Tafuta

2021.12.04 Mkutano wa Papa na Maaskofu, Watawa, Mapadre na Walei 2021.12.04 Mkutano wa Papa na Maaskofu, Watawa, Mapadre na Walei  Tahariri

Kuwa Kanisa dogo hakumaanishi kutokuwa na maana

Utambuzi wa kuwa Kanisa dogo hakumaanishi kutokuwa na maana bali ni thamani kwa Makanisa.Ujumbe wa Papa kwa Kanisa Katoliki la Ugiriki ni tunu kwa wote.

ANDREA TORNIELLI

Papa Francisko akihutubia kwa Kanisa la Ugiriki Jumamosi iliyopita amezungumzia thamani za kuwa na udogo kwa sababu kuwa Kanisa moja dogo, kama ilivyo kesi ya zizi katoliki la Nchi hiyo, na ambalo linafanya kuwa ishara muhimu ya Injili. Mungu aliyetangazwa na Yesu alichagua wadogo na maskini na kujionesha katika jangwa na si katika majumba ya madaraka.

Kanisa, sio tu lile la Kigiriki ambalo limeombwa lisijivunie kuwafuatilia watu wengi, likiacha tamaa ya kidunia ya kutaka kuhesabu, ya kutaka kuwa muhimu katika jukwaa la dunia. Kuwa chachu ambayo huchachua ikiwa imejificha ndani ya unga wa ulimwengu kiukweli ni kinyume cha kujisalimisha katika maisha ya utulivu, kusonga mbele kwa nguvu ya hali. Njia iliyooneshwa na Papa ni ile ya uwazi kwa wengine, ya huduma, ya kusindikiza, ya kusikiliza, ya ushuhuda thabiti wa ukaribu na kila mtu na ambayo ni kinyume kabisa cha Kanisa linalijikunja lenyewe  na ambalo linapendezwa na udogo wake.

Mbele ya kubobea na ulimwengu na  ugumu ulio dhahiri ambao leo hii Wakristo wanakumbana nao katika kueneza imani, inawezekana kujifunga wenyewe huku tukijaribu kuunda jumuiya kamilifu, zinazojitenga na ulimwengu ili kuhifadhi kundi dogo au dogo sana, likingojea dhoruba nakupita huku likililia ya zamani ambayo hayapo tena. Au na hii pia ni hatari ambayo ipo sana leo hii, ya kujitolea kwa bidii sana katika mikakati ya kimisionari, kwa kujiaminisha na hakika kwamba kutangaza, kushuhudia na hata kuongoka si matunda ya Roho ambayo yanahitaji kutoa nafasi yake bali ni matokeo ya ujuzi wetu na ustadi wetu na kuwa wahusika wakuu. Kwa maana hiyo kuna hatari, kwa bahati mbaya inayojirudia katika zama za kidijitali, kwamba katikati ya uinjilishaji kuna anayejiinjilisha na uvumbuzi wake, badala ya Injili kuwa mhusika wake mkuu. Kuachia nafasi Mhusika Mkuu ndiyo maana ya kina ya kufanya uongofu, kama badiliko la mawazo katika mwanga wa Injili.

Kutokana na hilo, ndiyo udogo anaouzungumzia Papa Fransisko kwamba ni zawadi. Ni kufahamu kwamba bila Yeye hatuwezi kufanya lolote na kwamba ni Mungu anayetutangulia, anayeongoa, anayeunga mkono, na anayebadilisha. Na ufahamu huu pia ni wa thamani kwa Makanisa ambayo bado ni muhimu kiidadi, kuwa fursa inayotolewa na njia ya sinodi ambayo ndiyo kwanza imeanza na inaweza kuzisaidia jumuiya za Kikristo kujikomboa kutoka katika vifungo vya ukiritimba, ukleri, kujiaminisha katika miundo, ili kujenga au kujenga upya Kanisa kiungo  cha mahusiano ya binadamu ambamo ushuhuda hustawi.

06 December 2021, 14:28