Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Isaac Bunde Dugu, kutoka Jimbo Katoliki la Gboko, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Katsina-ala nchini Nigeria. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Isaac Bunde Dugu, kutoka Jimbo Katoliki la Gboko, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Katsina-ala nchini Nigeria.  

Askofu Isaac Bunde Dugu Jimbo Katoliki La Katsina-ala, Nigeria

Askofu mteule Isaac Bunde Dugu wa Jimbo Katoliki la Katsina-ala alizaliwa tarehe 14 Aprili 1971 huko Gboko. Baada ya masomo na malezi yake ya Kipadre, tarehe 21 Oktoba 2000 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre Jimbo Katoliki la Makurdi, Nigeria. Baadaye alijiunga na Jimbo Katoliki la Gboko lililoundwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI mwishoni mwa mwaka 2012.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Sana Padre Isaac Bunde Dugu, kutoka Jimbo Katoliki la Gboko, kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Katsina-ala nchini Nigeria. Hadi kuteuliwa kwake, Askofu mteule Isaac Bunde Dugu, alikuwa ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Shughuli za Kichungaji, Sekretarieti kuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria. Itakumbukwa kwamba Askofu mteule Isaac Bunde Dugu wa Jimbo Katoliki la Katsina-ala alizaliwa tarehe 14 Aprili 1971 huko Gboko. Baada ya masomo na malezi yake ya Kipadre, tarehe 21 Oktoba 2000 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre Jimbo Katoliki la Makurdi, Nigeria. Baadaye alijiunga na Jimbo Katoliki la Gboko lililoundwa na Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI mwishoni mwa mwaka 2012.

Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria
Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria

Baada ya kupewa Daraja Takatifu ya Upadre, tangu wakati huo, ametekeleza dhamana na utume wake kama: Paroko-usu, Katibu mtendaji wa Sekretarieti kuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria tangu mwaka 2004 hadi mwaka 2007. Baadaye kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2011 alitumwa kujiendeleza zaidi nchini Ujerumani na kuhitimu masomo yake na wakati huo huo alikuwa ni Padre mlezi wa Chuo cha Wakunga Ujerumani (Nursing and Midwifery. Baadaye aliporejea Jimboni kwake Gboko aliteuliwa kuwa kati ya Washauri wa Jimbo Katoliki la Gboko kati ya mwaka 2013 hadi mwaka 2019. Wakati huo aliteuliwa kuwa ni Mtalaam wa Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria. Na kuanzia mwaka 2019 hadi wakati wa uteuzi wake, amekuwa ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Shughuli za Kichungaji, Sekretarieti kuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Nigeria.

Uteuzi Nigeria

 

 

 

09 April 2022, 15:27