Tafuta

2022.01.25. Kardinali Kurt Koch akitoa shukrani kwa Papa 2022.01.25. Kardinali Kurt Koch akitoa shukrani kwa Papa   (Vatican Media)

Kard.Koch:Kama Mamajusi tuendelee katika njia ya Uekumene

Katika salamu alizompatia Papa Francisko kutoka kwa Rais wa Baraza la Kipapa la Umoja wa Wakristo,mwishoni mwa Masifu ya Pili katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta,Kadinali huyo amesema kwamba taalimungu pekee yenye uwezo wa kupiga magoti mbele ya fumbo itatuleta karibu zaidi kufikia umoja kamili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Janga la sasa linatuathiri sisi sote na linatuunganisha katika muungano wa kina zaidi wa sala, na kuamsha ndani yetu hamu ya nuru inayoweza kuangazia giza. Amesema hayo Kardinali Kurt Koch, rais wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo, mwishoni mwa masifu ya Pili ya jioni ya Maadhimisho ya Siku ya Kuongoka kwa Mtakatifu Paulo, na hitimisho la Juma la 55 la Kuombea Umoja wa Wakristo.

Masifu ya jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta
Masifu ya jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta

Kardinali Koch amependa kumshukuru Papa kwa kuongoza maadhimisho hayo, katika Kanisa la Mtakatifu Paolo Nje ya Ukuta, licha ya hali ngumu iliyosababishwa na dharura ya kiafya. Baadaye  amekumbuka mada ya Juma la Maombi, isemayo “Katika Mashariki tuliona nyota yake ikitokea nasi tukaja hapa kumsujudu”, iliyochaguliwa na Baraza la Makanisa ya Mashariki ya Kati, alipendelea  kuwa na wazo la eneo la Asia ambao leo pia wanapitia  wakati wa giza kuu.

Kwa maana hiyo Kadinali Koch amebainisha kwamba kama vile Mamajusi walivyofunga safari na kuifuata nyota inayotangaza kuzaliwa kwa Bwana, kwa njia hiyo hiyo Wakristo wanaweza kuendelea kwenye njia ya umoja ikiwa hawafuati nyota zao binafsi, bali tukigeuka pamoja kuelekea nuru ya Kristo, na tena kwamba ni taalimungu tu itakayoweza kupiga magoti mbele ya fumbo itakaribia umoja.

Masifu ya jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta
Masifu ya jioni katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Ukuta

Sisi Wakristo tutapata umoja ikiwa tu tutaongoka pamoja na Yesu Kristo, ikiwa tutajiruhusu kuangazwa na kuongozwa ndani ya sala yake mwenyewe kwa ajili ya umoja wa wanafunzi wake, aliongeza Kardinali, na kusisitiza kwamba harakati za kiekumene ni kama monasteri isiyonekana, ambapo Wakristo wa Makanisa tofauti katika nchi nyingi na mabara huomba pamoja kwa ajili ya umoja wa Kanisa.

Hatimaye, Rais wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Umoja wa Wakristo, alimshukuru Papa Francisko tena kwa kutiwa moyo mara kwa mara kutembea njia ya umoja na upatanisho na hasa, kwa kumtangaza Mtakatifu Ireneus wa Lyons, kuwa Mwalimu wa Kanisa kwa jina ‘Dotor unitatis'. Kwa upande wa Kardinali ni ishara ya kuahidi pia kwa uekumene.

25 January 2022, 20:43