Tafuta

Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa linaloratibu shughuli za kimisionari amejikita kuelezea wafisu wa Pauline Jaricot, mwanzislishi wa matendo ya kimisionari. Katibu mkuu wa Baraza la Kipapa linaloratibu shughuli za kimisionari amejikita kuelezea wafisu wa Pauline Jaricot, mwanzislishi wa matendo ya kimisionari. 

Siku ya kimisionari ulimwenguni 2021:hatuwezi kunyamaza tulichoona na kusikia

Alhamisi tarehe 21 Oktoba jijini Vatican katika ukumbi wa waandishi wa habari umefanyika mkutano kwa waandishi habari katika kuwakilisha Siku ya Kimisionari ulimwenguni 2021,inayoongozwa na mada “hatuwezi kunyamaza kile tulicho kiona na kusikia.Monsinyo Giampiero Dal Toso, mkuu wa Baraza la Kipapa linaloratibu shughuli za kimisionari amejikita kuelezea wasifu wa Pauline Jaricot, mwanzilishi wa matendo ya kimisionari.

Alhamisi tarehe 21 Oktoba 2021, Vatican umefanyika mkutano kwa waandishi habari katika kuwakilisha Siku ya Kimisionari ulimwenguni 2021, inayoongozwa na mada “ hatuwezi kunyamaza kile tulicho kiona na kusikia. Katika uwakilishi huo, Monsinyo. Giampietro Dal Toso, Rais wa Shughuli za Kipapa za Kimisionari (PMS), na Katibu Msaidizi wake kutoka wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu wametoa maelezo yao kuhusu siku hiyo. Monsinyo Dal Toso yeye ametaka kutoa mtazamo zaidi wa Siku ya Kimisinonari ulimwenguni kuelekea  mwaka 2022 ambao wataadhimisha katika ulimwengu wa kimisionari miaka 400 ya Shirika na miaka 200 ya kuanzishwa kwa mfuko wa kwanza wa shughuli za kimisionari na shughuli za  (Propaganda Fidei) kueneza imani na miaka 100 tangu kutangazwa kwa moja ya mihimili mnne ya shughuli zao. Katika muktadha huo wataadhimisha huko Lione nchini Ufaransa mnamo tarehe 22 Mei 2022  kutangazwa Mwenyeheri  Pauline Jaricot, mwanzislishi wa matendo ya kimisionari.

Akifafanua juu ya wasifu huo maalum,  walikuwa wameanda kijitabu cha historia yake na wawapatia wandishi wa habari katika ukumbi huo. Akianza kueleza juu ya kijana huyo wa Leon aliyefariki mnamo 1862 amesema ni kijana mwamke. Mara nyingi “Wanazunguzwa kwa upana katika nyakazi hizi juu ya uhamasishaji wa mwanamke katika Kanisa. Mtazamo wa kihstoria , unaonesha kuwa mwanamke amekuwa mstari wa mbele katika maisha ya Kanisa na huo ni mfano ambao unajionesha hai na kwa hakika ambao unapata nafasi katika Kanisa na labda kwa sababu unatokanana mwanamke” amesisitiza. Lakini ameongeza kusema kwamba  isishauliwe kuwa katika karne hiyo hiyo ya 19 kulitokea chanuo  kwa kasi kubwa ya mashirika ya kitawa ya wanawake ambayo yalijikita na masuala ya shule, utunzaji wa watoto yatima, katekesi, utume hospitalini: na katika muktadha huo ndipo tunamwona  mwanamke ambaye lakini hakuingia katika konventi!

Pauline alikuwa mmisionari mkubwa. Inaonekana kuwa ni muhimu kutaja kwamba ufunguo wa kumwelewa mwanamke huyo ulikuwa wasiwasi wake wa kimisionari. Kazi ya Uenezaji wa Imani, hata kabla ya hapo maombi yake yalizunguka kwa ajili ya utume, Rozari iliyo hai, jaribio lake la kujenga kiwanda bora cha kukidhi mahitaji ya kiroho na kukuza utu wa watenda kazi wa wakati huo iliyofanywa ili kuinjilisha mazingira ya Ufaransa na kuunga mkono utume katika kipindi cha nguvu ya ukristo baada ya mapinduzi ya Ufaransa. Kwa ufupi, inaweza kusemwa kwamba alitaka kushiriki katika utume katika nchi za mbali ili kuinjilisha  pia katika nchi jirani.

Ili kutumia kile alichosema mwenyewe, Pauline ni mbegu ambayo mti mkubwa ulizaliwa. Yeye ni wa kipekee sio tu kwa utakatifu wa maisha, bali pia kwa ukubwa wa matunda ya kazi yake. Alianzisha harakati ya kweli ya kimisionari ya kiroho shukrani kwa Kazi ya Kueneza Imani, ambayo ilikua na kuenea haraka pia kwa sababu ilijengwa kwa mfumo ulio rahisi lakini mzuri: vikundi vya watu 10, ambao walikusanyika katika sehemu  100 na baadaye katika elfu moja na wahusika katika kila ngazi. Hata mwaka mmoja baadaye matendo hayo yalitambuliwa na Papa Pio VII na mnamo 1825 Mfalme wa Ufaransa aliichukua jukumu la kuwekea ulinzi wake na zawadi ya faranga 4,000. Ikiwa mnamo 1822 alikusanya faranga 22,915, mnamo 1838 alikuwa tayari 1,343,000 na miaka miwili baadaye milioni 2.5, ambayo ni 45% ilikusanywa nje ya Ufaransa. Ikiwa nakala ya taarifa ya Matendo hayo mnamo 1825 iliuza nakala 10,000, mnamo 1830 tayari kulikuwa na 40,000, bila kuhesabu tafsiri.

Kwa mujibu wa Monsinyo Forbin-Janson alisema kuwa Pauline alikuwa wa aina yale ua kutumia mtindo huu kwa Kazi ya  kuchangia Utume wa Umisionari. Aidha amesema kwamba anaweza kutamka  bila kusita kwamba mchango wa Kazi za utume , ambao ulitokana na fahamu hii, ulikuwa muhimu kwa historia ya utume wa kimisionari  katika karne ya kumi na tisa na ishirini, kwa sababu walihusika na msingi wa waamini Wakatoliki na kuwafanya wafahamu utume huo. Lakini hii si historia tu, ikiwa unafikiri kwamba katika mwaka huu wa shughuli ya  Kueneza Imani imeunga mkono  kwa  makanisa 893 katika eneo la utume wa kimisionari kwa mchango wa gharama za sasa na imewekeza zaidi ya dola milioni 10 kwa ajili ya malezi ya makatekista wakati katika mfuko wa  Mtakatifu Petro Mtume ilifadhili mafunzo ya waseminari 76, 541 katika seminari 746.

Wote waliobatizwa wameitwa kwenye utume kama ishara ya shukrani na furaha, ambayo huzaliwa kutokana na uzoefu wa upendo wa Mungu. Katika uwasilishaji wa Siku ya 95 ya Kimisionari Duniani2021 naye , Kardinali Luis Antonio Tagle, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, amechukua kifungu cha  kauli mbiu ya Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko kwa  2021. “Hatuwezi kukaa kimya juu ya kile tulichoona na kusikia”  ambacho kitahusisha majimbo yote na mipango, mikutano yote. “Kukutana na Mungu ambaye amegusa mioyo yetu na ambaye ametenda kazi za ajabu hatuwezi kuhifadhiwa kwetu wenyewe”, anathibitisha Kardinali, akituhimiza kushiriki upendo tuliopata kama zawadi kwa wengine. Watu wanaonya kwamba ikiwa hatushirikishi imani, ikiwa tunaiweka katika kikundi kidogo, inakuwa biashara ya wasomi na inadhoofika, kufikia mataifa yote, kijiografia na kuwepo nyakati za kuinjilisha ukristo ambapo kwanza kabisa ni muhimu kuomba, kwa sababu imani ni zawadi ya Roho Mtakatifu. Injili inatufundisha kupenda, hata katika ishara ndogo za kila siku na mambo madogo.”

22 October 2021, 16:46