Tafuta

Kardinali De Donatis Makamu wa Papa Jimbo la Roma. Kardinali De Donatis Makamu wa Papa Jimbo la Roma. 

'Kusikiliza'ni kaulimbiu ya Ujumbe wa Siku ya 56 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni 2022

Kusikiliza kwa masikio ya moyo ni changamoto iliyozinduliwa na Papa kwa ulimwengu wa mawasiliano,akiomba kujifunza kusikilizaIli na lazima kufanywe kwa moyo.Kiukweli kila mazungumzo,kila uhusiano huanza na kusikiliza na ndiyo maana ili kukua,hata kitaaluma,kama wawasilianaji,inahitaji kujifunza tena jinsi ya kusikiliza.Amesema hayo Kardinali De Donatiskatika Misa ya Mtakatifu Francis wa Sales msimamizi wa mawasiliano

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

“Kusikiliza kwa moyo Ndio kaulimbiu inayoongoza Ujumbe wa Siku ya 56 ya Upashanaji Habari Ulimwenguni 2022,  uliochapishwa tarehe 24 Januari 2022 ambayo ni changamoto iliyozinduliwa na Papa Francisko kwa ulimwengu wa mawasiliano huku akiomba kujifunza kwa upya kusikiliza. Kusikiliza lazima kufanywe kwa moyo. Kiukweli, kila mazungumzo, kila uhusiano huanza na kusikiliza, na ndiyo maana ili kukua, hata kitaaluma, kama wawasilianaji, unahitaji kujifunza tena jinsi ya kusikiliza sana.  Hayo yamesemwa na Makamu wa Papa wa jimbo la Roma, Kardinali  Angelo De Donatis, katika mahubiri ya misa ya kumbukumbu ya Mtakatifu Francis wa  Sales, mlezi na msimamizi wa waandishi wa habari na wanahabari, aliyoadhimisha asubuhi Jumanne tarehe 24 Januari kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Maria huko Montesanto.

Wanamawasiliano washiriki kikamilifu katika safari ya sinodi iliyoanza tayari

Kardinali amesema kuwa ujumbe huo ni wa wakati muafaka kwamba  wote katika wakati huu ambapo Kanisa zima linaalikwa kusikiliza ili kujifunza kuwa Kanisa la Sinodi, na wote wanaalikwa kugundua tena kusikiliza kama umuhimu wa wema katika mawasiliano. Kwa mujibu wa  Makamu wa  Papa wa Jimbo la Roma, ametoa mwaliko  kwa waandishi wa habari na wanamawasiliano ili kushiriki kikamilifu katika safari ya sinodi iliyoanza tayari na kwamba wajisikie kama washiriki wa Kanisa lao la Roma  kwani ni faraja ya kutoa ushirikiano katika jumuiya za parokia ya kila mmoja  kwa kusaidia kusoma hali halisi za sehemu mbalimbali za jiji la Roma, kutembea nao katika awamu hii ya kusikiliza, kusaidia katika kutoa sauti, historia  na uzoefu wa watu ambao wangehatarisha kutowafikia na kuwasikiliza.

Waandishi kuza udadisi na uwazi kuwasukuma kwenda pembezoni

Hisia nyingine iliyojitokeza katika maneno ya Kardinali, akikumbuka maneno ya Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe kwa Siku ya Upashanaji habari Kijamii wa mwaka jana, 2021, amehimiza waishi taaluma yao kama wito katika huduma ya ukweli, bila kuchoka, kuishi  uandishi wa habari kama historia ya ukweli ambayo inahitaji uwezo wa kwenda mahali  ambapo hakuna mtu anayekwenda huko  ili kuwa na hoja na shauku ya kuona. Ameomba kukuza  udadisi, uwazi na shauku ambayo iweze kuwasukuma 'kuchakaa soli za viatu vyao, kwenda kukutana na watu kutafuta historia  au kuthibitisha hali fulani ana kwa ana na hatimaye ametoa  shurani  kwa kujitolea, ujasiri na ukarimu uliooneshwa katika nyakati ngumu zaidi za janga la UVIKO-19 katika, kuhakikisha kunakuwapo na huduma ya habari.

24 January 2022, 17:35