Tafuta

Enzi za kiteknolojia Enzi za kiteknolojia 

Mkutano kuhusu teknolojia,amani maendeleo fungamani katika enzi za Uviko

Tarehe 9 Desemba,Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu imeandaa mkutano ili kuweka bayana masuala ya kimaadili na adili katika mtazamo wa muktadha wa teknolojia mpya katika ulimwengu baada ya janga la uviko-19.Wataalam watatoa uchambuzi wa kisayansi na maadili na kuonesha jinsi teknolojia mpya inaweza kuwekwa katika huduma ya maendeleo fungamani ya binadamu.

Na Sr. Angella Rwezaula - Vatican

Kuhamasisha maendeleo fungamani ya Binadamu na amani katika enzi za kidijitali. Teknolojia katika ulimwengu baada ya Covid ndiyo mkutano uliondaliwa na Baraza la Kipapa Huduma ya Maendeleo ya Binadamu, tume ya Vatican ya COVID-19, Mfuko wa Diplo, Taasisi ya Masuala ya Dunia ya Torino, Chuo Kikuu katoliki cha Kimataifa cha Pax Christi cha Marekani, Alhamisi tarehe 9 Desemba 2021 saa 8.00 kamili mchana majira ya Ulaya. Lengo lake kwa mujibu wa taarifa ni kutoa mchango wa mazungumzo ulimwenguni juu y anafasi za teknolojia za enzi hizi wakati wa janga, kwa mtazamo wa ekolojia fungamani, haki  mkakati jumuishi unaozingatia 'Afya kwa wote' na mfumo wa kiuchumi wa jumuiya jumuishi zaidi.

Wataalam hao watatoa uchambuzi wa jumla wa kisayansi na maadili ambao utaonesha jinsi teknolojia mpya inaweza kuwekwa katika huduma ya maendeleo fungamani ya binadamu, hasa katika nyanja za usalama wa chakula, afya fungamani, pamoja na ufikiaji wa haki na usawa wa chanjo ya Covid-19, yenye hadhi, kazi, amani na usalama na kuhamasisha uchumi wa kijumuiya. Katika mkutano huo watazingatia maono yaliyoainishwa na Papa katika Waraka wa “Laudato si 'na katika Fratelli tutti”.

Mkutano huo utafanyika ana kwa ana na kupitia  mtandaoni, kwa utiririshaji wa moja kwa moja kupitia akaunti ya YouTube ya Baraza la Kipapa la Maendeleo ya Binadamu  katika Kiingereza na tafsiri inayopatikana kwa wakati mmoja katika Kiitaliano na Kihispania. Baada ya utangulizi wa Kardinali Peter Turkson, Mkuu wa Baraza la Kitawa kwa ajili ya Kukuza Maendeleo fungamani ya Binadamu. Zitafuata hotuba za Askofu Mkuu  Paul Gallagher, Katibu wa Vatican wa Mahusiano na Mataifa na Monsinyo Paul Tighe, Katibu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni. Katika Mkutano hu kwa mujibu wa maandalizi umegawanyika katika vikao viwili vya kina na hitimisho limekabidhiwa Sr. Alessandra Smerilli, Katibu wa muda Mpito wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu na Mjumbe wa Kitume wa Tume ya Vatikani COVID-19.

06 December 2021, 15:38