Tafuta

Kard.Gambetti:Mfuko mpya wa Fratelli tutti,Vatican kwa ukuaji endelevu na ubinadamu mpya

Mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro Kardinari Mauro Gambetti ameeleza chanzo cha muundo mpya unaojikita katika Waraka wa Papa.Utafunguliwa kwa ajili ya mafunzo ya vijana na kujenga mtandao na kufanya mpango kuhusu mazingira,kisiasa, kiuchumi na ujasiriamali.Bila maono shirikishisiyo rahisi kuuishi ulimwengu.

Na Sr. Angella Rwezaula - Vatican.

Kardinali Mauro Gambetti, mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, amezindua rasimi mfuko uitwao Fratelli tutti, yaani Wote ni ndugu  akia  katika chumba cha Seneti mbele ya Waziri wa Afya, Roberto Speranza. Huo ni  uzinduzi msingi mpya wa Vatican uliojitoa kwa  ajili ya maandishi ya hivi karibuni ya Waraka wa Papa Francisko. Kardinali amesema: "Hii ni fursa nzuri kwangu kutoa muhtasari wa ndoto ambayo iko karibu kutimia kuzungukia  Kanisa kuu la Mtakatifu Petro na nguzo zake ambazo ni mfano unaokumbatia ulimwengu na ndio kizingiti cha wale wanaotafuta wa kweli, uzuri na uadilifu. Ndoto iliyokuzwa tangu nikiwa Assisi na ambayo sasa inashirikishwa hasa na Padre Francesco Occhetta, mshiriki wangu wa karibu na baadhi ya Mabaraza ya Kipapa yanazoshughulikia masuala yanayohusiana na malengo yetu".  Aidha amesema kuwa " Kupitia Mfuko utakaoitwa Wote ni Ndugu tungependa kuchangia katika kubuni na kutekeleza ubinadamu mpya,  kukuza mchango wa kila mmoja kwa njia ya sinodi kulingana na maeneo yao ya kujitolea na uwezo" .

Katika maelezo yake Kardinali Gambetti amesema: "Siasa na uchumi, ubora wa uhusiano wetu wa kijamii na kibinafsi ​​vinahitaji ubinadamu endelevu, Papa Francisko angeweza kusema, ni kuweka wazo juu ya haki  kijamii, hali ya mshikamano, ujenzi kwa ajili ya faida kwa wote, ukuaji wa kibinadamu na endelevu, hali za uwazi ambazo zinapendelea na kuwa na shauku ya kuwa jumuiya moja, ambayo inapitia maoni kwa maana hii  na hivyo ni muhimu kuandiaka kwa upya neno la mwanadamu ambalo linatufanya tutambue hata wakati hatujulikani kibinafsi na tunaruhusu tuite kwa jina: kaka yangu na dada  yangu".

Kwa jinsi hiyo mmfuko ambao utazaliwa kutokana na mfuko wa Fabbrica di San Pietro utakuwa na  maeneo makuu matatu ya utendaji: eneo linalohusiana na sanaa, hasa takatifu, ambalo litashughulika na mafunzo na kuhusu mazungumzo na watu, tamaduni na dini. Litakuwa na zana za utelezaji, ya uwazi katika huduma ya watu na wanataka kuwekeza katika watu kwa  kuwapa nafasi, kuwaruhusu kukutana tena, kujenga jamii ya mawazo na maisha na kushiriki katika ulimwengu kama alivyofanya kizazi cha Mariella Enoc, Rais wa Jamhuri Italia na, hata kabla ya hapo, kizazi cha baba zao. Kuhusiana na imani yao na kiroho walianzisha ushirikiano na kukuza ujuzi wao kama zawadi kwa ajili ya huduma ya wote.  Wataanda matukio na michakato ya safari ya uzoefu na kuzungukia katika Kanisa Kuu Katoliki kwa kuhamasisha uwajibishaji wa maadili ya uhuru, usawa na undugu, amefafanua mkuu wa Kanisa Kuu la Mtakatifgu Petro Kardinali Gambetti.

21 October 2021, 17:06