Tafuta

2021.10.21 Zawadi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Slovakia kwa Papa, kwa ajili ya mahitaji ya vituo vya afya ili kusaidia wenye kuhitaji,vilivyo wasilishwa tarehe 21 Oktoba jijini Vatican. 2021.10.21 Zawadi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Slovakia kwa Papa, kwa ajili ya mahitaji ya vituo vya afya ili kusaidia wenye kuhitaji,vilivyo wasilishwa tarehe 21 Oktoba jijini Vatican. 

Rais wa Slovakia ametuma zawadi kwa Papa:vifaa vya kujikinga na Uviko

Katika kuonesha moyo wa shukrani kwa ajili ya zira ya kitume ya Papa Francisko nchini Slovakia,Rais wa Serikali hiyo Bi. Zuzana Čaputová amewezesha kutma zawadi kwa Papa kwa kufikisha vifaa vya kimatibabu ili viwekwe kwenye miundo ya vituo vya Afya vya Vatican kuwasaidia wenye kuhitaji zaidi.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Mashine moja ya kupumulia mapafu, zaidi ya barakoa 100,000 yenye tisshu tata  na vifaa vingene vingi vya usafi ambavyo vinaweza kutumika kwa ajili ya kuzuia janga la UVIKO-19 na kuwasadia walio wadhaifu zaidi, maskini na wagonjwa katika miundo ya kiafya na vituo vingine vya kijamii ambavyo vipo chini ya mamlaka ya Vatican;  Ndiyo zawadi ambayo Alhamisi tarehe  21 Oktoba 2021, vimefika kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Slovakia Bi Zuzana Čaputová kama ishara ya shukurani kwa ziara ya kitume iliyotimizwa na Baba Mtakatifu Francisko hivi karibuni nchini humo.

Aliyetoa taarifa hizo ni Balozi wa Jamhuri ya Slovakia anaye wakilisha nchi yake jijini Vatican na katika Jimbo la Kijeshi la Malta. Katika fursa hiyo Balozi wa Jamhuri ya Slovakia, aliyeko Vatican, Marek Lisánsky, alikutana na Katibu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, ambaye pia amepongeza ishara hiyo nzuri kwa Rais wa Jamhuri ya Slovakia kwa niaba ya Papa kwa kuwa na mtazamo wa kujali watu ambao ni wadhaifu zaidi na waliobaguliwa.

22 October 2021, 17:15