Tafuta

2021.10.22Sr  Lucia Ripamonti ametangazwa kuwa mwenyeheri tarehe  23 Oktoba 2021 huko Brescia Italia. 2021.10.22Sr Lucia Ripamonti ametangazwa kuwa mwenyeheri tarehe 23 Oktoba 2021 huko Brescia Italia. 

Mwenyeheri mpya Sr. Lucia Ripamonti ni roho iliyouzwa kwa upendo

Leo katika Kanisa la Brescia ametangazwa mwenyeheri Sr. Lucia Ripamonti katika Misa iliyoongozwa na Kardinali Semeraro,ambaye amesema kuwa aliishi katika ukimya na urahisi wa Kiinjili kwa kupata kila kitu hata wakati wa kukemewa na kusahihishwa alikuwa mvumilivu na hata wakati wa kunyenyekezwa aliendelea katika njia ya utakatifu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Upendo, ukarimu na kujitoa vilivikuwa ni saifa ya maisha ya Sr. Lucia Ripamonti,  aliyetengazwa Mwenyeheri siku ya Jumamosi tarehe 23 Oktoba 2021 wakati wa Misa iliyoongozwa na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mchakato wa kuwatangaza wenye heri na watakatifu kwa niaba ya Papa huko Brescia nchini Italia. Kardinali Semeraoi amesema katika mahubiri yake akikimbuka yale maneno yaliyosemwa na watu juu yake kwamba alikuwa mnyenyekevu sana. Yeye mwenyewe alizoea kusema kuwa jambo bora kabisa kwa ajili ya roho ni kufanya kile ambacho Mungu anataka kwake na kwa hakika ujenzi wake wa kiroho umesaidia kwa kina na msingi wa unyenyekevu. Sr. Lucia hakuwa ni mtu wa maneno bali alikuwa akiyaweka katika matendo na ambayo zaidi ya kuwa zoezi la kishujaa la fadhila, sauti ya ushuhuda ni ya umoja  na kwamba alikuwa anafurahia kwa sababu ndiyo njia ambayo angeweza kuishi mafichoni.

Jitieni nira yangu, kwa maana nira yangu ni tamu na uzito wangu ni mwepesi. Mwenyeheri Lucia Ripamonti alijitwika nira hii: akikubali kwa ukarimu wito wa Bwana wa maisha ya kuwekwa wakfu, ambapo alichagua kujituma mwenyewe na kubaki mahali pa mwisho; kujitoa kwa Mungu hadi kufika kusema juu yake kwamba "aliuzwa katika upendo". Vile vile Sr Lucia alijiachilia katika mapenzi yake na hii hasa katika siku za uchungu za ugonjwa wake alifanya mazoezi ya utii kwa uaminifu na utulivu. Huo uliwezekana  kupatikana kwa jirani yake hadi kufikia hatua ya kujisahau kwa sababu alikuwa anasema “ikiwa kweli tunataka kuifanya nira ya Kristo kuwa nyepesi, hakika hatutatumia njia ya kuibeba vibaya au kuitikisa mabegani mwetu. Ikiwa tunaitamani, kama alivyoifafanua, kwamba ni tamu na nyepesi, ambayo ni, chanzo cha nguvu, uaminifu, maisha,ni  lazima tuibebe kwa uaminifu, uthabiti, uelewa, ambao ndiyo kusema kwa moyo wetu wote.

23 October 2021, 17:05