Tafuta

Tahariri

Yule anayewaogopa ninyi hakuwatazama machoni!

Katika kituo cha kupokea na kurekodi wakimbizi cha Mytilene,katika kisiwa cha Lesbos,Papa Francisko dominika tarehe 5 Desembaakiwa katika hija yake ya kitume huko Ugiriki ametoa angalisho kwa wahusika wa ulimwengu kuwa na mshikamano mbele ya wale wanaotafuta maisha yenye hadhi.

ANDREA TORNIELLI

Mara baada ya miaka mitano Papa ametaka kurudi katika kisiwa hiki kutembelea wahamiaji na wakimbizi. Mwanzoni mwa hotuba yake alinukuu maneno yaliyotamkwa hapa na patriarki wa Constantinople Bartholomeo I mnamo 2016: “Yule anayekuogopa hakutazami machoni. Yule anayewaogopa ninyi hajaona nyuso zenu. Yule anayewaogopa hawaoni watoto wenu. Anasahau kwamba hadhi na uhuru unashinda hofu na migawanyiko. Anasahau kwamba uhamiaji ni shida ya ulimwengu”.

Maneno hayo ya Patriaki ambayo Papa Fransisko amependelea kuyarudia yanatusaidia tusisahau, na kugeukia upande mwingine. Daima tunajifunza kwa upya kwamba watu waliopo hapa, wanaobisha kwenye mipaka yetu, sio wahamiaji au wakimbizi, sio idadi, bali ni watu.

Tujifunze kuwaangalia machoni. Ni wahanga wa vita, chuki, mabadiliko ya tabianchi, wasafirishwaji haramu wa binadamu, kwa njia ya wanasiasa wanaowatumia kama bidhaa. Badala ya kukengeuka au kujigawanya sisi wenyewe kwa kutumia hofu, sisi sote tujaribu, kwa pamoja, kuhoji mfumo unaosababisha ukosefu wa usawa na kuchochea vita.

05 December 2021, 15:18