Tafuta

 Muonekano wa Kanisa Kuu la Munich ya Bavaria- Freising. Muonekano wa Kanisa Kuu la Munich ya Bavaria- Freising.  Tahariri

Ripoti ya Munich na mapambano ya Ratzinger dhidi ya nyanyaso

Baada ya kuchapishwa kwa uchunguzi wa miaka ya uaskofu wa Bavaria wa Papa Mstaafu,uko katika uangalizi.Ni haki kukumbuka mapambano ya Benedikto XVI dhidi ya nyanyaso za kijinsia kwa makasisi na utayari wake wakati wa upapa wake wa kukutana na kuwasikiliza waathirika akiomba msamaha kwao.

ANDREA TORNIELLI

Maneno yaliyotumika wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuwasilisha ripoti juu ya nyanyaso katika Jimbo la Munich, na kama ilivyo katika kurasa sabini na mbili za hati ziliowekwa kueleza uaskofu mfupi wa Bavaria wa Kadinali Joseph Ratzinger, katika wiki ya mwisho zimejaza kurasa za magazeti na kutoa uchochezi wa maoni hata makali sana. Papa Mstaafu, kwa msaada wa wahudutangu uaskofu wa Kardinali Michael von Faulhaber, hadi ule wa sasa wa Kadinali Reinhard Marx. Benedikto XVI alijibu kwa kurasa 82, baada ya kuweza kuchunguza kwa kiasi, hati za kumbukumbu za Jimbo. Kwa ilivyokuwa imekadiriwa, ilikuwa miaka minne na nusu ambayo Ratzinger alitoa huduma katika uongozi wa jimbo la Bavaria ambayo ilihodhi umakini wa maoni.

Baadhi ya madai hayo yalikuwa yamejulikana kwa zaidi ya miaka kumi na tayari yalikuwa yamechapishwa katika vyombo vya habari vikubwa vya kimataifa. Kuna kesi leo hii nne zinazopingwa kwa upande wa Ratzinger na katibu wake binafsi, Monsinyo Georg Gänswein, ambaye alitangaza kwamba, Papa Mstaafu atatoa taarifa ya kina mara baada ya kumaliza kuchunguza ripoti hiyo. Wakati huo huo, hata hivyo, inawezekana kulaani kwa uhalifu huo, ambapo Benedikto XVI, amekuwa akisisitiza daima na inawezekana kabisa kurudia kwa nguvu na kurejea kile ambacho kimefanyika katika Kanisa kwa miaka ya hivi karibuni tangu upapa wake.

Unyanyasaji wa watoto ni uhalifu mbaya. Unyanyasaji unaofanywa kwa watoto na makasisi ni uhalifu mbaya zaidi na hili limerudiwa tena na Mapapa wote wawili wa mwisho bila kuchoka kamwe: wanalia kulipiza kisasi mbele ya Mungu, watoto wadogo wanateswa na unyanyasaji na makasisi au watawa ambao kwao, wazazi wao waliowakabidhi ili waelimishwe katika imani. Haikubaliki kwamba wanajikuta ni waathirika wa wanyanyasaji wa kingono waliofichwa nyuma ya tabia ya kikanisa. Maneno fasaha zaidi, juu ya hili, yanabaki kuwa yale yaliyotamkwa na Yesu: yeyote anayewachukiza wadogo angefanya vyema zaidi kufungwa jiwe la kusagia shingoni mwake na kujitupa baharini.

Haiwezekani kusahaulika kwamba Ratzinger, ambaye tayari alikuwa kama Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa alipambana na jambo hilo katika awamu ya mwisho ya upapa wa Mtakatifu Yohane Paulo II,  ambaye alikuwa mshiriki wa karibu na mara tu alipotangazwa kuwa Papa, aliweka kanuni kali sana dhidi ya wanyanyasaji kwa upande wa  makasisi, sheria maalum za kupambana na unyanyasaji.  Zaidi ya hayo, Benedikto XVI alishuhudia, kwa mfano wake halisi, juu ya uharaka wa mabadiliko hayo ya mawazo ambayo ni muhimu sana kukabiliana na hali ya unyanyasaji: kusikiliza na kuwa karibu na waathirika ambao lazima waombwe msamaha daima. Kwa muda mrefu sana, watoto walionyanyaswa na jamaa zao, badala ya kuchukuliwa kuwa watu waliojeruhiwa ili kukaribishwa na kusindikizwa kwenye njia za uponyaji, wamekuwa wakiwekwa mbali. Kwa bahati mbaya, mara nyingi wamefukuzwa na hata kutajwa kuwa “maadui” wa Kanisa na jina lake zuri.

Alikuwa ni Joseph Ratzinger mwenyewe kuwa Papa wa kwanza kukutana na waathirika wa unyanyasaji mara kadhaa wakati wa safari zake za kitume. Alikuwa ni Benedikto XVI, hata dhidi ya maoni ya watu wengi wanaojiita “Ratzingerians”, ambaye alipendekeza, katikati ya dhoruba ya kashfa huko Ireland na Ujerumani, kuwa na uso wa Kanisa la toba, ambalo linajinyenyekeza katika kuomba msamaha, ambalo anahisi kufadhaika, majuto, maumivu, huruma na ukaribu. Moyo wa ujumbe wa Benedikto upo katika taswira hii ya toba. Kanisa sio kampuni, haliokolewi tu kwa mazoea mazuri au kwa matumizi, pamoja na kuwa ya lazima, ya sheria kali na nzuri. Kanisa badala yake  linahitaji kuomba msamaha, msaada na wokovu kutoka kwa yule aliye wa kipekee na anayeweza kuwapatia, kwa yule Msulibiwa ambaye daima amekuwa upande wa wahanga na kamwe hawi upande wa wauaji.

Kwa uwazi wa hali ya juu, akiwa kwenye ndege iliyompeleka huko Lisbon mnamo Mei, 2010, Benedikto XVI alitambua kwamba:“mateso ya Kanisa yanatoka ndani ya Kanisa, kutokana na dhambi iliyo katika Kanisa. Hili pia limejulikana siku zote, japokuwa  leo hii  tunaliona kwa njia ya kutisha sana: kwamba mateso makubwa zaidi ya Kanisa hayatokani na maadui wa nje, bali yanatokana na dhambi katika Kanisa na kwamba Kanisa linahitaji kujifunza tena,  kuwa na toba, kukubali utakaso, kujifunza msamaha kwa upande mmoja, lakini pia haja ya haki. Msamaha hauchukui nafasi ya haki”. Haya ni maneno yaliyotanguliwa na kufuatiwa na ukweli halisi katika mapambano dhidi ya janga la nyanyazo za makasisi. Haya yote hayawezi kusahaulika au kufutwa.

Marekebisho yaliyomo katika ripoti ya Munich, ambayo ni lazima ikumbukwe, sio uchunguzi wa mahakama na  wala hukumu ya mwisho, yatasaidia kukabiliana na nyanyaso katika Kanisa ikiwa hayatapunguzwa katika utafutaji wa ushushu rahisi na muhtasari wa hukumu. Ni kwa njia ya kuepuka hatari hizi tu, ndipo wanaweza kuchangia katika kutafuta haki katika ukweli na uchunguzi wa pamoja wa dhamiri juu ya makosa ya wakati uliopita.

26 January 2022, 12:44