Tafuta

Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP26 Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP26 

COP26,Glasgow.Changamoto na hatari kwa viongozi wa dunia

Dominika tarehe 31 Oktoba umefunguliwa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa wa COP 26 huko Glasgow,Scotlanda hadi tarehe 12 Novemba na kuendelea na mchakato ambao utaendelezwa na wanadiplomasia zaidi kutoka nchi 200,ambao wanajikita kutafuta namna ya kuthibiti ongezeko la joto ulimwenguni.Wawakilishi wa Vatican News huko Glasgow wanatoa habari.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika tukio la sasa linaloendelea tangu Dominika tarehe 31 Oktoba ambapo ulifunguliwa rasimi mkutano wa Umoja wa Mataifa wa COP26 huko Glasgow nchini Scotland, wawakilishi wa Vatican Francesca Sabatinelli na Marine HenriotKwa mujibu wao wanasema kuwa awali ya yote walifunguwa kwa ukimya, ili kukumbuka waathiriwa wa Uviko, kwa kuona viongozi karbu 200 wa dunia ambao wanaomba mabadiliko ya kweli ambayo ni muhimu na dhata ambayo hayajawahi kuwapo hapo awali.

Ikiwa mkutano wa Glasgow utashindwa, kila kitu kitashindikiza, alisema hayo mkuu wa nyumba Boris Johnson, akielezea kwa hisia yake na ushirikishaji kwa wajumbe wote wa  COP 26  na kwamba kwa hakika mkutano huo uwe mchakato wa kutfuta suluhishi za dhati.  Kwa maana hiyo wiki mbizi hizi, viongozi wa kisiasa ambapo miongoni mwake kuna Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Antonio Guterres, Rais wa Tume ya Ulaya Bi  Ursula von der Leyen na kwa upande wa Vatican, anawakilisha Papa, Katibu , Kardinali Pietro Parolin, pamoja na wanasiasa, mashirika yasiyo ya kiselikali, wawakilishi wa kidini, wanaharakati, wote hao wakitaka kukabiliana kwa hakika na msimamo wa kisiasa kuhusu mabadiliko ya tabianchi ulimwenguni.

Katika COP21 huko Paris  nchi zilishoshiriki zilikuwa zimetaka na kutoka ahadi ya kuzuia uongezeko la joto kwa kiwango cha sayari  chini ya nyuzi  2°C kulingana na viwango vya viwanda na kuendelea na matendo ili kufikia joto a 1,5°C, na ulazima wa kupunguza hatari na matokeo ya mabadiliko ya tabianchi. Licha ya hayo yote, kwa mujibu wa wasomi wamebainisha kwamba ahahadi hizo hazikuweza kutimiswa na hasa kwa miaka ya mwisho ambayo imeona ongezeko la gasi chafuzi na ambayo inasabababisha kuongezeka kwa joto la dunia.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mnamo 2020 joto limeongezaka zaidi baada hata baada ya kupunguza shughuli za kiuchumi kutokana na janga, kwa maana hiyo inabidi kubaki katika kiwango ambacho hakizidi 1,5°C kulinganisha kabla ya mapinduzi ya viwanda  (kati ya  1850 na 1900), na upunguzaji wa hewa chafuzi unapaswa ufikie asilimia 7 kila mwaka kulingana na kiwango cha sasa kwa kufikia 2030 kama wanavyoeleza wataalam. Katika miaka 10 hii ni muhimu sana kwani inahitaji sera za kisiasa za kweli katika kujikita kwenye matendo ya kweli na nchi lazima siweke juhudi kwa kiasi kikubwa.

Sauti kutoka Kusini mwa dunia:  Kati ya wa kwanza kuzungumza kwa maana ya nchi za Kusini mwa dunia alikuwa ni Waziri wa Barbados Mia Mottley ambaye aliwaalika nchi za Magharibi kutunza ahadi zao. Kwa wote ambao wana macho ya kuona, maskini ya kusikia na mioyo ya kuhisi, ili kuweza kuishi tunahitaji kupunguza joto chini ya +1,5°C, na nyuzi 2°C zitakuwa ni kifo kwa watu wa Antigua na Barbuda, Maldive, Fiji, Kenya au Msumbiji, Samoa na Barbados”amesisitiza.  Kwa maana hiyo ni wazi kwamba Jamii ndogo ndogo za mahalia zina mchango mkubwa katika kuendeleza ajenda ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi. COP26 inahimiza ushirikishwaji wa vijana katika vita hii dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, na kwa maana hiyo  wito umeitikiwa na vijana wanashiriki miradi mbalimbali. Na hata hivyo Bwana Boris alirudia msemo w Greta kijana mwanaharakati kuhusiana na Blabla bila kutekeleza malengo. Na kwa nchi au mataifa yaliyoendelea yawasaidie nchi maskini kwani hawahusiki pakubwa kuchafua mazingira lakini ndio wanaobeba gharama za athari zake.

Hata hivyo katika ufunguzi wa Mkutano huo, kuna uwakilishi ndogo wa Nchi ambazo zinaathiriwa sana, kwa namna ya pekee kutokana na chanjo ya lazima na gharama kwa namna ya pekee ilivyo gharama na malazi. Moja mambo yaliyo ya  moto katika mkuntano huu wa COP 26 ni ahadi ya Nchi za Magharibi ya kuweze kutoa bilioni 100 za dola ya kimarekani kusaidia kwa nchi zilizo maskini, ambazo wala hazihusiki na uongezekaji wa joto ulimwenguni,lakini licha ya hayo wanateseka zaidi. Ahadi hiyo ilitolewa katika mkataba wa Paris mnamo 2015 na ambayo haikutimizwa, kwa kuongeza mgogoro mkubwa wa kuwa na imani kati ya Nchi za Kaskazini na Kusini mwa dunia.

02 November 2021, 16:55