Ratiba za maadhimisho ya kipapa kwa mwezi Januari na Februari 2022
Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican
Ratiba za kiutamaduni ndizo zinaonekana kwanza katika shughuli ya utume wa Papa katika mwanzo wa mwaka 2022, zilizotolewa taarifa kutoka kwa Mshereheshaji wa Kipapa mjini Vatican. Ratiba ya Papa itakuwa na maadhimisho aliyoanzishwa yeye mwenyewe mnamo 2019 kuhusu Dominika ya tatu ya Kipindi cha kawaida cha Mwaka kwa ajili ya kujikita na Neno la Mungu, tafakari na na ugunduzi kwa barua binafsi ya motu proprio Aperuit Illis. Dominika hiyo kwa Mwaka huu, inaangukia tarehe 23 Januari ambapo Baba Mtakatifu anatarajia kuongoza katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro saa 3.30 asubuhi majira ya Ulaya.
Masifu ya Jioni katika siku kuu ya Mtakatifu Paulo sanjari na wiki ya kuombea umoja wa Wakristo
Tarehe nyingine muhimu baadaye ni Jumanne, Januari 25 katika Siku Kuu ya Uongofu wa Mtakatifu Paulo Mtume wa Watu, ambapo maadhimisho ya Kipapa yatafanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo, Nje ya Ukuta, Roma mahali ambapo Papa ataongoza Masifu ya ya Pili ya Jioni, sambamba na hitimisho la Wiki ya 55 ya Kuombea Umoja wa wakristo, ambayo inaanza tarehe 18 Januari kwa maana hiyo itakuwa ni kipindi cha kwanza cha Kiekumene cha mwaka 2022 na ambacho kwa mwaka huu kinachoongozwa na kauli mbiu kutoka Injili ya Matayo:“ Tuliona nyota ya Mashariki ikichomoza na sisi tumekuja hapa kumwambudu”.
2 Februari ni Siku ya kuwekwa Bwana Hekaluni, sambamba na siku ya Watawa duniani
Ratiba ya Papa Francisko kwa Mwezi Februari itamwona akiadhimisha kama kawaida yak ila mwaka, tarehe 2 Februari ya Siku Kuu ya Kuwekwa kwa Bwana Hekaluni sambamba na Siku ya Watawa duniani ambapo, majira ya saa 11.30 jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Papa atadhimisha misa kwa ushiriki wa watawa wa kike na kiume na mashirika mbali mbali ya kitume.
24-27 Februari ni Mkutano wa Maaskofu Italia na Mameya wa miji karibu na Mediteranea
Hatimaye, mnamo tarehe 27 Februari 2022, Papa Francisko anatarajia kwenda huko Firenze, Italia ili kuhitimisha Mkutano wa Maaskofu wa Italia na Mameya walio karibu na Mediteranea ambao utafunguliwa tarehe 24 Februari 2022. Huo ni mkutano unaongozwa na sura muhimu ya Giorgio La Pira, ambaye alikuwa Meya wa mji huo aliyetambua kuunganisha siasa na dini na kuwa kioo cha Mkristo wa kweli wa jana na leo, kwani alitetea kwa nguvu zote wadhaifu zaidi, wasio kuwa na nyumba na haki kwa wafanyakazi. Alihamasisha mikutano ya amani na ustarabu wa kikristo na kufanya mazungumzo ya kimediteranea kwa ajili ya upatanisho kati ya dini za familia ya moja ya Ibrahimu. Mnamo 1959, mwanasiasa wa kwanza wa Magharibi kushinda “Pazia la Chuma”, alikwenda Urusi, huku akiunda daraja la sala, umoja na amani kati ya Mashariki na Magharibi. Alifariki mnamo tarehe 5 Novemba 1977 huko Firenze. Kaburi lake liko katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Marko na Papa Francisko alimtangaza kuwa Mtumishi wa Mungu mnamo tarehe 5 Julai 2018. Kwa maana hiyo uwepo wa Papa katika mji huo wa Firenze unatazamiwa katika Kanisa Kuu la Msalaba Mtakatifu kuanzia saa 4.30.