Tafuta

Bwana Jorge Eduardo Román Morey, Balozi mpya wa Perù tarehe 22 Novemba 2021 amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Bwana Jorge Eduardo Román Morey, Balozi mpya wa Perù tarehe 22 Novemba 2021 amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. 

Bw. Jorge Eduardo Román Morey, Balozi Mpya wa Perù mjini Vatican

Bw. Jorge Eduardo Román Morey, Balozi mpya wa Perù mjini Vatican. Alizaliwa tarehe 13 Januari 1954 huko Callao nchini Perù, ameoa na kubahatika kupata watoto watatu. Ni kiongozi ambaye kwa muda mrefu ametoa huduma yake katika Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa. Amewahi kuwa Balozi wa Perù kwenye Jamhuri ya Watu wa Dominican na Bolivia.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 22 Novemba 2021 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Jorge Eduardo Román Morey, Balozi mpya wa Perù mjini Vatican. Alizaliwa tarehe 13 Januari 1954 huko Callao nchini Perù, ameoa na kubahatika kupata watoto watatu. Ni kiongozi ambaye kwa miaka mingi amekua akitoa huduma yake katika Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa. Amewahi kuwa Balozi wa Perù kwenye Jamhuri ya Watu wa Dominican na Bolivia.

Kati ya mwaka 2013 hadi mwaka 2016 alikuwa ni Balozi wa Perù nchini Ugiriki na Balozi asiye mkazi nchini Albania na Bulgaria. Kati ya mwaka 2016-2018 aliteuliwa kuwa ni Balozi wa Perù nchini El Salvador na Balozi asiye mkazi nchini Belize. Amewahi pia kuwa ni Mkurugenzi mkuu wa Protokali na Dhifa za Kitaifa nchini Perù kati ya mwaka 2012 hadi mwaka 2013. Akateuliwa tena kwenye nafasi hii kati ya mwaka 2018 hadi mwaka 2021. Tarehe 22 Novemba 2021 amewasilisha nyaraka zake kwa Baba Mtakatifu Francisko kama Balozi wa Perù mjini Vatican.

Balozi Perù
22 November 2021, 14:09