss waliapa kwa ajili ya utume wa Kipapa
Kikosi cha Walinzi wa Kipapa kutoka Uswiss waliapa kwa ajili ya utume wa Kipapa
08 May 2022, 14:20