Tafuta

Askofu mkuu Bienvenu MANAMIKA BAFOUAKOUAHOU, Jimbo kuu la Brazzaville, nchini Congo Askofu mkuu Bienvenu MANAMIKA BAFOUAKOUAHOU, Jimbo kuu la Brazzaville, nchini Congo 

Askofu Mkuu Bienvenu Manamika Bafouakouahou Jimbo Brazzaville

Askofu mkuu mteule Bienvenu M. B wa Jimbo kuu Katoliki la Brazzazille nchini Congo alizaliwa tarehe 16 Oktoba 1964 huko Brazzaville. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 29 Agosti 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo la Kinkala, Congo. Mwaka 2013 akateuliwa kuwa Askofu wa Dolise na Mwaka 2020, Askofu Mwandamizi, Jimbo kuu la Brazzaville.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasililishwa kwake na Askofu mkuu Anatole Milandou wa Jimbo kuu Katoliki la Brazzazille nchini Congo la kutaka kunga’tuka kutoka madarakani. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteua Askofu mwandamizi Bienvenu Manamika Bafouakouahou wa Jimbo kuu Katoliki la Brazzazille nchini Congo kuwa Askofu mkuu wa Jimbo Katoliki la Brazzaville. Askofu mkuu mteule Bienvenu Manamika Bafouakouahou wa Jimbo kuu Katoliki la Brazzazille nchini Congo alizaliwa tarehe 16 Oktoba 1964 huko Brazzaville, nchini Congo.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 29 Agosti 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo la Kinkala, Congo. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 24 Mei 2013 akamteuwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Dolise, Congo na kuwekwa wakfu tarehe 25 Agosti 2013. Ilipogota tarehe 18 Aprili 2020, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu mwandamizi wenye haki ya kurithi Jimbo kuu la Brazzaville, Congo. Na Jumapili tarehe 21 Novemba 2021, Baba Mtakatifu amemteuwa kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Brazzaville.

Brazzaville
21 November 2021, 15:49