Papa Francisko:Lebanon ina ujumbe mzuri wa kuweza kuamka tena na kuanza upya!
Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu FranciskoAlhamisi tarehe 25 Novemba 2021 amekutana na Waziri Mkuu nchini Lebanon Bwana Najib Mikati, ambaye mara baada ya mazungumo yao amewakilisha familia yake katika ukumbi wa Clementina na kubadilishana zawadi. Mara baada ya kubadilisha zawadi hizo Papa amesema maneno machache kuwa Nchi ya Lebanon inajieleza ujumbe wake wa ahadi na kwa maana hiyo lazima kuupambania.
Baba Mtakatifu ameongeza kusema kwamba Lebanon inapitia vipindi vibaya sana na vigumu na amewakikishia sala zake, ukaribu wake na jitihada zake ili nchi hiyo iweze kuwa na nguvu za pamoja katika kusaidia nchi hiyo ipata kuamka tena. Katika hilo Papa amekumbusha kifungu cha sehemu ya Injili ambayo Yesu alikwenda katika nyumba ya Gairo, aliyekuwa na mtoto amekufa na kumshika mtoto akisema “ hamka” na kwa kufananisha na hiyo amesema “Bwana anashika mikono ya Lebanon na kusema “amka”.
Kabla ya kuagana, Papa Francisko amewaalika wote waliokuwamo kufanya muda mfupi wa sala ya ukimya na baadaye Waziri amekwenda kukutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin huku akisindikizwa na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican kwa ajili ya Uhusiano na Ushirikiano na Nchi. Katika mchakato wa mazungumzo yao kwa mujibu wa taarifa za Msemaji wa vyombo vya habari Vatican, wamesisitiza juu ya uhusiano mwema wa kihistoria uliopo kati ya Vatican na Lebanon na umuhimu wa nafasi ya Kanisa katoliki katika shughuli zake zinazoifunika nchi hiyo. Vile vile wamegusia suala la sasa ambao watu wa Lebanon wanaishi hasa kwa mtazamo wa mgogoro wa kisiasa na hali za kijamii, kiuchumu, wakiwa na matashi mema kwamba haki na ulazima wa kuwa na magezuo na msaada wa Jumuiya ya kimataifa unaweza kwa dhati kusaidia kutatua matatizo yaliyo jitokeza kwenye Nchi hiyo ya Mwerezi.
Na hatimaye viongozi hawa wamezungumzia juu ya umuhimu wa kuhamasisha mukatadha wa uraia wa kila Mlebanon na kusisitiza umuhimu wa kuishi kwa amani ili nchi ya Lebanon iendelee kuwa ni jumbe wa amani na udugu ambao unahitajika katika nchi zote za Mashariki ya Kati. Ikumbukwe hata hivyo katika kubadilishana zawadi, WazirioMkuu amemzawadia Papa Francisko Picha ya Kanisa la Kimelkita la Mtakatifu Salvatore ambalo limeharibiwa vibaya wakati wa mlipuko wa moto mnamo tarehe 4 Agosti 2020. Picha ya ya Papa aliyomzawadia Waziri Mkuu inaonesha shamba la mizabibu, ambao kuna andiko:“ Tunda la mizabibu na kazi ya binadamu iwe kwetu kinywaji cha wokovu”; Kikasha ndani mwake chenye mkusanyiko wa hati za kipapa ambazo ni ujumbe wa amani wa wa 2021, Hati ya Udugu wa Kibinadamu na Kitabu kuhusu Statio Orbis la 27 Machi 2020, lilichoandaliwa na LEV.