Tafuta

2021.10.25 Kijana wa Caritas Internationalis akitoa hduma nchini Lebanon 2021.10.25 Kijana wa Caritas Internationalis akitoa hduma nchini Lebanon 

Ukaribu wa Caritas Mashariki ya Kati&Afrika Kaskazini

Caritas Internationalis inafanya safu za mikutano kwa njia ya mtandao katika fursa ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanza utume wake.Ilianza mwezi Oktoba uliopita kwa kujikita na Bara la Amerika Kusini,baadaye Ulaya,Australia na kanda nyingine.Alhamisi 2 Desemba 2021 ilikuwa na mkutano kwa kundi la MONA,ikiwa na maana ya Caritas ya Nchi za Mashariki na Afrika Kaskazini.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Semina kwa njia ya mtandao iliyokuwa inaongozwa na kauli mbiu, 'kuhamasisha  maendeleo fungamani ya binadamu',  Caritas ya Bara la Austalia katika roho ya Laudato si ', iliwasilisha nafasi ya Caritas katika eneo la Nchi za Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (MONA), pamoja na ushuhuda kutoka Lebanon, Siria, Mauritania na nchi nyingine za eneo hilo. Kwa kutazama nchi zinazounda eneo hilo, mtu anaweza kujiuliza ni kitu gani kinafanana, ambalo lilikuwa ni swali lililoulizwa, mwanzoni mwa semina kwa kutazama eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini na rais wa Caritas Internationalis, Gabriel Hatti.

Akijibu Bwana Hatti alisema kuwa kwa pamoja kuna njia panda ya matatizo mengi, ndiyo, lakini pia ya mazungumzo na kuwa Kanisa ndilo linatutuunganisha zaidi. Zaidi ya hayo, Caritas zote ziwekwa muhuri wa  vinasaba vyao na katika zile za jamii, wito huo wa kudumu wa mazungumzo, kukubaliana kwa pande zote utofauti na kushirikiana na wote kwa manufaa ya wote. Kama ambavyo wanaweza kufikiria, amesema safari hiyo wanayosafiri pamoja sio rahisi. Inafanyika juu ya yote katika hali ya dharura na katika hali mbaya zaidi kama vile vita, ajira, shinikizo la kisiasa na kiuchumi. Ingawa njia hii ni ngumu, safari hii pia ni neema, kwa sababu shida hizi zote ni fursa ya kweli kwa Caritas amesisitiza , kwa kurekebisha kila wakati kusudi ambalo iliundwa na kujaribu kuwa waaminifu  zaidi kwa maadili yake na kwa moyo wa dhamira yake ni nini;  upendo thabiti na usio na malipo, katika huduma ya kila mwanadamu katika shida na kwa nia ya maendeleo fungamani ya  binadamu; katika roho ya sinodi na kuongozwa na nyaraka mbili za “Laudato si 'na Fratelli Tutti”.

Yote hayo na mengine yasikiliza Alhamis tarehe 2 Desemba 2021 katika mkutano huo ambapo uingiliaji kati mwingi wakati wa mkutano ni  pamoja na ule wa Padre Michel Abboud, Rais wa Caritas Lebanon, nchi ambayo katika mwaka mmoja na nusu uliopita imeona idadi ya watu wanaohitaji msaada ikiongezeka kwa kasi kubwa. Lebanon, ikipambana na mzozo mkubwa wa kiuchumi na kijamii, pia imelazimika kukabiliana na  afya inayohusishwa na janga la UVIKO-19. Mgogoro ambao pia umeathiri huduma msingi za umma kama vile umeme na maji, na athari kubwa pia kwa ajili ya elimu. Uhaba wa chakula na bidhaa nyingine unafanya iwe vigumu kwa watu kuwa na lishe bora. Zaidi ya hayo, kupunguzwa kwa muda mrefu kwa umeme kunasababisha sumu ya chakula. Mfumuko mkubwa wa bei umewalazimu familia za ya chini na  kati kutafuta msaada wa chakula, kwani wastani wa gharama ya kila mwezi ya chakula kwa familia ni mara tano ya thamani ya mshahara. Kazi ya Caritas ya Lebanon imeongezeka na inaendelea kukua, siku baada ya siku.

06 December 2021, 15:46